Malawi President, opposition leaders to discuss Tanzania dispute on 08 October

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Malawi President Joyce Banda on Monday met leaders of various political parties at Sanjika Palace in Blantyre in second round of consultative meeting on the border wrangle with Tanzania, Nyasa Times learnt. State House press officer Brian Banda confirmed when asked by Nyasa Times that the meeting took place and included Leader of Opposition John Tembo representing MCP, Dr. George Mtafu and Friday Jumbe (UDF), Kamlepo Kalua (MDP), Gwanda Chakuamba (NRP), Mark Katsonga Phiri (PPM), Kamuzu Chibambo (Petra) and George Nnensa (Mafunde) .

"The President briefed opposition leaders on the Lake Malawi border negotiations with Tanzania and about discussions she had with her Tanzanian counterpart Jakaya Kikwete during the Sadc meeting in Mozambique," the press officer said.
Banda said the Malawi leader recognised the need to consult opposition leaders on matters of national interest, saying they have a role to play.

Tembo_JB_Meet-e1346700426801-300x180.jpg

President Banda and leader of opposition John Tembo

He however said the meeting was cordial and opposition members were "pleased" to be consulted and share their inputs. Tembo could not disclose what they had discussed saying it was for the consumption of the leaders present at the meeting only.
But he expressed satisfaction with the "refreshing approach" by the leadership to consult them.

Nyasa Times understands that President Banda informed the leaders that Malawi and Tanzania failed to agree after their recent talks recently. She told the leaders that Malawi government's position is that the boundary dispute has to be determined by the International Court of Justice (ICJ).

The opposition reportedly unanimously backed government's position since the matter is legal in nature. Tanzania media reported that Tanzanian president Jakaya Kikwete speaking in his end-of-the-month-address to his country, that the Anglo-German Treaty of 1890 that gave Malawi the sole ownership of Lake Malawi was flawed and Tanzania has every reason to demand this be corrected.

Kikwete said the Heligoland Treaty-an agreement between then colonial powers Germany and Britain-denies Tanzanians living on the shores of Lake Malawi "their given right to utilise proximate water and marine resources to earn their daily living" He argued that the treaty is erroneous because it contravenes international law that requires states to share adjoining water resources.
 
..msimamo wa Malawi unaeleweka tangu mwanzo.

..hebu nielezeni what was Membe trying to achieve kwenye vikao na ujumbe wa Malawi??

..nahisi kama vikao hivyo vilikuwa na fursa za ULAJI wa POSHO kwa Membe na genge lake la usuluhishi.

..wengine tulishasema tangu mwanzo suala hili lipelekwe haraka sana ktk MAHAKAMA YA KIMATAIFA.
 
Madame president action zake dhidi ya mpaka zipo taratiibu but vitendo vizito. Nimependa kweli alivyofanya, ingependeza pia kama raisi Jakaya pia angekuwa kawahusisha viongozi wa vyama pinzani kupokea mawazo juu ya hili tiff la chini chini...

She speak less, she act more:poa
 
Huyo Mama ni Ngangari na watashinda kesi. Hii kesi Jk aliyopeleka UN, itazidi kuthibitisha kauli ya Mh Mnyika "JK ni DHAIFU"
 
walau anaonyesha anajipanga kimkakati. Sisi tuendelee kuzurura, muda wa kesi hakuna maandalizi yoyote yaliyofanyika.
Kama kawaida, tunatengeneza mazingira ya kushindwa kabla.
Lakini kwa hili, uzembe hautavumilika.
 
Ziwa linakwenda kama mchezo wa kuigiza tena huku wa TZ tukishuhudia, sababu kubwa longolongo za meembe na mr. dhaifu, hawa wanyasa wangejaribu enzi za mkapa wangejuta!
 
Madame president action zake dhidi ya mpaka zipo taratiibu but vitendo vizito. Nimependa kweli alivyofanya, ingependeza pia kama raisi Jakaya pia angekuwa kawahusisha viongozi wa vyama pinzani kupokea mawazo juu ya hili tiff la chini chini...
Atawahusisha vipi wapinzani kwani mwanzoni alimuambia Mama Banda kuwa Wanaotaka vita ni wapinzani sasa huyo mama banda akijasikia JK kawaita wapinzani wajadili hili suala ndio atamsua kabisa jk na vikao vyake...

Ila huyu mama ni Mjanja sana anawashirikisha wapinzani ili baadae hata akijashindwa asipatikane wa kulaumiwa ndani ya malawi... naye ni Dhaifu
 
“The President briefed opposition leaders on the Lake Malawi border negotiations with Tanzania and about discussions she had with her Tanzanian counterpart Jakaya Kikwete during the Sadc meeting in Mozambique,” the press officer said.
Banda said the Malawi leader recognised the need to consult opposition leaders on matters of national interest, saying they have a role to play.
Hapa nimepapenda. Hivi Tanzania hiki kitu KIPO?
 
Madame president action zake dhidi ya mpaka zipo taratiibu but vitendo vizito. Nimependa kweli alivyofanya, ingependeza pia kama raisi Jakaya pia angekuwa kawahusisha viongozi wa vyama pinzani kupokea mawazo juu ya hili tiff la chini chini...

ahaaa haa wapo busy na maandamano!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Madame president action zake dhidi ya mpaka zipo taratiibu but vitendo vizito. Nimependa kweli alivyofanya, ingependeza pia kama raisi Jakaya pia angekuwa kawahusisha viongozi wa vyama pinzani kupokea mawazo juu ya hili tiff la chini chini...

Hawa wenzetu akili zao ziko next level.
Sisi huku,CCM wanajua wata tawala milele,kwa hiyo kila maamuzi
ni ya kwao tu.

Hawawazi kama maamuzi magumu kama haya wakiyafanya wenyewe yanaweza
kugeuzwa na chama kingine ambacho hakita kubaliana nayo kitakapo ingia
madarakani.
 
Kwa nini hapa kwetu swala la mpaka iwe ni shughuli ya ikulu na wizara ya mambo ya nje peke yao BILA KUWATAFUTA MAONI VIONGOZI WA UPINZANI kama huyu mama yetu Joyisi anavyoonekana kufanya?

Jamani maswala muhimu kiasi hiki kitaifa yasiendeshwe KI-ITIKADI kihivo.
 
...ina maana na dohutwa nae ashirikishwe...?
 
Atawahusisha vipi wapinzani kwani mwanzoni alimuambia Mama Banda kuwa Wanaotaka vita ni wapinzani sasa huyo mama banda akijasikia JK kawaita wapinzani wajadili hili suala ndio atamsua kabisa jk na vikao vyake...

Ila huyu mama ni Mjanja sana anawashirikisha wapinzani ili baadae hata akijashindwa asipatikane wa kulaumiwa ndani ya malawi... naye ni Dhaifu

Hawa wenzetu akili zao ziko next level.
Sisi huku,CCM wanajua wata tawala milele,kwa hiyo kila maamuzi
ni ya kwao tu.

Hawawazi kama maamuzi magumu kama haya wakiyafanya wenyewe yanaweza
kugeuzwa na chama kingine ambacho hakita kubaliana nayo kitakapo ingia
madarakani.

Hapa naona tatizo ni kulichukulia swala ki Siasa zaidi kuliko ki taifa... Nina wasi wasi sana na hatma ya hili zengwe itakavyokuwa. So far namna linavyoendeshwa naona kama vile kuna uwezekano wa sie kukosa haki yetu.
 
Tanzania ndiyo ya kwanza ku-file kesi mahakama ya kimataifa. It's already there.
Sidani kama tutapata nusu, ila sidhani kama mpaka utakuwa ufukweni.
Wapinzani wenyewe wamekaa kimya kuhusu suala hili, actually wapinzani huwa foreign policies zao hazijulikani hasa kuhusu Palestine, Sahrawi na Syria sasa hivi hatujui kama wapinzani wanaunga mkono msimamo wa serikali au la.
 
Ungangari wa Malawi umejirudia enzi za Banda, lakini banda aliponusa tu dalili ya kuona mtazamo wa taratibu za kimataifa kuhusu mipaka inayotokana na kugawanywa na maji aliamua kurudi nyuma na kubaki kimya na kuachia watakaofuta wafanyie kazi.

Presiden aliyemtangulia Banda alikuwa na dalili ya kufanya kile ambacho mwafaka ungefanyika kadiri ya mwona wa kimataifa, tatizo khofu yake wengine walio ngangari kufikiria ziwa lote lao.

Huyu mama Joyce asipoangalia suala hili laweza kuwa mafanikio au kushindwa kwake katika uchaguzi Mkuu ujao nchini Malawi.
Mambo mengi ambayo yanagombaniwa ni it looks like some lake something in common. Kama angetumia kuungo cha kawaida ambacho wengi hukitumia kufikiri asingekuja juu na mishipa yake kusimama usoni hadi kupata hatari yakupasuka kwa shinikizo la damu kwa sababu zifuatazo"

  • Kando ya Ziwa Nyasa upande wa mashariki ni ardhi ya Tanzania
  • Kando ya Ziwa Nyasa kuna raia watanzania wakazi halali katika ardhi yao ambayo uhai wao hutegemea ardhi na maji ya ziwa Nyasa
  • Je, ingetokea mkataba huo unasema ziwa Nyasa belongs to Tanzania angekubali mpaka wa Malawi kupita ukingonimwa magharibi mwa ziwa Nyasa na hivyo Tanzania kuhodhi ziwa?

Pamoja na hayo, anapozidi kung'ang'ania hilo kuna tetesi kwamba wapinzani wa serikali yake wanamwona kama anapoteza muda kudao jambo ambalo kimataifa halitampa ushindi kwani kila upande una haki ya kutumia maji ya ziwa hilo naturally, kwa vile ziwa halijatengenezwa na Wamalawi. Hata mifereji ya kuchimbwa kama ile ya Zuez na Panama hakunaga ile itu ya uthibiti wa maji ila tu vyombo vinavyopita kwa vile waliochimba miferejihiyo iliwagharimu.

  • Sheria za kimataifa katika kusuluhisha migigoro mingi ya aina hiyo iliishia kuamua kwamba mipaka ipite katikati ya maji
  • Asije kuonekana ni kiongozi wa kike asiyeweza kupima mambo kwa upeo wa kimataifa na kufikiria kitaifa tu.
  • Yawezekana udhaifu wake katika kuongoza nchi wenye upeo mdogo katika jambo hili wanamtumia.

Kwa hili nampa pole, kwani watanzania kuna waliposimamia kudai haki za mpaka kupita kati, ingekuwa nchi kavu hili halingekuwa na ubishi.
Joyce Banda anaoekana kucheza ngoma asiyoijua miondoko yake.
 
Back
Top Bottom