#COVID19 Malawi kuharibu chanjo 19,000 za Covid 19 zilizopitisha muda wa matumizi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,830
2,000
Mamlaka za afya nchini Malawi zinatarajiwa kuharibu zaidi ya dozi 19,000 za chanjo ya Covid 19 kutoka AstraZeneca baadaye siku ya Jumatano.

Wanasema chanjo hizo zimepitisha muda wa matumizi na hakuna data ya kutosha kujua ikiwa ni salama kutumiwa, kufuatia mwongozo kutoka kwa Shirika la Afya Duniani, WHO. Itakuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kuharibu hadharani chanjo zilizopitisha muda wa matumizi

Mamlaka zinasema hatua hiyo inataka kuwapa imani Wamalawi kupata chanjo dhidi ya Corona wakati inapopatikana.

Kufikia sasa, ni watu wachahe waliopewa yaCovid-19 nchini humo , haswa kwa sababu ya habari potofu iliyoenea juu ya matumizi yake.
Maafisa wanaogopa kwamba kutumia chanjo iliyopita tarehe ya kutumiwa itawaogofya raia kukubali kuchanjwa

Walakini serikali nchini Malawi ina matumaini kuwa idadi ya watakaokubali kuchanjwa itaongezeka mara tu watakapopata shehena ifuatayo kutokaCovax.
Zaidi ya Wamalawi 330,000 wamepewa chanjo hiyo

BBC Swahili
 
Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
4,127
2,000
Nchi ya Malawi imetangaza kuchoma moto chanjo ya Corona aina Astrazeneca iliyokuwa ikitolewa nchini humo baada ya wananchi kuingiwa na hofu kuwa shehena ya chanjo hizo imepitwa na wakati na itawaletea madhara.

Wizara ya afya nchini humo imethibitisha kuchoma moto chanjo hizo zilizotolewa kwa msaada ili kulinda imani kwa wananchi .

Source. Bbc swahili.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,584

Shehena iliyochomwa moto ni ile ambayo ime expire. Jambo la kawaida kabisa.

Mwendazake alichoma moto vifaranga hai sembuse chanjo iliyokwisha muda wake?

Malengo ya kuleta taharuki kuhusiana na hii chanjo yatashindwa vibaya kama vile nyungu ilivyofariki kifo cha mende!
 
Mpandisha mishahara

JF-Expert Member
Mar 1, 2014
1,345
2,000
Nchi ya Malawi imetangaza kuchoma moto chanjo ya Corona aina Astrazeneca iliyokuwa ikitolewa nchini humo baada ya wananchi kuingiwa na hofu kuwa shehena ya chanjo hizo imepitwa na wakati na itawaletea madhara.

Wizara ya afya nchini humo imethibitisha kuchoma moto chanjo hizo zilizotolewa kwa msaada ili kulinda imani kwa wananchi .

Source. Bbc swahili.
Taarifa ya lini hii?
 
My Sons Legacy

JF-Expert Member
Feb 4, 2019
3,108
2,000
Hio Inaweza kuwa ni njia nzuri ya kumuenzi Mpendwa wetu Baba yetu JPM

As far as tumekataa kumtanguliza MUNGU mbele katika janga hili na tunataka kukimbilia chanjo, kitu ambacho alitukataza

Raha ya milele umpe eeeeh bwana na jina lihimidiwe

Innalilaah wainairaih rajioun
 
Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
4,127
2,000
Hio Inaweza kuwa ni njia nzuri ya kumuenzi Mpendwa wetu Baba yetu JPM

As far as tumekataa kumtanguliza MUNGU mbele katika janga hili na tunataka kukimbilia chanjo, kitu ambacho alitukaza

Kweli kabisa mkuu
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,941
2,000
Nchi ya Malawi imetangaza kuchoma moto chanjo ya Corona aina Astrazeneca iliyokuwa ikitolewa nchini humo baada ya wananchi kuingiwa na hofu kuwa shehena ya chanjo hizo imepitwa na wakati na itawaletea madhara.

Wizara ya afya nchini humo imethibitisha kuchoma moto chanjo hizo zilizotolewa kwa msaada ili kulinda imani kwa wananchi .

Source. Bbc swahili.
Acha upotoshaji bwana hizo chanjo sio kwamba zimekwatiliwa bali zimekwisha muda wake, hata south sudani nako, zipo ambazo zimeisha muda wake wa matumizi.na ni dose 20, 000 tu, kwani WHO, waliwaambia kuwa zinaweza kutumika kwa miezi 3 zaidi toka muda wake wa matumizi kumalizika .Ila malawi wamekataa na ndio maana waameamua kuziteketeza live ili wananchi wawe na imani kuwa hizo hazipo ila zinazoendelea kutolewa ni salama.JAMANI tumeshakubaliana hizo chanjo sio za lazima kama huna imani nazo achana nazo waache wengine wapate, sasa cha ajabu kundi hilo linatumia muda mwingi sana kupotosha ili watu wasipatiwe chanjo hizo!!eti damu zinaganda yaani kati ya watu milioni 19, watu 76, 000 ndio wamekutana na tatizo hilo!!(0.0004%)hapo kwa waliosoma hesabu wanafahamu huwa inaitwajwe hiyo
 
Kwa nini ziishe muda wake wakati watumiaji wapo?

Bidhaa inayoisha muda wake ni ile inayokaa sana bila kutoka.
 
DEMBA

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,428
2,000
Hio Inaweza kuwa ni njia nzuri ya kumuenzi Mpendwa wetu Baba yetu JPM

As far as tumekataa kumtanguliza MUNGU mbele katika janga hili na tunataka kukimbilia chanjo, kitu ambacho alitukaza

Raha ya milele umpe eeeeh bwana na jina lihimidiwe

Innalilaah wainairaih rajioun
Mbona Sasa na yeye amefia hospital? Inamaana hakumtanguliza Mungu?
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,584
2,000
Acha upotoshaji bwana hizo chanjo sio kwamba zimekwatiliwa bali zimekwisha muda wake, hata south sudani nako, zipo ambazo zimeisha muda wake wa matumizi.na ni dose 20, 000 tu, kwani WHO, waliwaambia kuwa zinaweza kutumika kwa miezi 3 zaidi toka muda wake wa matumizi kumalizika .Ila malawi wamekataa na ndio maana waameamua kuziteketeza live ili wananchi wawe na imani kuwa hizo hazipo ila zinazoendelea kutolewa ni salama.JAMANI tumeshakubaliana hizo chanjo sio za lazima kama huna imani nazo achana nazo waache wengine wapate, sasa cha ajabu kundi hilo linatumia muda mwingi sana kupotosha ili watu wasipatiwe chanjo hizo!!eti damu zinaganda yaani kati ya watu milioni 19, watu 76, 000 ndio wamekutana na tatizo hilo!!(0.0004%)hapo kwa waliosoma hesabu wanafahamu huwa inaitwajwe hiyo

Ni nia yao kupotosha na kuleta wanachoita taharuki.

Ukweli mchungu tutasimama na mama Samia dhidi yao. Na tuko wengi kweli kweli.

Habari hiyo iwafikie pande zile za Lumumba wakapate kutambua hii ni awamu ya sita.
 
Samia amewapuuza
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,584
2,000
Samia amewapuuza

Hahaahaaa😂😂😂😂!

Kwa kuachana na porojo za vita vya kiuchumi, nyungu, juice za jamukaya, na maombi kufukuza Corona ni kweli kawapuuza.

Ndiyo maana ni mwendo wa mapovu kuliko ya Omo masaa 48 kwa siku kama ya yule bwana.

Mwaka huu mtayamaliza makopo yote mitaani.

Hapana kusahau, awamu ya tano haipo na hairudi tena!
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,617
2,000
Acha upotoshaji bwana hizo chanjo sio kwamba zimekwatiliwa bali zimekwisha muda wake, hata south sudani nako, zipo ambazo zimeisha muda wake wa matumizi.na ni dose 20, 000 tu, kwani WHO, waliwaambia kuwa zinaweza kutumika kwa miezi 3 zaidi toka muda wake wa matumizi kumalizika .Ila malawi wamekataa na ndio maana waameamua kuziteketeza live ili wananchi wawe na imani kuwa hizo hazipo ila zinazoendelea kutolewa ni salama.JAMANI tumeshakubaliana hizo chanjo sio za lazima kama huna imani nazo achana nazo waache wengine wapate, sasa cha ajabu kundi hilo linatumia muda mwingi sana kupotosha ili watu wasipatiwe chanjo hizo!!eti damu zinaganda yaani kati ya watu milioni 19, watu 76, 000 ndio wamekutana na tatizo hilo!!(0.0004%)hapo kwa waliosoma hesabu wanafahamu huwa inaitwajwe hiyo
Na huku kwetu hadi hizo chanjo zifike Shitimbi ambako hata umeme hakuna na kufika inabidi upande mtumbwi sijui kama hizo chanjo zitakuwa kwenye ubora wake kama wa hao wanakamati wanaodai chanjo ni salama,bado najiuliza logistic na usalama wa hizo chanjo kuwafikia wananchi huko vijijini ambako hata basi linapita mara moja kwa wiki.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom