Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,057
- 16,737
Kiburi cha Malawi kinatoka hapo kwenye red. Waingereza ni wabuni sana, wako upande wa Tanzania at the same time wanawapa kiburi Malawi especially kipindi hiki ambacho Malawi wana matatizo ya fedha watanfaya chochote ili mradi mdomo uelekee kinywani. Kuna jambo moja inabidi serikali iwe makini sana, ukanda wa kusini una makampuni ya ulinzi toka nje ya nchi na wana silaha kubwa! Hichi kitu kiliongelewa bungeni lakini hakuna majibu ya maana. Uingereza wana tabia ya kutumia 'meceenaries', kwa nje inaonekana serikali haihusiki lakini ukweli hao hao mecenaries wanakuwa na link na serikali.
Waingereza na binadamu mahili sana wa kuhuma na kupuliza, watu tunasahau kwamba IRAQ ilikuwa ni nchi moja wakati ya utawala wa Uingereza kabla hawajaondoka IRAQ; Waingereza walihakikisha wanamega kipande cha aridhi ya IRAQ na kukipachika jina la KUWAIT - nia yao hasa hasa walikuwa hawataki nchi ya IRAQ imiliki vitalu zingi vya mafuta, naona mbinu hizi ndizo wanataka kuzitumia nchini Malawi baada ya kuona kuna uwekano mkubwa wa ziwa Nyasa kuwa na mafuta. Malawi haiwezi kuwa na ubavu wa kuitisha Tanzania kwa njia yoyote ile bila ya kuwa na watu wanao wapa jeuri for a reason.
Kuhusu matumizi za mercenaries wakijidai ni walizi wa kawaida, hilo wala alishangazi, Waingereza utumia sana kikosi cha SAS kufanikisha AZMA zao za kimaslahi yanayo husu nchi yao, wana mbinu nyingi.
Nakumbuka nilipo kuwa nasoma shule ya msingi, ramani ya Tanzania tulikuwa tuna chora kwa kuonyesha mpaka wa ziwa Nyasa ulikuwa unapita katikati ya ZIWA, hata ramani zilizo chorwa na Harper Collins wa Uingereza zilionyesha hivyo hivyo - sasa tatizo linaibuka kutoka WAPI tena!