Malawi Nchi Yenye Wanawake Wengi Kupiga Marufuku Ndoa za Wake Wengi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malawi Nchi Yenye Wanawake Wengi Kupiga Marufuku Ndoa za Wake Wengi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, May 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa masuala ya jamii wa Malawi, Patricia Kaliati Friday, May 07, 2010 3:38 AM
  Malawi nchi ambayo ina idadi kubwa sana ya wanawake kuliko wanaume, inatarajia kupitisha sheria itakayowapiga marufuku wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja hali ambayo imeamsha hasira za wanaume wa kiislamu nchini humo. Serikali ya Malawi inatarajia kupiga marufuku wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja hali ambayo imewakasirisha waislamu ambao idadi yao ni ndogo sana nchini Malawi.

  Msemaji wa Umoja wa Waislamu nchini Malawi akiongea na shirika la habari la BBC la Uingereza alisema kwamba sheria hiyo itakapopitishwa itakuwa ikiwabagua waislamu wa nchini humo.

  Msemaji huyo alisema kwamba Malawi ina wanawake asilimia 6 zaidi ya idadi ya wanaume hivyo kama wanaume watazuiliwa kuoa mke zaidi ya mmoja basi wanawake wengi watabaki bila kuolewa na matokeo yake kugeuka makahaba.

  Akiongelea sheria hiyo mpya, waziri wa masuala ya jamii wa Malawi, Patricia Kaliati, alisema kwamba serikali ya Malawi imepanga kupiga marufuku wanaume kuoa zaidi ya mke mmoja ili kuwalinda wanawake na manyanyaso wanayoyapata katika ndoa za mitala.

  Waziri huyo alisema kuwa tatizo hutokea kwakuwa wanaume hawawezi kuwapenda na kutoa mapenzi yao sawa kwa mwanamke zaidi ya mmoja.

  "Wakati mwanaume anapokuwa na wake wawili, watatu au wanne huwa hamna ushirikiano, mwanamke mmoja hupendelewa zaidi kuliko wenzake", alisema waziri Patricia.

  Hata hivyo katibu wa umoja wa Waislamu nchini humo, Imran Shareef Muhammed aliipinga sheria hiyo akisema kuwa mbali ya waislamu kuna makabila mengi yanayoruhusu ndoa za mitala ambayo nayo yanaipinga sheria hiyo.

  "Kama watapiga marufuku ndoa za mitala itamaanisha kuwa wanawake wengi watageuka machangudoa", alisema katibu huyo wa waislamu.

  "Kila mwanamke ana haki ya kuolewa na kuwa chini ya hifadhi ya mumewe".

  "Kwa mujibu wa sheria za kiislamu ndoa za mitala si lazima hivyo mwanaume halazimishwi kuoa mke zaidi ya mmoja, ingawa mwanaume anaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja iwapo ana uhakika ataweza kuwapa haki sawa wake zake", aliendelea kusema katibu huyo wa waislamu.

  Iwapo sheria hiyo mpya itapitishwa, wanaume ambao tayari wapo kwenye ndoa za mitala sheria hiyo haitawagusa lakini wale watakaotaka kuongeza mke baada ya sheria hiyo kupitishwa huenda wakatupwa jela.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4447898&&Cat=2
   
 2. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  A good move by malawi govt!!,sababu competition is high, hao wanawake wachache wenye 'bahati' ya kuolewa huko in my opinion watajitahidi to run their homes effectively!,hivyo kuzuia wanaume wao kutoka nje!...hivyo si kweli kuwa vitendo vya kikahaba vitashamiri!au nimeelewa sivyo?
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Unadhani hao wanaume watajali? Haiwi Ulaya huko ambako kuna sheria ya kuwa na mke mmoja na issues kama adultery zinachukuliwa seriously, na wao wanakuwa na wanawake kibao, itakuwa kwetu Afrika?

  Labda kusubiri watoto wa nje wengi na ongezeko la ugonjwa wa ukimwi.

  Hebu angalia hapa kwetu kwa wakristo ambao wanaambiwa ni ndoa ya mke mmoja, ni wangapi wameweza kufanya hivyo? Yaani kutokuwa na wanawake wa nje. Na mwanamke huwa anaelewa kwamba huyu bwana anae mume lakini na yeye anaendelea nae na anazaa nae bila ya woga.
   
 4. T

  Tall JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  watapiga marufuku mke zaidi ya mmoja na nyumba ndogo je?
   
 5. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Sipati Picha kama Vita Ikipigwa kati ya Tanzania na Malawi Wanajeshi wengi wa Malawi watakuwa Wanawake.
  Watanzania Wengi Jeshini ni Wanaume Sasa kama Wakija patikana Mateka wa Kivita wa Kimalawi nina wasiwasi watashikiliwa kwa muda mrefu hata kama Vita itaisha Mapema oi
   
 6. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  ndo U-Great Thinker Huu?
  Mweeeh!
   
 7. Me370

  Me370 JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 995
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nadhani ndoa zitafanyika kisiri bila mke mkubwa kujua na hawatoweka uthibitisho wowote
   
 8. k

  kyelatz Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  arabu thinking tanzania!!! Very premitive
   
 9. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna uthibitisho wowote kuwa wenye wake wengi hawana nyumba ndogo???? Tupeni data ndugu zetu wa kule mara na kwingineko.
   
 10. J

  Jots Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uzoefu unaonyesha Kwamba wenye wake Wengi sana wana vimada Wengi pia,sijui nini huchangia au wamezoea vitu tofauti kila siku au wao wananguvu sana?
   
 11. F

  Fursa Pesa JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2,324
  Likes Received: 789
  Trophy Points: 280
  hizo ni njama za mabeberu kuutokomeza uislamu malawi,na pindi malawi itakavyofanikisha hili basi zawadi yake ni ziwa nyasa lote.we need to be creative & not to depend external moral support even for our social way of living,if that bill pass na sisi ndo tunaenda vitani hivi tutakuwa tunapigana na malawi au mabeberu wanaopitia malawi?.we african the time is now to eradicate all forms of exploitation,mental dependent & mental slavery we can be economic giant 50yrs to come.what to do is to reject all polices which in one way or another may harm our nations interest & dignities.
   
Loading...