Ngigana
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 2,103
- 1,440
Siku za karibuni imesemekana kuwa kuna mbu wengi sana jijini Dar na hasa huko Muhimbili. Wakati huo kuna taasisi inayojishughulisha na kutokomeza malaria (mpango wa Taifa wa kutokomeza malaria). Hawa walioko Muhimbili nani awashughulikie maana inaonekana hakuna anayehusika na kampeni ya kutokomeza mbu. Je kauli mbiu yetu imekosewa? Nadhani Mbu hakubaliki na siyo malaria haikubaliki. Naomba nisikie mchango wenu waungwana ili ikibidi labda policy makers wetu wafikirie upya kuhusu hizi kampeni za malaria haikubaliki.