Malawi refers lake border dispute with Tanzania to UN

Tupo Tayari muda wowote kuingia vitani na MALAWI ikiwa watalazimisha kulichukua Ziwa Nyasa na kulifanya la kwao.

Serikali itoe leseni kwa makampuni ya kimataifa kufanya exploration kwenye ziwa hilo.
 
Joyce banda ni kweli alikosa kura hadi kwao na aliondoka kwa kilio.Kuna mengine siandiki hapa.Ila ninachoweza sema huyo Raisi wa sasa wa Malawi akae kwa Amani na Tanzania akitaka akaulize kwa nini Raisi Kamuzu Banda aliamua kuacha uadui na Tanzania na kusalimu amri.Kama hajui ngoja nimmegee kidogo.Mipaka ya Tanzania kila upande tulikuwa tunasumbuliwa.Uganda kulikuwa na shida ya akina Idi AMIN,Rwanda kulikua na shida,Burundi kulikuwa na shida,Congo mobutu alikuwa anatusumbua,Malawi alikuwa Kamuzu BANDA anatusumbua,Msumbiji wareno wakawa wanatusumbua.Tanzania ikaamua kuwa huo usumbufu lazima ukome kwa hiyo ikaamriwa kuanzisha mashambulizi ya mfululizo kote kuhakikisha wasumbufu wote wanang`ooka ili nchi ikae salama.Ikaanza ng`oa.Banda akapata taarifa kuwa watanzania wameamua kuskushughulikia akanywea.KIMBUNGA kilipoanza akanusurika maana Tanzania iling`oa IDD amin IKAWEKA wapenda Tanzania akina museveni,Rwanda maruhuni walikuwepo wakang`olewa wakawekwa akina Kagame,Burundi akina BUYOYA waliokuwa wakitusumbua wakang`olewa WAKAWEKA wapenda Tanzania akina NKRUNZINZA,Kongo MOBUTU akang`olewa akawekwa mtoto wa MBEZI BEACH mkazi wa Tanzania MZEE kabila baba yake Raisi kabila aliyepo.Mozambique tukawasaidia vita mreno akang`olewa wakawekwa watanzania wa msumbiji akina Samora machel.Kile kimbunga Raisi Kamuzu BANDA kikamkosa sababu aliamua kusalimu amri mapema na akawa rafiki wa Tanzania hadi alitembelea Tanzania na akaachana na choko choko

Sasa hivi mipaka yote imetulia kasoro huo wa Malawi ndio unaleta fyoko.Ina maana akileta fyoko sasa hivi ni rahisi sababu nguvu zote zitaelekezwa malawi kumshughulikia barabara.

Huo mgogoro wa mpaka anaotunga utamgharimu
Sijui wanajiamini ni malawi na mkoa wa morogoro,morogoro mkubwa
Tunaingia lilongwe ndani ya masaa mawili tu
 
Source kubwa ya maji ya Ziwa Nyasa (inflows) ... yanatoka mito ya Tanzania (mto Ruhuhu)..huu nao ni ushahidi kuwa sehemu ya Ziwa ni yetu maana tunachangia hayo maji....

Kwa kuwa source kubwa ya ziwa nyasa ni mito yetu nafikiri fyokofyoko zikizidi cha kufanya tuchukue magreda tuchepushe hiyo mito badala ya kwenda ziwa nyassa iende mikoa ya ruvuma ,lindi na mtwara kuendesha kilimo cha umwagiliaji wakati tukiendelea na kushughulikia huo mgogoro
 
Hao wanapoteza muda, walikutana na mwanasheria mmoja mahiri sana kwenye mambo ya international law akawapelekesha mpaka wakakubaliana na utaratibu wa kugawana ziwa nusu kwa nusu.

Hizi chokochoko ni mpya, zinaanzishwa na watu ambao labda hawajui nini kilikubaliwa kati ya serikali ya awamu ya nne na uongozi wa yule Mama.
 
Du! Je, Mafia na Kisiwa cha Latham vipo Tanganyika au Zanzibar? Kwa historia ya bara letu migogoro hii itaibuka mingi, tutumie busara zaidi kuliko nguvu au sheria. Karibu kila nchi barani Afrika ina mgogoro wa mpaka na jirani, bahati tu tuseme nchi nyingi zimepotezea tu lakini watawala hubadilika, kila watakapokuja wakorofi migogoro hiyo itaibuliwa na huenda ikasababisha vita.
 
Wanadai wamepewa na Wakoloni (Helgoland Treaty), Sisi tutadai tumepewa na Mungu...haiingii akilini watu wameishi miaka maelfu na ziwa lao eti leo unawaambia Ziwa sio lenu mpaka upo mwaloni kisa Helgoland ; Seriously??

Source kubwa ya maji ya Ziwa Nyasa (inflows) ... yanatoka mito ya Tanzania (mto Ruhuhu)..huu nao ni ushahidi kuwa sehemu ya Ziwa ni yetu maana tunachangia hayo maji....
Si Ruhuhu tu kuna mito mingi sana inaingia ziwani kutoka TZ
 
Joyce banda ni kweli alikosa kura hadi kwao na aliondoka kwa kilio.Kuna mengine siandiki hapa.Ila ninachoweza sema huyo Raisi wa sasa wa Malawi akae kwa Amani na Tanzania akitaka akaulize kwa nini Raisi Kamuzu Banda aliamua kuacha uadui na Tanzania na kusalimu amri.Kama hajui ngoja nimmegee kidogo.Mipaka ya Tanzania kila upande tulikuwa tunasumbuliwa.Uganda kulikuwa na shida ya akina Idi AMIN,Rwanda kulikua na shida,Burundi kulikuwa na shida,Congo mobutu alikuwa anatusumbua,Malawi alikuwa Kamuzu BANDA anatusumbua,Msumbiji wareno wakawa wanatusumbua.Tanzania ikaamua kuwa huo usumbufu lazima ukome kwa hiyo ikaamriwa kuanzisha mashambulizi ya mfululizo kote kuhakikisha wasumbufu wote wanang`ooka ili nchi ikae salama.Ikaanza ng`oa.Banda akapata taarifa kuwa watanzania wameamua kuskushughulikia akanywea.KIMBUNGA kilipoanza akanusurika maana Tanzania iling`oa IDD amin IKAWEKA wapenda Tanzania akina museveni,Rwanda maruhuni waliokuwepo wakang`olewa wakawekwa akina Kagame,Burundi akina BUYOYA waliokuwa wakitusumbua wakang`olewa WAKAWEKA wapenda Tanzania akina NKRUNZINZA,Kongo MOBUTU akang`olewa akawekwa mtoto wa MBEZI BEACH mkazi wa Tanzania MZEE kabila baba yake Raisi kabila aliyepo.Mozambique tukawasaidia vita mreno akang`olewa wakawekwa watanzania wa msumbiji akina Samora machel.Kile kimbunga Raisi Kamuzu BANDA kikamkosa sababu aliamua kusalimu amri mapema na akawa rafiki wa Tanzania hadi alitembelea Tanzania na akaachana na choko choko

Sasa hivi mipaka yote imetulia kasoro huo wa Malawi ndio unaleta fyoko.Ina maana akileta fyoko sasa hivi ni rahisi sababu nguvu zote zitaelekezwa malawi kumshughulikia barabara.

Huo mgogoro wa mpaka anaotunga utamgharimu
Tanzania ya wakati ule si ya leo. Wakati ule uzalendo ulikuwa mkubwa na intelejensia ya uhakika hata kaburu alishindwa
 
Tanzania ya wakati ule si ya leo. Wakati ule uzalendo ulikuwa mkubwa na intelejensia ya uhakika hata kaburu alishindwa

Uko sahihi kabisa ...sasa hivi hakuna uzalendo kabisa....
 
Hao Malawi wangekomalia kabisa na Mbeya kuwa yao , ili tuhamie kule tuwaachie nchi ya matamko
 
Hawa wamalawi wana tamaa za mchwa kama ccm, malawi na ccm hawana tofauti na mchwa
 
Ni kweli watu hawa siyo wa kudharauliwa hivi hivi....yule Rais wao miezi miwili iliyopita 'alizamia' Marekani sijui alikuwa ana ajenda gani huko...
Yes, huyu hawezi kusimama peke yake kulumbana na Tanzania! Wazungum, tena super powers wanatafuta resources kwa ajili wa raia wao especially Marekani ambayo inasema "USA interests first"!
 
Maji ya Ziwa Victoria eti ni ya Wamisri

Maji ya Ziwa Nyasa eti ni ya Wamalawi

Kule Mashariki, Kabahari ketu kanaishia Chumbe, iliyobaki ni ya Wazanzibari

Sasa sisi Tanganyika tumezunguukwa na maji kumbe si yetu?
 
Sijui wanajiamini ni malawi na mkoa wa morogoro,morogoro mkubwa
Tunaingia lilongwe ndani ya masaa mawili tu
Acha ulevi wako wewe. Unafikiri vita ni rahisi kama unavyodhani? Mbona Marekani hajaweza kumpindua Asadi, mbona Marekani hajaiweza Somalia, Mbona Kenya inasoteshwa na alshababu. Umeshiba maharage kisha unakuja kubeua tu hapa. Siku zote busara ni kutafuta ufumbuzi kwa njia ya amani kwanza kwa kuwa vita vina madhara ya muda mrefu kwa pande husika. Usidhani huo ni u CDM na ULUMUMBA uliozoea.
 
Kuna kitu Wamalawi wanasahau kuwa vitu kama maji na hewa alivigawa kwa watu na mataifa yote! Vitu hivyo ndiyo vimewezesha uhai, hivyo vinapokuwa katika mipaka ya nchi au mabara matumizi yake lazima yawe ya pamoja na kushirikiana. Maji au hewa ikichafuliwa upande mmoja athari zake zitafika hadi upande wa pili!
 
Tanzania ya wakati ule si ya leo. Wakati ule uzalendo ulikuwa mkubwa na intelejensia ya uhakika hata kaburu alishindwa
Joyce Banda kashughulikiwa zama hizi.Kipindi cha Kikwete!! Hajashighulikiwa zama za Nyerere!!
 
Back
Top Bottom