Malawi: Baada ya Mahakama kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu, Rais Peter Mutharika atangaza kukata rufaa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1580967535190.png

Rais wa Malawi, Peter Mutharika amekosoa uamuzi wa Jumatatu wa Mahakama ya Kikatiba kuwa ulikuwa wenye kujaa dosari ambazo zilipaswa kurekebishwa.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kutolewa kwa hukumu, Mutharika ameshutumu mahakama kwa kushambulia demokrasia ya nchi hiyo.

Mapema Alhamisi, alitangaza nia yake ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama katika Mahakama Kuu.

Ni wazi kuwa sasa Mutharika hatapoteza nafasi yake bila mikikimikiki.

Baada ya kuweka wazi nia yake ya kupinga uamuzi wa Jumatatu, Mutharika anafikiria kutetea ushindi wake wa mwezi Mei.

Amesema uamuzi huo ni kitendo cha 'uharibifu wa haki', na kusisitiza kuwa inahusisha na masuala ya utaratibu na si wizi wa kura.

Muthatika amewashukuru viongozi wa upinzani kwa kupeleka malalamiko yao mahakamani, akisema kuwa nchi yenye demokrasia pekee huruhusu hatua hiyo.

Lakini amekemea uamuzi wa majaji akisema ni mwanzo wa 'kifo cha demokrasia ya Malawi.'

Upinzani umekuwa ukishangilia uamuzi wa mahakama kama mwanzo wa uwepo wa demokrasia nchini humo, lakini huenda rufaa inayokuja inaweza kuzima furaha hiyo.

Chanzo: BBC Swahili
 
I hope one day Katiba yetu itafanyiwa massive changes ili turuhusu matokeo ya Urais yaliyotangazwa na NEC yawe challenged Mahakamani. It is beyond me how akina Msekwa walikubali kupitisha udwanzi kama ule.
 
TURUDIE MANENO HAYA YA RAIS MUTHARIKA
"Muthatika amewashukuru viongozi wa upinzani kwa kupeleka malalamiko yao mahakamani, akisema kuwa nchi yenye demokrasia pekee huruhusu hatua hiyo"
SIASA YA AFRICA BHNA!INABOA SANA,
 
AAAA FIIII LIII KAAA.... who cursed this beautiful continent.

Rais wa Malawi, Peter Mutharika amekosoa uamuzi wa Jumatatu wa Mahakama ya Kikatiba kuwa ulikuwa wenye kujaa dosari ambazo zilipaswa kurekebishwa.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu kutolewa kwa hukumu, Mutharika ameshutumu mahakama kwa kushambulia demokrasia ya nchi hiyo.

Mapema Alhamisi, alitangaza nia yake ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama katika Mahakama Kuu.

Ni wazi kuwa sasa Mutharika hatapoteza nafasi yake bila mikikimikiki.

Baada ya kuweka wazi nia yake ya kupinga uamuzi wa Jumatatu, Mutharika anafikiria kutetea ushindi wake wa mwezi Mei.

Amesema uamuzi huo ni kitendo cha 'uharibifu wa haki', na kusisitiza kuwa inahusisha na masuala ya utaratibu na si wizi wa kura.

Muthatika amewashukuru viongozi wa upinzani kwa kupeleka malalamiko yao mahakamani, akisema kuwa nchi yenye demokrasia pekee huruhusu hatua hiyo.

Lakini amekemea uamuzi wa majaji akisema ni mwanzo wa 'kifo cha demokrasia ya Malawi.'

Upinzani umekuwa ukishangilia uamuzi wa mahakama kama mwanzo wa uwepo wa demokrasia nchini humo, lakini huenda rufaa inayokuja inaweza kuzima furaha hiyo.

Chanzo: BBC Swahili

Jr
 
Back
Top Bottom