Malawi wamelianzisha je na sisi tulianzishe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malawi wamelianzisha je na sisi tulianzishe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by segwanga, Jul 20, 2011.

 1. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  [h=1]Machafuko yazuka mjini Lilongwe Malawi[/h]
  Machafuko yamezuka mji mkuu wa Malawi, Lilongwe, wakati makundi ya upinzani yakipinga serikali ya Rais Bingu wa Mutharika.
  [​IMG]Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi


  Mwandishi wa BBC mjini Lolongwe Joel Nkhoma, amesema waandamanaji walikuwa wanachoma vizuizi barabarani na kupora.
  Serikali imezuia radio kutangaza moja kwa moja ghasia hizo.
  Matatizo yalianza baada ya mahakama kutoa hukumu siku ya Jumanne kwamba maandamano ya nchi nzima, yaliyoitishwa kupinga kupanda gharama za maisha, ni haramu.
  Mwandishi wa BBC amesema licha ya uamuzi huo wa mahakama, maandamano pia yamefanyika katika mji mkuu wa kibiashara Blantyre, na katika mji wa kaskazini wa Mzuzu.
  Lakini hali imekuwa mbaya zaidi mjini Lilongwe, ambapo waandamanaji wenye hasira walikuwa wakipiga kelele, "Mutharika aondoke", amesema mwandishi wetu.
  Mwandishi huyo amesema polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na wameweka vizuizi barabarani kuzuia waandamanaji kuingia katikati ya mji wa Lilongwe, ambapo maduka yote yamefungwa na mitaani hakuna watu.
  Kwa mujibu wa mwandishi wetu ghasia zipo zaidi katika miji midogo iliyo karibu na Lilongwe ya Biwi, Kawale na Nchesi.
  Kumekuwa na majibizano ya kushambuliana kati ya polisi na waandamaji, kwa mujibu wa msemaji wa Tume ya Haki za Binadamu ya Malawi Mike Chipalasa.
  "Watu wana hasira sana. Hali si nzuri hapa," amesema.
  Duka linalomilikiwa na Mbunge kutoka chama kinachotawala cha Democratic Progressive Party (DPP) na ghala la mfanyabiashara mwenye uhusiano na Rais Mutharika yameporwa kwa mujibu wa mwandishi wa BBC.
  Pia kuna taarifa za kuchomwa moto nyumba za askari polisi watatu mjini Lilongwe.
  Polisi pia wamezuia kamera ya mpiga picha mmoja aliyekuwa akipiga picha maandamano hayo.
  Kuna taarifa nyingine zinasema polisi walimpiga risasi sikioni mwandamanaji mmoja, wakati mali ya waziri mmoja iliposhambuliwa.
  Maandamano hayo yaliitishwa kupinga kupanda bei ya mafuta, upungufu wa hazina ya fedha za kigeni, kukosekana utawala bora na uhusiano mbaya wa kimataifa.
  Wiki iliyopita Uingereza ilisimamisha misaada kwa Malawi baada ya kutokea mzozo wa kidiplomaisa na serikali ya Mutharika.
  Uingereza iliishutumu Malawi kwa kushindwa kusimamia uchumi na haki za binadamu.
  Hivi karibuni serikali ilipitisha hatua za kubana matumizi, ikapandisha kodi na kupunguza utegemezi wa misaada.
  Malawi ni moja ya zilizo masikini sana duniani, ikikadiriwa asilimia 75 ya watu wa nchi hiyo wanaishi chini ya dola moja kwa siku.
  My take:Kwa serikali ,ukiona mwenzako akinyolewa tia maji!
   
 2. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ubinafsi umetutawala ndio maana unaona watumishi wa serikali wanawaza kupata mishahara mikubwa tu! siyo mapinduzi ya kiitikadi, CCM itawaongezea mshahara wakati wa kampeni alafu utaona wanavyoipigia CCM kampeni kwa nguvu zao zote 2015.
   
 3. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni libeneke ya nguvu, lakini kila kitu kina chanzo, huu moshi unaofuka ni hatari pia kwetu, ngoja tuone!!!!!!!!!!Angalia hapo kwenye red!!!!!!!!
   
 4. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tuna amani sisi tanzania ndio urithi wetu
   
 5. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Mi naona tulianzishe, sababu kubwa ni umeme. Umepanda gharama alafu haupo kila kitu hovyo rushwa bungeni hadi mahakamani. Tlianzishe tuifukuze CCM la sivyo hatutafika.
   
 6. M

  Magarinza Senior Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: May 9, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Peoples' power........................... Peoples' power...,,......................
   
 7. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  na huku nako muda si mrefu tutaandamana
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Jul 20, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Inatakliwa hii movie tuifanye mbayuwayu akiwa ughaibuni, yaani tunafunga viwanja vyote vya ndege kwa nguvu ya umma asishuke arudi huko huko alipotoka.
   
 9. c

  chief m Member

  #9
  Jul 20, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwendawazimu wewe, laiti ungeipenda Tanzania hungekuwa na wazo la kuchochea machafuko ndani ya nchi yako. Do you know the exact cost. Mawazo yako ya kiubinafsi na ulafi wa madaraka. Huyo unayemhangaikia awe Rais mmeo na kama ni mmeo sio mwite rais muwapo kitandani? Kwani lazima aende ikulu? Look at you! Machafuko nayo ni ya kushabikia?
   
 10. c

  chief m Member

  #10
  Jul 20, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnakula nini mpaka ubongo unageuka kuwa kamasi? Ungekuwa na ubongo wa kawaida huwezi ukafikiri kwa kutumia kamasi kuwa eti kuna machafuko mahali fulani nasi tuanzishe, a shame to you. Tumia akili kama ni pepo la kuandamana nenda kaombewe
   
 11. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Inatubidi na sisi tuandamane tena nchi nzima.
   
 12. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  naunga mkono hoja mia kwa mia. wewe je?
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Amani? My foot!! Amani ipi?

  Tuko gizani, viwanda vimefungwa vijana wetu hawana kazi, wewe unasema tuna amani? Hakuna amani, tumejawa na uoga usio kuwa wa maana, maisha yamepanda maradufu!! wewe unasema tuna amani....

  Fyuuuuu.......
   
 14. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #14
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Siku zenu zinakaribia nenda kawaambie wenzako Watanzania wanakuja
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Soon tutaamka tuu!
   
 16. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #16
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hivi unadhani babu zako kina Mkwawa, Mirambo, Kinjekitile wangekuwa na mawazo kama yako ungekuwa wapi wewe usiye na haya..hakuna haki inayokusubiri ukiwa umekaa ipiganie na kupigana ndo huku..acha wewe unadhani nani atakukomboa..jisimamie..pambaf
   
 17. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wenzenu hawabaguani kikabila na kidini kama CDM inavyofanya! Chadema hakiwezi kuwa kiongozi wa mabadiliko kwa Tanzania nzima kwa sababu ni chama cha kikwaya kwaya na mbege mbege!
   
 18. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Utawajua tu kwa magamba yao,mimi nimeuliza swali sijataja tanzania,unajua jf inafka wapi na unajua mi niko wapi?unajua ninalenga watu gani? rejea kwenye kichwa cha habari.Unakuwa na akili kama za spika makinda,anauliza endapo kiongozi mkuu kama waziri mkuu akidanganya bunge atachukuliwa hatua gani yeye anakurupuka kusema thibitisha kwamba waziri mkuu kasema uongo.Mi nimetahadhalisha,sijashabikia machafuko.THIBITISHA KAMA NIMESHABIKIA MACHAFUKO ZAIDI YA KUTOA HABARI KUHUSU KINACHOJIRI MALAWI NA KUULIZA SWALI
   
 19. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Pala...mpalaa....mpalaa...tila..tilaa! Hili goma la Manzese...Magomeni mje tucheze woteee!! Tipi...tipi...tipi..top...!!!
   
 20. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Watu wa aina yako,wenye fikra na waoga wa mabadiliko,waliokosa uthubutu wa kufanya maamuzi magumu wako wengi nchi hii!Na ndio mnaorudisha nyuma harakati za kuirejesha TANZANIA mikononi mwa wa Tanzania!
   
Loading...