Malalamiko kuhusu uhalali wa matokeo ya Urais kama ilivyowekwa katika rasimu ya Katiba chini ya Jaji Warioba

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
cdwce.png

Ibara ya 81.-(1): Endapo mtu yeyote aliyeshiriki kama mgombea katika nafasi ya Madaraka ya Rais katika Uchaguzi wa Rais hakuridhika na matokeo ya uchaguzi huo, anaweza kuwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Juu kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi

(2) Malalamiko ya kupinga Matokeo ya Uchaguzi wa Rais yatawasilishwa Mahakama ya Juu ndani ya muda uliowekwa na sheria ya nchi baada ya siku ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa Rais

(3) Mahakama ya Juu itasikiliza na kutoa uamuzi wa shauri la kupinga Matokeo ya Uchaguzi wa Rais ndani ya muda utakaoainishwa na Sheria ya Nchi tangu kupokea malalamiko yaliyowasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (2) na uamuzi huo utakuwa wa mwisho

(4) Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (3), Mahakama ya Juu inaweza kutoa uamuzi bila kutoa sababu za uamuzi na sababu hizo zikatolewa ndani ya kipindi kisichozidi siku thelathini tangu siku ya
kutoa uamuzi

(5) Iwapo Mahakama ya Juu itaamua kuwa matokeo ya Uchaguzi wa Rais si halali, Uchaguzi wa Rais utarudiwa ndani ya siku sitini baada ya uamuzi kutolewa
 
Ilikuwa imekaa vizuri sana,kama unayo rasimu yote share humu mkuu ili tujikumbushe zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom