Malawi inahitaji Taasisi imara ya Urais kama iliyopo Tanzania chini ya Rais John Magufuli, si kutoa chama tawala kuweka Upinzani

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
MALAWI INAHITAJI TAASISI IMARA YA URAIS KAMA TAASISI YA URAIS ILIYOPO TANZANIA CHINI YA RAIS JOHN MAGUFULI, SI KUTOA CHAMA TAWALA KUWEKA UPINZANI

Leo 09:22am 27/06/2020

Rais wa tatu wa Malawi, Bingu wa Mutharika kipenzi cha Wamalawi, muanzilishi wa Chama cha DPP alichokianzisha 2005 na mwaka 2009 kilibeba viti vingi vya Wabunge bungeni,alifariki Mwaka 2012 akiacha sifa njema katika nchi ya Malawi.

Rais anayemaliza muda wake,Peter Mutharika ni mdogo wa Rais Bingu wa Mutharika.

Arthur Peter Mutharika anapewa tuhuma na Wamalawi kuwa ni mtu aliyeendesha maisha yake Ulaya na kurudi Malawi kugombea Urais kwa kivuli cha sifa za kaka yake Rais Bingu wa Mutharika aliyesemekana kuwa Mzalendo kwa nchi ya Malawi.

Wamalawi wamemkataa Peter Mutharika kwa kuwa haijui Malawi kama alivyokuwa anaijua kaka yake Bingu wa Mutharika,hiyo ndiyo hali iliyowakuta Wamalawi na kuamua kumtoa Rais Peter Mutharika madarakani na kumuweka madarakani Lazarus Chakwera wa Chama Cha Malawi Congress Party.

Rejea hapo juu Chama Cha Bingu wa Mutharika ndicho Chama Cha Peter Mutharika,takwa la Wamalawi si juu ya Chama lakini juu ya Peter na watu waliomzunguka kama taasisi ya Urais,Prof Peter Mutharika ni mtu mwema lakini waliomzunguka kwa maana taasisi ya Urais ni Mafisadi,

Prof Peter Mutharika alitakiwa kuwa na ukali wa Rais John Magufuli wa Tanzania kuweza kuinyoosha taasisi ya urais na kuwafukuzia mbali ama kutowasikiliza washauri ambao daima walimpotosha Mh Rais,Sasa kama wapinzani wa Tanzania wanataka kuitoa CCM waiweke Chadema,Akti,Nccr Mageuzi au CUF basi watakuwa wapumbavu,

Malawi haiko hivyo na changamoto ya Malawi haikuwa Chama bali taasisi ya urais,na kama wapinzani wa Tanzanian wanadhani Malawi walifikiri kama wapinzani wa Tanzania basi ni kituko,

Hakuna nchi ya Africa imefanikiwa kwa style hiyo ya kutoa Chama tawala kuweka Chama Cha Upinzani. Rejea Ghana, Kenya, Sudan na Libya awa wote Wana Maendeleo ya kimkokotenge,

Afrika inahitaji taasisi imara siyo vituko vya kubadilisha vyama kutoa Chama tawala kuweka Chama Cha Upinzani, Kenya wamefanya hivyo watengeneza wizi,Ufisadi zaidi na zaidi na utawala wa kikabila kukomaa,na kuota mizizi,

Kenya hivi sasa macho yao yapo Tanzania,Kenya Mapebari yameshachukua kila kitu na kuvitawala,makabwela na walalahoi wapo sokoni wanauza kabichi,Mwokozi wa Kenya ni biashara za kimataifa,Wakenya wanavuka mipaka kuja Tanzania kuwekeza kwenye mabenki na Makampuni ya ulinzi, Shule na Clearing and forwarding,ili Wananchi wao wapate ajira mbali na nchi yao maana kila kitu nchini Kenya kimehodhiwa na Mabepari na Mafisadi,

Sudan wamebadili chama wakazalisha mfumuko wa bei wa asilimia 100 sasa hivi wanaomba mkopo wa bilioni 1.8 wa chakula, pesa ambayo inakusanywa na mamlaka ya maji ya Dawasco jijini Dar es Salaam kwa wiki mbili tuu.

Ya nchini Libya yanajulikana leo Libya kuna biashara ya watumwa,Kwa Wamalawi wenye GDP ya dola bil 7 kwao ni sawa na kuwachukua kuja kufanya kazi za ndani Tanzania kuliko kuishi kwao.

Sasa je wapinzani bado wanataka kukufunza toka Malawi au Sudan ambayo leo inflation ni asilimia 100 na wanaomba msaada wa bil 1.8 pesa inayokusanywa kwa week mbili na Mamlaka ya maji DSM achana na TRA.Watu kama Zitto au Tundu Lissu wanaotumiwa na wazungu,hao wazungu wanaowatuma wanajua wakisha ua mifumo ni vyepesi kutawala na kuchukua dhahabu,Tanzanite,Gesi na daima watapiga vita Ujenzi wa bwawa la kuzalisha Umeme ili tusiweze kujitegemea kiuchumi kwa viwanda kuzalisha bidhaa zetu, Huo upuuzi hata kwao haupo,

Wapinzani wa Tanzania wanasema tuige Mabadiliko ya Malawi,Sasa unajiuliza kwa vigezo vipi au kwa mazingira gani hasa ukirejea mazingira tofauti wanayopitia Wamalawi.

Malawi ni nchi yenye ukubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sasa Tanzania ni nchi yenye ukubwa kama wa Soviet Union,Wamalawi na Wazambia wakija kununua vitu Kariakoo wanashangaa nchi ya Tanzania ilivyo kubwa,wakipita Mbeya,Iringa, Morogoro kuja Dar es Salaam,

Kutokana na ukubwa wetu wa nchi mfano wa Soviet Union,ni vyema tungeiga Mabadiliko ya Urusi au China ya kuongeza muda kwa Rais ambaye amevunja rekodi ya Miaka minne tu kututoa kwenye nchi ya kipato cha chini hadi nchi ya kipato cha kati,

Taasisi ya Urais ya awamu hii ya tano ni imara sana pengine kushinda taasisi zote za Urais kuwahi kutokea katika mihula yote iliyopita hapa Tanzania,Pengine baada ya Awamu ya Mwinyi iliyohitaji kukopa pesa stimulas package kwa ajili ya kufufua Uchumi,

Pengine Awamu ya Mkapa ilitotaifisha Mashirika ya Umma yaliyoonekana mzigo kuyaendesha hasa kulipa mishahara wafanyakazi na gharama za uendeshaji,

Pengine Awamu ya Kikwete ilianza kusimama kwa miguu yake kwa Serikali kuanza kujiendesha lakini ikagubikwa na Ufisadi katika mifumo ya uendeshaji wa Serikali,

Awamu hii ya tano ya Rais Magufuli ndiyo tumeona "reforms" kubwa mabadiliko makubwa ya Kiuchumi kutoka kutegemea misaada na kuanza kujenga misingi ya kujitegemea,

Awamu hii ndio tumeshuhudia miradi mikubwa ya kimkakati kama reli ya Umeme (SGR) na Ujenzi wa bwawa kubwa la Umeme la Rufiji ili kuweka mazingira bora ya Ujenzi wa Viwanda vikubwa,

Hii Awamu ya Rais John Magufuli ndio awamu muhimu zaidi na haitakiwi kuingiliwa, energy inayoonekana katika awamu hii inapaswa kuachwa iendelee hata tukifikia lengo letu la Tanzania ya Viwanda itayozalisha bidhaa zetu na kuziuza Mataifa mengine kuingiza pesa ya kigeni na wakati huo huo Viwanda vikitengeneza ajira kwa mamilioni ya vijana wanaomaliza elimu ya Chuo kikuu kila mwaka,

Rejea UK Malkia yupo na atakuwepo mpaka afe , Rejea Germany Angela Markel ana miaka 14 madaraki , Rejea Russia na Putin na tumalizie China na Xi Jiping ..

Rais wa Zamani wa USA Barack Obama wakati akihudumu kama Rais akiwa ziarani South Africa alisema Africa need Strong institutions. Africa inaitaji taasisi imara siyo kubadilisha vyama,

Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1990 wakati akiwa ziarani Brazil alisema Demokrasia siyo chupa ya Coca Cola mtu anaweza ibeba kama ilivyo kutoka nchi moja hadi nyingine,kila Taifa liangalie ustawi wake mazingira na maslahi ya Taifa kwa kizazi kijacho,

Ni vyema tukamuangalia Rais Magufuli akaacha afanye reforms nyingi zaidi kwa ajili ya kuitoa Tanzania kwenye tope la umasikini,tope la kutegemea wazungu na misaada yao hadi kwenye Taifa la Tanzania litalosimama lenyewe kiuchumi bila kutegemea misaada ya Mabeberu.

Ni muda sasa kuwaza vizuri kama Watanzania ambao tunaishi katika nchi kubwa na yenye nguvu za kiuchumi,The Great Tanzania.

Tuache unyonge kwa maana Tanzania sasa inasimama katika mstari mmoja na nchi za Uchumi wa kati kama Kenya,Misri,Algeria,Morocco na tunaelekea kusimama mstari mmoja na nchi ya Uchumi wa juu,nchi ya Afrika ya kusini,

Kimkokotenge tutakuwa tumepiga bao sana kiuchumi tukimpa miaka mingine kumi Mh Rais Magufuli,tutakuwa Kama Afrika ya kusini au zaidi ya Afrika ya kusini,it can be done,play your part.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research;Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Naunga mkono Baba wa Taifa mwalimu Nyerere aliwahi kusema ukiwa na chama legelege utasababisha Serikali legelege na dhaifu.
 
Naunga mkono hoja ila Mheshimiwa awe anakubali kukosolewa pale inapobidi kwa faida ya nchi.
 
Unaelekea concept ya taasisi imara imekupitia kando kabisa kutokana na maandishi yako. Obama alisema africa inahitaji taasisi imara na sio viongozi wenye nguvu.

Malawi wameonyesha mfano bora, raisi alilala mbele na kura zao, akapelekwa mahakamani na mahakama ikafanya maamuzi independently. Raisi akataka kutumia jeshi kuwabana wananchi-mkuu wa Jeshi akasimama na wananchi.

Kinachotakiwa ni kuwa na institutions zitakazo simamia checks and balances. Kama chama tawala kitashinda kihalali sidhani kama kuna atakae taka kiondolewe madarakani. Tatizo ni kutumia njia za panya na UCHAMADOLA kung'ang'ania madaraka.
 
CCM ni taasisi imara,bahati mbaya amekabidhiwa mtu asiyefaa ambaye ni fika kama asingetumia vyombo vya ulinzi na wahuni wachache,ingekuwa mbioni kumtema kwenye kura za maoni kabla ya uchaguzi mkuu 2020.

CCM ni taasisi kubwa kuliko JPM
 
Kwa kifupi, baada ya awamu mbili, JPM at atampisha mwingine.

Katiba iheshimiwe. Mwanzilishi wa Taifa JK Nyerere alishasema yeye ndio raisi mwisho kukaa muda mrefu madarakani.

Acheni kampeni za kipuuzi.
 
Si ungeandika tu Rais aliyeshindwa uchaguzi na mpinzani? Eti "rais anayemaliza muda wake"!!😂😂
 
WEWE NI LIJINGA NA BWEGE.
Mkuu hauja itendea haki ID yako.
Jamaa anaweza kuwa ameandika mambo ya ajabu kwa mtazamo wako au wa watu wengine, kinachotakiwa ni wewe kuonesha wapi huyo mleta mada hayupo sahihi na nini kifanyike au kipi ni sahihi.

Mkosoe kwa kupangua hoja zake moja baada ya nyingine, yaani hoja kwa hoja.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom