Malawi Wameonyesha Njia - Je Tanzania Tutaweza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malawi Wameonyesha Njia - Je Tanzania Tutaweza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakalende, May 23, 2009.

  1. K

    Kakalende JF-Expert Member

    #1
    May 23, 2009
    Joined: Dec 1, 2006
    Messages: 3,259
    Likes Received: 33
    Trophy Points: 135
    Wakati Dr. Bingu wa Mutharika alipoamua kupambana na mafisadi nchini mwake, wengi hawakuamini kama atafanikiwa. Mambo yalikuwa magumu hadi akalazimika kukiacha CHAMA kilichomweka madarakani.

    Mafisadi nao wakatangaza vita dhidi ya raisi huyo na ikapita mizengwe mingi sana bungeni wakijaribu kuifanya serikali yake ishindwe kufanya kazi na wakati fulani wabunge ambao wengi wao ni mafisadi walijaribu kukwamisha miswada ya serikali ikiwemo bajeti.

    Sasa katika uchaguzi huu wananchi wa Malawi wamesema kwa kauli nzito kwamba wako nyuma ya kiongozi wao katika mapambano haya kwa kumchagua kwa karibia 70%

    SWALI hapa ni kama hata sisi tunaweza? JK yuko tayari kuiacha CCM tukamuunga mkono? Wadau Tujadili!     
  2. PakaJimmy

    PakaJimmy JF-Expert Member

    #2
    May 23, 2009
    Joined: Apr 29, 2009
    Messages: 16,236
    Likes Received: 309
    Trophy Points: 180

    YES-WE CAN!

    Hiyo Mjomba tunaiweza- just the matter of deciding na

    kuweka hasira zetu kwenye ballot box.

    Ila JK mmmhhh!!, si rahisi akabadilika, coz anaogopa

    kuhukumiwa na historia ya chama!

    Labda akina Kingunge et al wawe wamesafiri!
     
  3. M

    MzalendoHalisi JF-Expert Member

    #3
    May 23, 2009
    Joined: Jun 24, 2007
    Messages: 3,869
    Likes Received: 116
    Trophy Points: 160
    JK je anaweza kuwa na huo ujasiri??

    Hana huo ujasiri!
     
  4. R

    Rwabugiri JF-Expert Member

    #4
    May 23, 2009
    Joined: Jul 10, 2007
    Messages: 2,777
    Likes Received: 11
    Trophy Points: 135

    Mhhh.. JK has failed us big time.. we need a stonger person than him!
     
  5. K

    Kakalende JF-Expert Member

    #5
    May 24, 2009
    Joined: Dec 1, 2006
    Messages: 3,259
    Likes Received: 33
    Trophy Points: 135
    Tuangalie mazoea yetu katika uchaguzi;

    Je, watanzania wako tayari kumchagua mtu bila kupewa zawadi za kanga na fulana?

    Itawezekana mtu makini kuteuliwa kugombea nafasi ya kisiasa bila kupitisha bahasha za RUSHWA kwa wajumbe wa kamati za vyama? (HILI NI WOTE SISIEMU NA WAPINZANI)

    Iwapo tuliwapigia kura viongozi kwa kuhongwa vijizawadi na bakhshishi; tunawashangaa nini wanapoingia ofisini na kuanza kujilimbikizia mali?

    Wakati tunapiga kelele kumkimbiza mwizi/fisadi, hakika hayuko peke yake, ana kundi kubwa la watanzania nyuma yake wanaotegemea kufanikisha maisha kwa njia za mkato. Tuliona jinsi wenzetu walivyokimbilia kupanda 'mbegu' kule DECI huku wakijua hakuna biashara yoyote inayozaa faida kiasi hicho.

    TUNAHITAJI MAPINDUZI YA UTAMADUNI!
     
  6. M

    MzalendoHalisi JF-Expert Member

    #6
    May 24, 2009
    Joined: Jun 24, 2007
    Messages: 3,869
    Likes Received: 116
    Trophy Points: 160
    Hivi JK akijitoa CCM na kuanzisha chama kingine-katiba yetu inasemaje- bado atakuwa raisi??
     
Loading...