mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,771
- 7,138
Mh. Lukuvi,
YAH: MALALAMIKO YA WAKAZI WA BUNJU JUU YA UBADILISHAJI HOLELA VIWANJA VYA MAKAZI KUWA VYA BIASHARA.
Mh., Bunju (Mradi wa viwanja elf 20 vya makazi bora) kumekuwa na ubadilishwaji holela ya matumizi sahihi ya viwanja vilivyopimwa kutoka kuwa makazi kuwa / magodown. Tabia hii ambayo inafanywa na wenye fedha, inaelekea kuleta uharibifu wa mipango miji kwani plan iliyoandaliwa haifuatwi hivyo itafanya sehemu husika iliyoandaliwa kama makazi ya mfano kuwa ya hovyo kama tunavyoona sehemu nyingine.
Kwa ujumla wananchi kwa pamoja tunapinga ubadilishwaji huu holela. Tunakuomba uingilie kati uwaagize watendaji wako wastishe zoezi la kubadilisha viwanja badala yake uwasisitize mwombaji afuate kilichoombwa kwa manufaa ya wakazi wote. Wakati tunaandika barua hii, kuna mtu ameomba kujenga majengo ya biashara, baa, kumbi za starehe, cha kushangaza kabla ya mwisho wa pingamizi, tayari ashaanza ujenzi.
Naambatanisha Tangazo lake aliloliweka, tunataka kujua aliyemruhusu kujenga kabla ya siku tajwa. Pia tunawaomba watendaji wako wafuatilie vibali vyote vya ujenzi kwani Bunju Beach inaelekea kuwa sehemu ya ujenzi holela.