Malalamiko ya wakristo wa zanzibar kunyimwa nafasi za uongozi wanapogombea.

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
581
Malalamiko hayo yametolewa mbele ya mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein
wakati alipokuwa na mazungumzo na viongozi na Waumini wa Madhehebu ya dini ya Kikristo huko katika ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni.
Wamesema kuwa kumekuwepo na ubaguzi mkubwa wa kidini pale kunapotokea nafasi za uongozi , ambapo wakristo wakigombea hunyimwa nafasi hizo kwakua wao ni wakiristo , wamesema kuwa jambo hilo huwakatisha tamaa sana na kuwafanya wao kuwa kama si watanzania na kuwa hawana haki kwenye nchi yao ya kuchaguliwa kuwa viongozi ...
Naye mke wa Rais Mama Shein katika kujibu malalamiko hayo alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba chini ya uongozi wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein inathamini sana mchango wa waumini hao kwa maendeleo ya ustawi wa jamii.

Alisema kuwa jitihada za taasisi za madhehebu ya dini zinatambuliwa katika kuungana na Serikali katika kuwapatia wananchi huduma ambali mbali za kijamii zikiwemo afya na elimu.

Alieleza kuwa jamii inatambua na kuthamini sana jitihada za waumini hao za kuhubiri amani hapa nchini.

Hivyo, Mama Shein alitoa wito kwa waumini hao wasichoke na waendelee kuilinda amani kwa nguvu zao zote kwani pasipo amani hakuna maendeleo wana waumini hawawezi hata kumuabudu Muumba wao.
Pia, Mama Shein aliwasisitiza waumini hao kuwasimamia watoto na vijana ili wawe makini katika matumizi ya mitandao ya kijamii sambamba na kujiepusha na madawa ya kulevya na kutoshiriki katika vitendo vyote vya kuvunja sheria.

Mapema Mama Fatma Karume nae alitumia fursa hiyo kueleza uhusiano wa kihistoria uliokuwepo kati ya waumini wa dini ya kikristo na dini nyengine hapa nchini huku akiwasisitiza haumini hao kuzidisha mashirikiano na kuendeleza amani na utulivu uliopo hapa nchini.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Maudline Castico aliwaeleza waumini hao.... huyu sasa ndo alimwaga chunvi kwenye kidonda kwa maneno yake (...............................................................................)
 
Unaulizwa A unajibu X . Imani zetu hizi ubinadamu unakuwa mbele kuliko hata huko kumtukuza Mungu, watu wametawaliwa na selfish.
 
Arrroooo mtoa mada usitutoe katika hoja za msingi za kujenga uchumi wa nchi yetu. Zanzibar hilo jambo halitakuja litokee! By the way zanzibar ni nchi ya kigeni sisi haituhusu kabsaaa!
 
Sheikh Khalifa aje atufafanulie hili maana huku bara amekuja na kila aina ya data kuonyesha umahiri wake katika kutetea usawa kwenye teuzi.
 
Back
Top Bottom