Malalamiko kwa NSSF: Inawezekana Mwajiri alipe michango ya Mwanachama lakini Mhusika asiione?

F35-Bomber

JF-Expert Member
Mar 18, 2017
1,245
961
Habari za mwaka mpya wanajamvi.

Poleni na jukumu la kulipa ada maana zamani watoto ndio tulikua tunakula ada ila siku hizi hao watoto wameshakua wazazi kwahiyo tabia bado inaendelea.

Naomba niende moja kwa moja kwenye hoja ya msingi.

Malalamiko yangu kwa uongozi wa NSSF embu wahusika jaribuni kufuatilia watendaji wenu kabla hamjatumbuliwa na kuaanza kutia huruma.

Hivi inawezekana vipi mwajiri analipa michango ya mwanachama lakini mwanachama haoni michango yake NSSF?

Nimeangalia jana 05.01.2020 hakuna michango toka mwaka 2018.

Je, michango yangu iko wapi, ukiuliza wanakujibu system inasumbua. Is it possible?

Kazi kwenu msijesema mwewe akukuambia.
 
Back
Top Bottom