Malalamiko dhidi ya baadhi ya wabunge;tunavuna tulichopanda.

HORSE POWER

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
2,077
1,392
Habari wanaJF,

Baada ya 'mnyukano' mkali wa kati ya bunge,wanaharakati,wanahabari,wapinzani,chama tawala na wananchi juu ya bunge kuonyeshwa au kutoonyeshwa 'live',hatimaye 'mshindi amepatikana'.

Bunge sasa linaonyeshwa moja kwa moja.Mnyukano huu ulikua tukio langu la pili la ajabu tangu mwaka huu uanze.
Baada ya watu kuanza kinachoendelea huko bungeni,malalamiko yameshaanza kurindima mitaani na kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya baadhi ya wabunge. Na kwa kweli mbunge makini anapimwa kwa hoja zake.Tunafahamu hoja za maana ziko upande upi na wale 'bora liende' wako upande upi.

Kiufupi ni kwamba hawa wabunge wanaolalamikiwa wamechaguliwa na waliomo miongoni mwetu.Hawakwenda wenyewe kule.Hili liko wazi.Sasa kwa kuwa jamii inayoumwa huchagua viongozi wanaoumwa,tumepoteza uhalali wa kulalamika kwa kuwa unachokigua uwe tayari kuishi na matokeo yake.

N.B.
Kutatua tatizo lile,kwa fikra na akili ile ile,kwa mbinu ile ile na kutarajia matokeo tofauti.
 
Back
Top Bottom