Malawi yateketeza tani 2 za meno ya tembo kutoka Tanzania

mshumbusi

JF-Expert Member
Oct 24, 2011
457
232
Malawi yatekeza tani 2 za pembe kutoka Tanzania

Malawi imeteketeza tani 2.6 ya pembe za ndovu ambazo zilinaswa na maafisa wa usalama zikitokea nchi jirani ya Tanzania.

Meno hiyo 781 ya tembo ambayo inakisiwa kugharimu takriban dola milioni tatu ilipatikana baada ya operesheni dhidi ya ulanguzi na uwidaji haramu.

Mkurugenzi wa idara inayosimamia mbuga za wanyama pori Bright Kumchedwa, amesema kuwa hiyo ni ishara ya kwanza na dhabiti kutoka kwa Malawi kuwa haitaruhusu tena ardhi yake kutumika kulangua bidhaa za uwindaji haramu.

Hafla ya hiyo ya kihistoria ilifanyika katika eneo la Mzuzu kaskazini mwa nchi hiyo.

Kenya inatarajiwa kutekeleza hatua kama hiyo mwishoni mwa mwezi huu.

Kenya imekamata takriban tani 120 ya meno ya ndovu.

=====================
Malawi on Monday burned 2.9 tons of ivory smuggled from Tanzania after a cross-border dispute over whether the elephant tusks should be saved as legal evidence against poachers.

Tanzania had succeeded in delaying the burning since September, but a court in Malawi this month ordered wildlife authorities to publicly destroy the 781 pieces of ivory — valued at nearly $3 million.

“This is a milestone for Malawi. We will not allow the country to be exploited as a market of this illegal trade,” Bright Kumchedwa, director of Malawi’s parks and wildlife department, told AFP.

“We want demonstrate to the world that the country is committed to eradicating wildlife crime.”

The stockpile was set alight outside a nature sanctuary in the small northern city of Mzuzu, 480 kilometres (300 miles) from the administrative capital Lilongwe.

Watched by police and court and wildlife officials, the fire sent a billow of smoke into the sky.

Two Malawian siblings were last year fined $5,500 for their part in trafficking the tusks, which were intercepted by Malawian customs officials in 2013.

Tanzania had won a three-month court order to postpone the burning, but did not apply for a further delay, Kumchedwa said.

Malawi has another 4.4 tons of stockpiled ivory that it plans to destroy.

In March last year, Kenya set fire to 16.5 tons of ivory, which conservationists said then was the largest-ever stockpile burnt in Africa.

Wildlife experts say poaching has halved Malawi’s elephant population from 4,000 in the 1980s to just 2,000 now.

“Malawi is vulnerable to exploitation by traffickers operating between the country and the surrounding countries of Zambia, Tanzania and Mozambique,” Jonathan Vaughan, director of Lilongwe Wildlife Trust, told AFP.

“It is being targeted by both poachers and traffickers.”

Malawi is widely considered a weak link in the fight against illegal ivory trade due to graft, weak wildlife legislation and poor law enforcement.

Ivory is highly sought for jewellery and decorative objects and much of it is smuggled to China and Thailand, where many wealthy shoppers buy ivory trinkets as a sign of financial success.


Source:
discovery.com
 

Attachments

  • 1457989770372.jpg
    1457989770372.jpg
    34.8 KB · Views: 48
Aisee afadhali wametusaidia kuyachoma maana yangekamatwa hapa wangekuwa wanauziana taratibu mpaka yote yangeishia china
 
Hivi hakuna namna serikali inaweza kuhalilisha meno iliyokamata ikayauza kwa manufaa ya taifa?
Hapo tumechoma $3bn ambazo zingefanya kitu cha maana $3bn*2185 = ~ TZS 6.5 tr..
Mwongozo tafadhali...
 
Kama nilisikia TZ imepeleka ombi Malawi kuzuia kuteketezwa kwa meno hayo....nikajiuliza maswali mengi kichwani, endapo Malawi wangeridhia, TZ ingetuma team ya kwenda kuyafuata? per diem, usafiri...na bado yarudishwe nusu....
 
Hivi hakuna namna serikali inaweza kuhalilisha meno iliyokamata ikayauza kwa manufaa ya taifa?
Hapo tumechoma $3bn ambazo zingefanya kitu cha maana $3bn*2185 = ~ TZS 6.5 tr..
Mwongozo tafadhali...

Unaona eeeh, Malawi mpaka Tanzania madawa hospitalini hamna, shule hazina madawati. Serikali ingekuwa inataifisha na kununua vitu hivyo au labda hela itumike kuboresha jinsi ya kulinda wanyama hao.
 
Mtaalam wa Kiswahili FaizaFoxy:Hivi ni meno ya Tembo au pembe za Tembo?Nirudi kwenye mada sasa:Hivi haya meno yanatokaje mbugani na kuvuka mipaka?Yanapita barabara zipi?yanavuka mipaka ipi?Au yanarushwa na chopper kutoka mbugani?Kuna sehemu inapwaya (jipu)
 
Hivi katibu mkuu wa chama atalala kweli leo mzigo wake mkubwa kiasi hicho umeangamizwa!!!! Safi sana Malawi kama hawa madentist wakiongozwa na mzee wetu katibu mkuu wakianza kupata hasara wataacha hiyo biashara haramu na dhalimu
 
Hivi hakuna namna serikali inaweza kuhalilisha meno iliyokamata ikayauza kwa manufaa ya taifa?
Hapo tumechoma $3bn ambazo zingefanya kitu cha maana $3bn*2185 = ~ TZS 6.5 tr..
Mwongozo tafadhali...
Unachozungumza ni sawa na kusema tuuzie bangi na Mirungi kwa nchi zilizohalalisha biashara hiyo.

Tambua kuwa sheria ya nchi yetu inakataza kufanya biashara ya nyara kwa mantiki hiyo huwezi kuwa unakamata nyara ili baadae uuze kama nchi hii itakuwa unajidanganya mwenye maana hakutakuwa na maana ya kuzizuia kisheria...

Kwa maana nyingine kuuza nyara na kuja kufanyia kazi za serikali huo utakuwa ni utakatishaji wa fedha chafu..... Tutafute vyanzo vingine halali za mapato kuendesha shughuli za serikali.
 
Back
Top Bottom