Malalamiko ya kuyumba kwa uchumi yanatolewa na wapiga dili tu?

ipyax

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
3,976
6,152
Malalamiko ya kuyumba kwa uchumi yanatolewa na wapiga dili tu?

Watu wengi wamekua wakilalamika kuhusu mkwamo wa kiuchumi uliopo sasahuku pia baadhi ya watu wengine wakiwaponda hao walalamikaji kwamba walikua wapiga dili tu toka utawala uliopita,sasa mirija ya dili imezibwa ndiyo maana wana lalamika.Nikiwa mjasiriamali nikaona nilete changamoto ambazo naziona kwenye shughuli zangu mtaani ambazo sikuwahi ziona kabla ili kuonyesha kwamba kweli kuna mkwamo mkubwa tu wa kiuchumi.

mimi na jamaa zangu tuna viduka katika soko moja kubwa tu huku nyanda za juu kusini na biashara zetu zilikua zinaenda vizuri sana mpaka december mwaka jana.Mauzo ya laki 5 mpaka 7 kwa siku lilikua jambo la kawaida kabisa na wateja wetu ni raia wa kawaida tu,waajiriwa serikalini,sekta binafsi,wamachinga nk.Baadhi yetu walikopa bank ili kutanua biashara zao huku hizo kazi zikitarajiwa kuleta marejesho kila mwisho wa mwezi bank.

kuanzia january mwaka huu kumekua na mdororo mkubwa sana wa kibiashara kwetu kwa kushuka kiwango cha mauzo sana,mtu alikua akiuza laki 5 mpaka saba kwa siku lakini sasa 80 mpaka laki na 50 max. mjasiriamali huyu kipato chake kimeshuka zaidi ya 50% ndani ya mwaka mmoja huku akiwa na marejesho ya mkopo bank kila mwezi lakini pia hununua mzigo kutoka viwanda vya ndani kama Murzah,Mo,Bakhressa nk.Imebidi wengine wafunge maduka kwa sababu biashara mbaya na pia rent iko juu.

Kufunga biashara kuna athiri wafanyakazi waliopoteza ajira,viwanda vya ndani vimepoteza mteja,serikali inakosa mapato,bank ame default mkopo na sio peke yake ni wafanyabiashara wengi na hata kama bank zitapiga mnada mali sio rahisi kupata pesa ya kutosha kama mteja angemudu kulipa mkopo.Kuna multiplier effect ambayo ina athiri sekta nzima ya kibiashara na uchumi ,ni muhimu serikali iingilie kati ili kuleta relief sio kwa kugawa pesa bali kuongeza mzunguko wa pesa .
 
Wanamiwani ya mbao na hawataki kuthibitisha hilo basi ngoja tuone,muda ndio huwa unaongea
 
Mimi sina shida na kuzuia wapiga deal ila basi ela ikiwa scarce basi vitu vishuke bei..
Maana vitu mtaani vinazidi panda bei. Unga wa sembe umepanda bei, mafuta ya kupikia yamepanda.
Pesa inakuwa adimu badala ipande thamani inazidi kushuka thamank.
 
Serikali haina pesa imefulia..je na serikali akiwemo rais ni wapiga dili???

Ukiangalia anayesema wanaoona maisha magumu ni wapiga deal hana hata elimu ya uchumi achilia mbali kumiliki kiduka cha mpesa
 
He! hatari hii.. tulitaka afadhari tumepata kemikali.. mategemeo ya wazazi ni mtoto kukuwa sasa hapa sijui nisemeje sijui utapiamlo! au ufupi duh!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom