Ni kampuni gani inaweza kutengeneza IDs za teknolojia ya smart card Tz? tusilaumu bila kujua ukweli wa jambo. Zabuni si ilitangazwa, mbona wawekezaji wa ndani waliingia mitini?
Unajua hata hao wanaoleta maneno sasa wanajua kwamba hakuna hata kampuni moja ya kitazania yenye uwezo huo. Wanachokasirikia ni kukosa uwakala (udalali) ambao unsababisha kupanda kwa bei na wao kujipatia cha juu kwa mfano ule wa mikataba ya ununuzi wa rada na ndege ya rais. Baada ya kuikosa kandarasi hiyo ya uwakala ndo sasa hasira zimegeukia kwa kampuni hii ya Malaysia na kunyooshea vidole kwa JK na Membe. Utoto mtupu!