The Stig
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 1,113
- 1,105
Kwa nini tusiwe na vinu vya kufua na kusafisha dhahabu hapo hapo Tanzania badala ya kuipeleka nje? Tunajua ni kiasi gani kinapelekwa nje kila wiki?
Geita, Bully, Nzega na migodi yote mikubwa inasafisha dhahabu kwa asilimia 99.8. Kufikia purity ya 99.999%, inabidi mitambo tofauti zaidi ambayo haileti sense kuijenga kwenye kila mgodi. Mtambo wa namna hiyo upo S. Africa, unaitwa Rand Refinery, na unahudumia karibu migodi yote ya Africa. Huu mtambo hutenganisha "uchafu" wa silver kutoka kwenye dhahabu
Kuna mitambo mingine hutoa "uchafu" wa copper na cobalt. Viwanda hivi ni vichache sana ulimwenguni. Dhahabu ya Bully ni mfano wa dhahabu yenye uchafu huu. Huwa inapelekwa Japan, kama jinsi migodi mingine ya dunia yenye dhahabu ya namna hiyo yanavyofanya.
Pamoja na hiyo, bado shughuli ya kusafisha dhahabu kufikia 99.8% ni shughuli pevu hasa, na ni moja ya shughuli inayokula kipande kikubwa cha ile 60% ya mauzo ya tofali la dhahabu.