Expedito Mduda
JF-Expert Member
- Sep 22, 2009
- 534
- 254
Watanzania wamebahatika kuwa katika nchi yenye kila namna ya utajiri. Mali asili nyingi zinatumiwa na watu ili kujiingizia kipato.
Moja kati ya maliasili zetu ni maziwa ambamo mwamo tunavua samaki. Pombe Magufuli ndo waziri anayehusika na mamabo haya ya samaki na vikolombwezo vyake.
Waziri amejitahidi sana kuhakikisha kuna kuwa na uvuvi endelevu. Moja ya mkakati aliofanya ni kuhakikisha wavuvi hawavui samaki wadogo na kuhakikisha hili nyavu zote ambazo zina matundu madogo ambayo yanafanya samaki wadogo wavuliwe zilikuwa zinakamatwa na kuchomwa. Kwa hili hongera sana. Kwa kweli waziri Magufuli tatizo lake moja tu. Nalo ni kuwa katika chama ambacho hakiaksi ufanyaji kazi wake. Wahenga walisema "Samaki mmoja akioza wote wameoza".
Kuna mwenzetu hapa JF ni mtu wa kutoa viroja muda wote. Huyu si mwingine bali ni kada wa Chama fulani. Malaria Sugu eti anasema kwa kuwa sehemu ambazo kuna wavuvi wa samaki na ko walipata kura na ndo maana wakapata 61% kwenye uchaguzi, basi hawa wavuvi waachwe wavue hata samaki wadogo kama shukrani ya kuwachagua.
Ndugu zangu hivi kweli huyu ni mtu au? Kuna wakati huwa nafikiri sana kuwa huyu anaweza asiwe mtu maana viroja vinavyotoka mdomoni mwake utakimbia!!
Eti kwa sababu wavuvi ni wapiga kura wao hivyo waachwe wafanye uvuvi haramu.
Haya jamani huyu naye ni Mtanzania mwenzetu!!!!