(MALARIA) Siasa inatumaliza mpaka Afrika itabaki milima na mabonde!

bundas

Member
Aug 1, 2011
79
9
Wadau tuwekane sawa hapa! Hili tatizo kubwa mno huku kusini mwa jangwa la Sahara (Maralia)! ni kweli ufumbuzi wake ni huu tunaotangaziwa na Wizara ya afya na vijiwe vya mawaziri na ndugu zao(NGOs)?

Ati tuyatokomeze maralia kwa kutumia vyandarua vyenye dawa hii inaingia akilini kweli? vyandarua sasa vinatumika kwa uvuvi wa dagaa kule Kilombero na kungineko na shamelessly tunashindwa ku-admit! Ni kweli dawa mseto yenye (rangi ya kijani )!!! itatokomeza malaria, je ni kweli kwamba malaria haikubaliki huku Afrika! Swali kwa wadau wote ,Je mwajua ya kwamba enzi za mapinduzi ya kilimo Marekani ilikuwa na kiwango cha juu cha mbu wanaoeneza malaria? tunajiuliza kweli kwamba walifanya nini kuwaangamiza?

Ni gharama kiasi gani kama kweli TZ imefanya tathmini na kugundua kwamba labda kiasi kinachihitajika ni shs ngapi? tunawaacha ma armatures kama kina Marry Nagu akishahongwa kwamba atapata mgao iwapo malaria yataendelea kuwepo ili Viwanda vya kutengeneza Vyandarua na Dawa za malaria pamoja na research institutions zisikumbwe na unemployment je tunajua huu uhusiano jamani?????

Niwaambie ukweli ni kwamba, tukifanya tatmini, tuka piga na mahesabu ya fedha kiasi gani zinahitajika kutokomeza malaria nchi nzima bila ufisadi hapo i am telling you, in one month malaria will be a history in this world! Otherwise MALARIA INAKUBALIKA MNO NA SERIKALI NDO MAANA INADHAMINI MATANGAZO YENYE UHAFIFU NA KUKARIBISH VIFO!!!

Natoa hoja!
 
maralia,....maralia....MARALIA!!!!???Msomi(Great Thinker?) anapodhihirisha makosa madogo kama hayo hata makala sisomi tena
 
maralia,....maralia....MARALIA!!!!???Msomi(Great Thinker?) anapodhihirisha makosa madogo kama hayo hata makala sisomi tena

sasa wewe ndio unafanya nini..........u-great thinker wako uko wapi?......this is typical of us!............to be quite honest/hapana shaka........unajua kabisa mleta mada anaongelea nini................badala ya kurekebisha na utoe hoja wewe unakimbia............anyway............

Back to the mada,

Ni kweli Ndugu mleta mada......naunga mkono hoja yako..........serikali haina nia ya kuutokomeza ugonjwa huu wa Malaria..........ni biashara ya vyandarua kwenda mbele
 
Ni sawa na waziri mwenye dhamana ya afya, dk mponda nilipomsikia bungeni zaidi ya mara 3 akisema CCRBT (!!?)
 
maralia,....maralia....MARALIA!!!!???Msomi(Great Thinker?) anapodhihirisha makosa madogo kama hayo hata makala sisomi tena
Can you come again!!! Wajua winners never quit no matter how long it takes to be victorious, again don be angry and start running with guns, that what they real want from you, it is time to get up and start concentrating and not only thinking! Kwenye kitongoji changu natumai kuanzisha utaratibu wa kushirikian nyumba hadi nyumba kuwa-convince watu kunyunyiza dawa mitaa kwa ujumla, BUT DO NOT think otherwise, serikali ishakuwa kilema hii!
 
Hii inadhihirisha uwezo mdogo wa kufikiri wa viongozi wetu. Vita dhidi ya malaria ni kupambana na chanzo chake na si matokeo yake. Net za mbu zinapambana na matokeo na si chanzo kwa hivyo vita hii tayari imesha tushinda kama maisha bora kwa kila mtanzania yalivyokwisha tushinda. Mi naona watu wanafanya biashara tu kupitia tatizo hilo....hivi mambo ya gen shimbo yaliishia wapi bandugu?
 
Malaria ni tatizo zito na hata huko mahosptalini wapimaji ni vilaza hivyo tutakwisha. Jana binti yangu kaenda dispensary ya pale home amepima malaria wakakuta wadudu 9 ; matibabu yake ni dawa mseto doz moja au kwinini drip 7. ok wakachukua mseto kabla ya kunywa dawa tukaamua twende tukahakikishe regency hosp. tukakuta malaria hakuna, haikutosha tukaamua kwenda aghakan hosp. tukakuta malaria hakuna dr. akasema ni mafua ndiyo yamemletea homa.
 
Vyandarua na dawa za miseto, kijani whatever ni sawasawa na biashara ya majeneza, whos the customer?
 
Malaria ni tatizo zito na hata huko mahosptalini wapimaji ni vilaza hivyo tutakwisha. Jana binti yangu kaenda dispensary ya pale home amepima malaria wakakuta wadudu 9 ; matibabu yake ni dawa mseto doz moja au kwinini drip 7. ok wakachukua mseto kabla ya kunywa dawa tukaamua twende tukahakikishe regency hosp. tukakuta malaria hakuna, haikutosha tukaamua kwenda aghakan hosp. tukakuta malaria hakuna dr. akasema ni mafua ndiyo yamemletea homa.
Pole sana Mamndenyi, inazidi kudhihirisha mpaka huku ndani, wanaona vifaa vya kupima malarai vita-expire, wanaona madawa yata-expire wanaona foleni za wagonjwa kujaa ma-hospitalini zitapungua, wanaona biashara zao za majeneza zitapungua mapato, it is well a different perspective, weye unazungumzia kutokomeza mwenzio ana-encapsulate kueneza huku headers na trailers zinasema ati haikubaliki! hiyo ni moja tu! hebu niulize swali UKIMWI ukitokomezwa TACAID na NGOs za aina yake si watakosa ajira? then comeback and re-think kama kuna udhati wowote wa kutokomeza magonjwa haya ambapo kule ulaya na marekani wameanzisha viwanda na research institutes zinalipwa na nchi zetu hohehahe mahela mengi ili kutuangamiza!
 
Mimi hili la kampeni za malaria wanalofanya serikali nalifananisha na mtu anaejikwaa na kuangalia pale alipodondoka kutaka kujua kilichomwangusha badala ya kuangalia alipo jikwaa. Tizama quba waliangalia walipojikwaa na sasa malaria kwa ni historia
 
Back
Top Bottom