ngoja tuone hiyo september meeting, ila sioni kama kutakuwa na jipya sababu malawi wameshatuweka mtegoni kwa kusema wanasheria wakuu wa serikali wakutane kuupitia mkataba wa 1890, kwa nini wapitie mkataba huo pekee ili hali kila mtu anajua hauipi favour tz kisheria?
huwezi kuwa fair kwenye hili maana umeshatamka wazi kwamba hawahatuvunjia haki NA Ndege zao kutua Mbambabay walikua NA haki na wanapaswa kwenda kutundika NA Bendera yao kule. Hongera sana Mkuu
ntasema kidogo juu ya hili
...ni kwamba tanzania inamiliki ziwa hilo kwa asilimia 50 na malawi asilimia 50.. ndipo malawi wakahoji kama tunamiliki ziwa hili kwa 50/50 je msumbiji inamiliki ziwa kwa asilimia ngapi maana sehemu ya ziwa hilo iko pia msumbiji.watanzania walishindwa kujibu. na hili swali liliuzwa pia na chiume waziri wa mambo wa nje wa malawi alipokutana na membe pale serena hoteli mwezi uliopita na membe hakulijibu swali hilo.
kwa kifupi ni kwamba wawakilishi hawakuwa uwezo wa kujenga hoja , maandalizi yalikuwa duni, taarifa a membe bungeni ilileta mkanganyiko mkubwa sana..
..naona Malawi wanatumia kila opportunity kueleza kwamba wanamiliki 100% ya ziwa nyasa.
..kwa upande mwingine Membe haelezi anacho-negotiate haswa ni kitu gani.
..Membe ameshindwa kueleza haki ya Tanzania ktk ziwa hilo ni ipi. je, ni 50%, 30%, au???!!
Nimejaribu ku-attach ule mkataba wa Heligoland Zanzibar ili tuone kama kuna hoja ya msingi kuendelea na majadiliano hayo ya Membe na Chiume. Issue ya mgogoro huu ipo katika article I (2) inaelezea mpaka utakavyokuwa ambapo hakuna shaka sisi kama Watanzania hatuna chetu kwa mujibu wa mkataba huu. Hata hivyo zipo loopholes ambazo tunaweza kuzitumia ili kuu-defeat mkataba huu kwa mfano sehemu ya mwanzo ina maneno haya:
'This treaty temporarily settled colonial disputes between Germany and Great Britain. It recognized Tanganyika as a German colony; in return, the Germans abstained from further encroaching into British Kenya. The agreement ceded Heligoland, an island off the coast of Schleswig-Holstein in the North Sea, to Germany. Because the treaty appeared to abandon German colonial claims to much of east Africa, it unleashed a storm of nationalist protest at home.'
Hapo kwenye nyekundu inaonekana kama ifuatavyo:
(1) Mkataba huu uliondoa migogoro ya kimipaka kati ya Uingereza na Ujerumani kwa muda (temporarily),
(2) Wajerumani walikuwa wakiendelea kuchukua maeneo kutoka koloni la Uingereza liitwalo Kenya; hivyo kwa mujibu wa mkataba huu waliacha kufanya hivyo.
Ni wazi kuwa hapakuwa na mgogoro wowote katika mpaka wa ziwa Nyasa, inawezekana Wajerumani walikuwa wamechukua eneo kubwa kutoka Kenya hatimaye walikubali mpaka wa kusini yaani huko Ziwa Nyasa upite kando kando ya ziwa, hata hivyo mkataba huu ulikuwa ni wa muda tu. Kwa kuunganisha na kijiramani cha German Osta Africa kilichoambatishwa hapa pamoja na ramani za Mwingereza zinazoonesha mpaka ukiwa ndani ya ziwa tunaweza ku-raise doubts kwa mahakama za kimataifa na hatimaye kutupiliwa mbali kwa madai ya Malawi kupitia Heligoland Zanzibar Treaty.
Lengo letu kuu sasa hivi ni kuufanya mkataba wa Heligoland Zanzibar usiwe na nguvu kwa wakati uliopo (kwa sababu huu makataba ndiyo kiini cha madai ya Malawi), tusipopata hoja za kupambana na huo mkataba hilo ziwa litakuwa limeondoka rasmi katika vitabu, ramani, nyaraka zote za Tanzania endapo Malawi watakwenda katika mahakama za kimataifa.
Mimi sio mtalaam wa sheria lakini ninachofahamu mshitakiwa hahitaji kuthibitisha mahakamani kuwa hakutenda kosa bali anatakiwa kuonesha mashaka mbele ya mahakama (to raise doubts) katika ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ili upande huo wa mashitaka ushindwe kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa mshitakiwa alitenda kosa.
AG na timu yako pamoja na wanasheria wote wa nchi hii bila kujali itikadi za kisiasa, unganisheni nguvu tuikomboe nchi yetu pasi na kumwaga damu.
Kuna mtu humu kaja na hoja ya kusema waandishi makajanja ndiyo wame-mislead jambo hili. Pamoja na kwaba sikubaliani sana na aliyesema hivyo lakini unavyokuja humu ni kama unaanza jambo jipya wakati tumetuma posts zaidi ya 600 ndai ya wiki mbili kwa hili.
Sasa ona, unakurupuka na suala la ndege kutua Mbamba_Bay ambalo ni la January mwaka huu wakati controversy hii ni ya zaidi ya miaka 50 sasa.
Hebu pitia thread zote ndiyo uje tujiunge behewa moja maana tunashindwa tukujibu nini. Soma walau thread hii: {Click Here}
Unaonesha hauna umakini wa kusoma na kuelewa, hilo ni tatizo kubwa sana kwa wengi wenye fikra hasi kila wakati.
Soma hiki kipande pekee labda utaacha kutupa madongo yasiyo na muelekeo:
Nikupateje,Hatutaki ufisadi wa kuwaibia wenzetu ziwa ambalo mkataba unasema si letu.
Kuna mtu humu kaja na hoja ya kusema waandishi makajanja ndiyo wame-mislead jambo hili. Pamoja na kwaba sikubaliani sana na aliyesema hivyo lakini unavyokuja humu ni kama unaanza jambo jipya wakati tumetuma posts zaidi ya 600 ndai ya wiki mbili kwa hili.
Sasa ona, unakurupuka na suala la ndege kutua Mbamba_Bay ambalo ni la January mwaka huu wakati controversy hii ni ya zaidi ya miaka 50 sasa.
Hebu pitia thread zote ndiyo uje tujiunge behewa moja maana tunashindwa tukujibu nini. Soma walau thread hii: {Click Here}
Ndugu zangu,...
....Prime Minister, Rashidi Kawawa, made three points: (i) that no part of Lake Nyasa fell within German East Africa; (ii) that since the boundary had not been altered by Britain after the assumption of the mandate, the Prime Minister's statement of 30November 1961 did not apply; and (iii) that whatever the disadvantages to Tanganyika, the Government could not contemplate negotiations with either the Central African Federal Authorities in Salisbury or with Britain. 'If there are to be negotiations on this question', he concluded, 'they must be with the Government of Nyasaland itself and must wait the attainment by Nyasaland of full Independence.
Kinachozungumzwa hapo juu katika point ya pili kinatokana na kauli ya PM Nyerere ya 30 Novemba 1961 ambapo Mwalimu alitoa muelekeo wa sera za nchi huru ya Tanganyika ambapo alisema kuwa Tanganyika ingeendelea kuheshimu makubaliano yaliyofanywa na wakoloni kwa miaka miwili zaidi baada ya kupata uhuru.
Hii maana yake ni kuwa kiongozi wa juu wa Tanganyika aliwahi kukili kuwa Tanzania hatuna chetu katika ziwa lile na kwamba ishu hii si miongoni mwa mikataba ambayo Tanganyika huru ingeendelea kuiheshimum kwa miaka miwili zaidi mara baada ya uhuru. Hii maana yake ni kwamba Mkataba wa Heligoland ni valid mpaka leo kwani haukuwa miongoni mwa mikataba ambayo Tanganyika huru ingeiheshimu kwa kipindi cha miaka miwili tu.
Mkuu kwani wewe ni Mmalawi? Maana sikuelewi elewi!