Malaya jela kwa kuuza miili yao lakini mafisadi wanauza mali zetu wanaachwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malaya jela kwa kuuza miili yao lakini mafisadi wanauza mali zetu wanaachwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUMBIRI, Apr 26, 2012.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Malaya jela kwa kuuza miil yao[SUP]1[/SUP]
  WAKAZI wawili wa Dar es Salaam, wamehukumiwa kifungo cha wiki mbili jela baada ya kukiri shtaka la kufanya biashara ya kuuza miili yao kinyume cha sheria. Washtakiwa hao ni Aisha Nassoro (20) na Upendo Julius (39), wote wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive,kujibu shtaka lililokuwa likiwakabili. Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi, alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Aprili 23, mwaka huu eneo la Buguruni.

  Magodi alidai siku ya tukio majira ya usiku eneo hilo, washtakiwa walikamatwa na polisi waliokuwa katika doria wakifanya biashara ya kuuza miili yao, huku wakijua ni kinyume cha sheria. Washtakiwa walikiri shtaka linalowakabili na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William Mutaki, aliwahukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha wiki mbili jela kama fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.

  Katika hatua nyingine, wakazi watatu wa Dar es Salaam wamefikishwa katika mahakama hiyo kujibu shtaka la kupiga debe na kubughudhi abiria katikati ya jiji. Watuhumiwa hao ni Said Salum (19), Rajae Ismail (28) na Damian George (25).

  Magodi alidai siku ya tukio Aprili 23, mwaka huu katikati ya jiji washtakiwa walikamatwa na polisi wakiwafanya vurugu na kubughudhi abiria waliokuwapo kituo cha daladala, huku wakijua ni kinyume cha sheria.

  Washtakiwa walikana shtaka na Hakimu Mutaki aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 7, mwaka huu itakapotajwa tena na washtakiwa walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini bondi ya Sh100,000 kila mmoja


  Source:
  [SUP]1[/SUP]
  Malaya jela kwa kuuza miili yao
   
 2. G

  Gayo junior Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! Fisadi hafungwi
   
 3. N

  Nabwada Senior Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tena haya mambo yananikera sana,mtu aliyefanya makosa anajulikana kabisa alafu anaachwa,wanaacha kumkamata aliye7bisha mpaka hao wadada wakawa macd,tazama mtu ameiuza Bandari ya Mtwara bila hata kutupatia taarifa hajashikwa.Hiv Mlima KILIMANJARO unaweza kuuzwa pasipo Wachaga kujua?,Wanakusini wenzangu hizi ni dharau za dhahiri.
   
Loading...