MALALAMIKO: BODI YA MIKOPO INAWADHURU HAKI WANAFUNZI WA CHUO CHA DAR INSTITUTE OF TECHNLOGY (DIT) KWA KUWAKATA HELA ZAO ZA ADA NA KUJIKIMU.

Malo Robi

JF-Expert Member
May 16, 2017
322
542
Salaam wanajamvi.....

Kama kichwa kinavyojionesha, Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania (HELSB) na washirika wake pamoja na serikali wameamua kuwakata wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu hela za ada, kujikimu na mafunzo kwa vitendo.

Hili jambo lilianza kiutani utani lakini wanafunzi wanapofuatilia wanazungushwa tuu na kupigwa mikwara mizito na vitisho kutoka bodi ya mikopo kwa kushirikiana na chuo!

Waadhirika wakubwa wa jambo hili ni wengi sana na hawana pa kuongelea kwani bodi imekuwa ikiwajibu kwa nyodo na matusi mengi.
Hii nchi kwa sasa kila mtu kwenye kitengo chake anakula awezavyo huku hakuna kumhoji na ukidhubutu unaumia.

Wanafunzi wengi wameahirisha mwaka kwani ukizingatia chuo hiki cha DIT kimeongeza kwa zaidi ya asilimia ishirini (20%) karo yake na wamelazimisha kuanza kutumika mwaka wa masomo unaokuja kwa wanafunzi wote hata wanaoendelea tofauti na utaratibu ambao unasema karo mpya huanza na wanafunzi wanaoanza (first year). Hiki chuo ni mateso, walimu ni corrupt, wababe na hawafundishi kutwa mizunguko tuu. (WIZARA HUSIKA IKIMULIKE HIKI CHUO NA MKUU WAKE KWANI KIMEOZA NA KINANUKA UOZO).

Waziri wa elimu mama Ndalichako fuatilia hili suala ujiridhishe kwani wanafunzi hawaelewi hatma yao kwenye jambo hili!

Bodi ya mikopo waache hii dhuruma kwa watanzania wanyonge!
 
Hii tunaenda week ya tano hamajatoa matokeo utaratibu wa chuo umekua mbovu kupita maelezo zamani Ila week ya pili tu matokeo mshayapata

Kibaya zaidi kuna wanafunzi ambao wanahitaji kuendelea na masomo kwa ngazi ya bachelor wanasubilia matokeo ili waweze kupata AVN na transcript ili waweze kuapply vyuo muda unazidi kwenda kiasi kwamba inawanyima fursa kwa wanafunzi wanaotaka kuendelea na masomo

Naucheleweshwaji wa kutuma matokeo NACTE
 
Pale sipaelewi kabisa, hadi sahivi matokeo bado hapa mtu hujui unasupplimentary ngapi halafu unapewa two weeks kujiandaa. dah nimesota sanaa pale nitawakumbuka daiama hawa jamaa kaswaa kila tittle ya project nilipeleka aliikataa, wa pili kanuti huyu jamaa mtihani wake ni kutafuta mpango nusu kupata B we mwanaume asee, na wa mwisho jovitas kato dah huyu mzee wa assignment ni complicater sanaa , lakini namshukru mungu nimemaliza salama ilikuwa safari ndefu sanaa nitakikumbuka sana hiki chuo .
 
Salaam wanajamvi.....

Kama kichwa kinavyojionesha, Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania (HELSB) na washirika wake pamoja na serikali wameamua kuwakata wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu hela za ada, kujikimu na mafunzo kwa vitendo.

Hili jambo lilianza kiutani utani lakini wanafunzi wanapofuatilia wanazungushwa tuu na kupigwa mikwara mizito na vitisho kutoka bodi ya mikopo kwa kushirikiana na chuo!

Waadhirika wakubwa wa jambo hili ni wengi sana na hawana pa kuongelea kwani bodi imekuwa ikiwajibu kwa nyodo na matusi mengi.
Hii nchi kwa sasa kila mtu kwenye kitengo chake anakula awezavyo huku hakuna kumhoji na ukidhubutu unaumia.

Wanafunzi wengi wameahirisha mwaka kwani ukizingatia chuo hiki cha DIT kimeongeza kwa zaidi ya asilimia ishirini (20%) karo yake na wamelazimisha kuanza kutumika mwaka wa masomo unaokuja kwa wanafunzi wote hata wanaoendelea tofauti na utaratibu ambao unasema karo mpya huanza na wanafunzi wanaoanza (first year). Hiki chuo ni mateso, walimu ni corrupt, wababe na hawafundishi kutwa mizunguko tuu. (WIZARA HUSIKA IKIMULIKE HIKI CHUO NA MKUU WAKE KWANI KIMEOZA NA KINANUKA UOZO).

Waziri wa elimu mama Ndalichako fuatilia hili suala ujiridhishe kwani wanafunzi hawaelewi hatma yao kwenye jambo hili!

Bodi ya mikopo waache hii dhuruma kwa watanzania wanyonge!

Mkuu, huenda ni kweli chuoni kwenu mnakumbwa na madhila mengi, ila nashauri tu kwamba ungejikita kwenye hoja moja na uieleze vizuri ili na sisi tuelewe na kama pengine kuna la kushauri au kusaidia tujue tunafanyaje.

Kichwa cha uzi wako kinahusu ninyi kukatwa hela na bodi ya mikopo, naomba ulieleze hilo kwa kina tafadhali, mimi bado sijaelewa hapo.

Vinginevyo uzi ungesomeka "matatizo mbalimbali katika chuo.....''

Nisaidie namimi kuelewa, lakini natoa pole kwa magumu yote mnayopitia.
 
Back
Top Bottom