Malalamiko mbalimbali kuhusu mabadiliko ya vifurushi yaliyofanywa na mtandao wa Tigo kwa mwaka 2020

Tigo wanadhani sisi ni wajinga.
Wametushawishi tununue line za chuo kwa bei kubwa.
Walipoona tumefanya hivyo, kabla ya mwaka kuisha wakaondoa huduma hiyo.

Nami sasa naiondoa line yao kwangu, kwa vile kilichonivutia wamekizuia kitapeli!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kipindi walikiweka kweli nilikifumania siku moja nikajiunga nilivyojiunga nimetumia siku moja tu kesho yake dk zimeisha 120 na nilijiunga usiku nikaongea dk chini ya 10, mb zikaisha nikaona siyo mbaya nikajiunga kesho yake hiki kikadumu ila kilivyoisha kucheck kwenye menu kimeshanyakuliwa kimebaki cha buku 3
 
Yaani nimenunua jana asubuhi vocha ili nijiunge kifurushi hicho maana nimewahi kujiunga . Kilichonitokea ndiyo hicho ulichokiandika . Nami nimeupotezea mtandao huu , nitatumia voda tu mpaka tigo watajapojitathimini . Ila sina uhakika kama salio langu lipo maana ni wepesi kukwapua kama tai . Tutaonana Mungu akipenda Tigo
 
To be honest kwangu nilivunja laini yangu ya Tigo ambayo niliisajili kwa alama za vidole sababu ya kubadilishiwa bando kutoka 2000 mpk 3000 per week

Baadae nikakutana na watu wao wa sales & promo wanajinadi kusajili laini za chuo. Nikawaeleza kisa changu, wakanichongea laini mpya yenye special namba

Toka May nakula dakika 250 all net, Gb 1.3 na sms 100 weekly.

Siku wakibadili nami naruka ukuta.
 
To be honest kwangu nilivunja laini yangu ya Tigo ambayo niliisajili kwa alama za vidole sababu ya kubadilishiwa bando kutoka 2000 mpk 3000 per week

Baadae nikakutana na watu wao wa sales & promo wanajinadi kusajili laini za chuo. Nikawaeleza kisa changu, wakanichongea laini mpya yenye special namba

Toka May nakula dakika 250 all net, Gb 1.3 na sms 100 weekly.

Siku wakibadili nami naruka ukuta.
Unamruka ukuta nani mkuu?
Muulize mwijako kamwaga mtondoro wiki nzima!
 
MALALAMIKO MBALIMBALI YALIYOTOLEWA NA WADAU:
Habari za mida hii wakuu, hivi haya mabadiliko ya bando za Tigo ni kwangu tu au kwa watu wote? Maana daah bando zimekuwa ghali sana kwa sisi Wananchi wanyonge.


=====

---

---


---

---

---

---

Tigo wamepandisha bando toka 1500 mpaka 3000 kwa wiki, yaani mbaya sana , tushaurini mtandao wa kuhamia.
=====

WADAU WENYE MTAZAMO TOFAUTI:

---

---

---




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnauza vifurushi halafu mnatupangia matumizi mmetoka dakika za usiku mmehamia longa nae.

Nipe dakika zangu zote nijue nahangaika nazo vipi.
 
Back
Top Bottom