Malawi kuingia kwenye duru ya pili ya uchaguzi baada ya matokeo ya mwaka jana kutupiliwa mbali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Malawi inatarajiwa kurejea debeni Jumanne kwa duru ya pili ya uchaguzi katika kinyang'anyiro cha kumchagua rais miezi mitano baada ya Mahakama ya Kikatiba kutupilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika mwaka jana uliokumbwa na utata.

Rais aliye madarakani Peter Mutharika alitangazwa mshindi mwezi Mei 2019 baada ya kupata ushindi mdogo wa asilimia 38.5 ya kura zote zilizokuwa zimepigwa.

Lakini viongozi wa upinzani walipinga matokeo hayo mahakamani wakidai kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu.

Majaji walikubaliana nao na kutupilia mbali matokeo hayo Februari na kuagiza marudio ya uchaguzi huo.

Kwa sasa upinzani umeungana na kutoa mgombea mmoja ambaye atakabiliana na rais Mutharika - anayewania muhula wa pili madarakani.

Kwa miezi kadhaa sasa, raia wa Malawi wamekuwa katika mgogoro wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo. Ni zaidi ya mwaka sasa tangu mamilioni ya raia walipojitokeza katika uchaguzi wa bunge na urais.

Lakini katika uchaguzi wa Jumanne, nchi hiyo imegawanyika vikali. Kumekuwa na maandamano ya kupinga serikali pamoja na kutokea kwa ghasia ambako kumetishia nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro mkubwa zaidi.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Malawi pia amejiuzulu huku wanachama wapya wa tume hiyo wakichaguliwa ili kusimamia uchaguzi huo.

Rais Peter Mutharika (kushoto) na mpinzani wake Lazarus Chakwera


Uchaguzi huu ni kinyanganyiro cha kati ya Bwana Mutharika dhidi ya mpinzani wake Lazarus Chakwera, aliyekuwa mwinjilisti, ambaye ameunganisha upinzani chini ya muungano ambao unaonekana kuwa tayari kukabiliana na chama tawala cha Democratic Progressive ambacho kiliundwa 2004 na kaka yake rais wa sasa.

Uchaguzi huu pia unafanyika chini ya sheria tofauti baada ya mahakama kutoa uamuzi kwamba mfumo wa chaguzi zilizopita (anayepata kura nyingi hata kama hajafikisha asilimia hamsini ya kura zilizopigwa anatangazwa mshindi) ulikuwa kinyume na katiba.

Atakayeibuka na ushindi kati ya wagombea hao wawili, atakuwa na kibarua kigumu cha kukabiliana na mgawanyiko uliojitokeza na kumaliza ghasia ambazo zimekuwa zikishuhudiwa katika kipindi cha mwaka moja uliopita.

Kukabiliana na ufisadi, kupunguza umaskini na ukosefu wa ajira ni miongoni mwa masuala ya msingi katika uchaguzi huo.

Raia wa Malawi wana imani kwamba sauti zao zitasikika na kuwa Jumanne pengine huenda ikawa ndio mwanzo mpya kwa nchi hiyo.

BBC
 
Hata sisi Bongo mpaka MTU achomoke mkono ila haki itendeke. Jiwe na wenzake wajiandae vizuri,
 
Hata sisi bongo mpaka MTU achomoke mkono ila haki itendeke. Jiwe na wenzake wajiandae vizuri

Huku kwetu Jecha(Boss mstaafu wa Tume ya uchaguzi) amechukua fomu kugombea urais Zanzibar kupitia CCM.

Huna haja ya kwenda huko duniani kwenda kuona maajabu ya dunia wkt yako hapa hapa bongoland.
 
Back
Top Bottom