Makwaiya wa Kuhenga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makwaiya wa Kuhenga

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Raia Fulani, Jul 22, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  mzee huyu kwa muda mrefu amekuwa mstari wa mbele kuibua mada mbalimbali katika jamii yetu na kutufungua macho katika mengi katika kipindi chake cha Je, tutafika? Lakini hivi karibuni nimeona mtazamo wake mwingine katika mada zake anazozileta. Awali sikujua kama Makwaia ni muislam, ila nimejua, tena anaweza kuwa kati ya wale extremists. Nilimwona katika mada ya Palestina, pamoja na zingine na hii hali ya sasa ya udini bongo. Namna anavyowasilisha mada zake na namna anavyowachagua wazungumzaji na namna anavyoonekana akiongea ni dhahiri kuna kitu ndani yake. Nadhani ukifungua moyo wake utaziona OIC, kadhi na korokoro zingine dhahiri. Akitaka mijadala yake iende sawa awaalike na na hao walioandaa hiyo ilani wanayosema ni ya kidini ilhali ni secular kabisa ila tu walioandaa ndio waamini (sio waumini!)
   
 2. l

  libidozy Member

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha udini huna lolote la kutuhabarisha kwanza shule yenyewe huna unataka kupambana na Makwaia!Kamalizie shule yako halafu ndio uje jamvini
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  karibu mtoto
   
 4. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hayo ndio majibu unjayo stahiki. Ukipanda pumba utavuna pumba.
   
 5. nkawa

  nkawa Senior Member

  #5
  Jul 23, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mziwanda.
  Unachosema hata mimi nimekiona...namna anavyowasilisha mada anaegemea upande mmoja na hata anaowaalika katika kipindi sijui anatumia kigezo gani. Kwa mfano kile kipindi cha Je tutafika? walipoongelea ule waraka wa kichungaji........alitakiwa awaite waliouandaa/kuundika ili wajibu kipengele kwa kipengele.
  Pole kwa majibu uliyopewa hawa wenzetu waamini baadhi ndivyo walivyo wanapanda jazba badala ya kusimamia kwenye ukweli.....
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kweli mkuu umenena. kuna watu humu wanatumia hisia tu badala ya mantiki. kama mtu anakosea hatuna budi kusema kweli. Makwaia ana lake jambo
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ulikuwa unajua ni Dini gani?.
   
 8. A

  August JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  tena wiki hii inayoishia 25/07/09 ameongelea tamko la maaskofu na kudai Ilani ni Manifesto, kwa translation yake, wakati ilani inaweza kuwa taadhari.na unaweza kukuta ilani inaweza kuwa na maana nyingi katika kamusi
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kwa jina lake nilijua ni dugu moja na kingunge (joking). Cha msingi kuhusu huyu mzee wetu aangalie asizeeke vibaya tu. Nchi ina ombwe (vacuum) la uongozi bora. Kama watu wenye imani zao wanaweza kutoa suluhisho kwa manufaa ya wote mbona wengine wanabweka tu? Waonyeshe mbadala basi
   
 10. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Makwaiya ni mchambuaji mzuri lakini ni mchochezi wa kidini, hata mimi nisiyekuwa na dini naliona hilo.
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Kimaumbile kila binadamu kuna mambo anayoyaamini yasiyoonekana na amabayo kwa kuamini kwake hayo mambo hufanyika kuwa ya msaada wake pale anapofikia ukomo wa kufikiria na hiyo imani ndiyo inaitwa DINI

  Kingunge anayo DINI kama ilivyo kwangu na wewe, tofauti ya Kingunge ni kwamba dini yake haijaandikwa kwenye karatasi na kutafsiriwa katika lugha mbalimbali kama zilivyo DINI nyingine mbalimbali.

  La msingi hapa ni kwamba mtu anapokuwa anaTETEA msimamo wa DINI yake neno "MANTIKI" linapotea kichwani kwake kwa maana ile imani yake ya DINI inasimamisha uwezo wa "ubongo" wake kufikiri "kawaida" na hivyo yawezekana akaonekana kama "mwendawazimu" kwa watu wenye imani ya DINI tofauti.

  Ndiyo maana nchi za kisoshalisti zilikataa sana (nyingine mpaka leo) watu kuamini katika DINI fulani fulani kwa maana jamii yenye kuwa na imani tofauti tofauti za ki-DINI ni vigumu kuweza kuifanya "Ndiyo Mzee"!

  Kwa maana hiyo Mzee Makwaiya, either ni Muslim or Christian or Pagan or Budha or NIL, yeye anaamini (probably kwa nje tu - maana undani wake siujuwi) kuwa Siasa na DINI havichangamani! Inawezekana anashikiria msimamo huo kwa sababu ya imani yake binafsi au kwa kuona DINI moja inajiingiza kwenye siasa na hivyo inaweza ku-suppress ile "DINI yake" in "material terms" au probably anasimamia msimamo huo kwa sababu ya "falsafa ya Mwalimu Nyerere" - serikali haina DINI au ....

  Have a nice Weekend
   
 12. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haya ndio matatizo ya kuacha kufikiri kwa ubongo na kuanza kufikiri kwa moyo! Anachosema mtoa mada ni kweli kabisa. Mimi nampenda sana Makwaia na uwa sikosi makala zake hasa kwenye The Citizen. Tatizo la Mwakwaiya kama alivyo Khalid Mtwangi (The African) linapokuja swala la dini hasa kuhusu dhehebu Katoliki mioyo yao inachukua nafasi ya akili yao.

  These two guys hate Christianity with a passion! Ni dhahiri wanapozungumza au kuandika mambo kuhusu dini wanachukua mkondo wa kifadhahiina zaidi kuliko ukweli na ikifika hapo huwa sikubaliani nao. Kama ni swala la Palestina msimamo wao unachukua udini zaidi kuliko facts on the ground. Kama ni swala la dini kama vile waraka wa Askofu wa juzi juzi hata kabla hawajausoma wanaingiza udini. Askofu Kilaini amewauliza kina Makwaia na Kigunge wataje ni wapi waraka wa Maasikofu unalenga kuwagawanya wananchi hakuna hata mmoja aliyejibu hadi sasa! Ndio Makwaiya wa Kuhenga kama alivyo Khalid Mtwangi ni Mafadhahina (extremists) wa Kiislam hasa kwa mtazamo wao.
   
 13. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya bwana.
  Mimi sidhani kama yuko so unique.
   
 14. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Maada za makwaiya hazina tatizo lolote. Katika vipindi vyake vyote amekuwa anakaribisha watu mwenye mitazamo tofauti na pale anapozungumzia dini basi amekuwa anakaribisha wachangiaji wenye dini tofauti.
   
 15. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Naungana nawe kwa asilimia 100. Hawa watu wawili wana udini sana. Simfahamu vizuri Khalid Mtwangi, lakini Makwaia ni extremist hatari sana. Mie pia husoma makala zake kwenye The Citizen na hata Daily News na ninazifurahia sana kwani zina mantiki. Lakini kutokana na udini wake unaopitiliza mipaka (na hasa kwa kulidharau tamko la Wakatoliki) kuanzia sasa sitazisoma tena makala zake!
   
 16. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Kingunge yeye ni CHAMA KWANZA, mengine hataki kusikia. Waraka unataka watu wachague viongozi BORA. Yeye hataki kwani anataka watu wachague viongozi wa CCM.

  Makwaia ame-prove kuwa yeye ni DINI KWANZA, mengine hapana.

  Wanaopinga wamekuwa challenged waeleze kipengele wanachopinga wameshindwa.

  Vipi tamko la Mufti Issa Shaban Simba kuwa waislamu wasiichague CCM? Huyu kiongozi wa waislamu ametaja Chama kabisa, na halaumiwi na mtu.

  Note:
  Hivi watanzania wote wakipigia kura wanadini wenzao? Kikwete angefika Ikulu? Jibu ni hapana...
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  I hope hii ni changamoto kwa wale wote hawataki kuona baadhi ya wazalendo wakitaka mambo yaende sawa humu nchini. Cha msingi hao walioandaa huo waraka ambao pia ni wapiga kura wasiyumbishwe na mamluki. Mbona maaskofu walipotangaza kuwa kikwete ni chaguo la Mungu hatukuona wafurukutwa wakitokwa mapovu ya jazba?
   
 18. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huyu ni mtu hatari sana hapa tz. tumekuwa tukimjadili mara nyingi sana kwenye vikao vyetu vya siri, lakini tumeona hana lolote. ni sawa tu na wale watu wa redio kheri. wanatapatapa. wanavyofikiri wanajenga, ndivyo wanavyozidi kubomboa na kuchafua. wanachafua kisima kinachonywewa maji na wengi walio wema tu(yaani anachafua waislam wema walio wengi). kuna siku lawama nyingi zitamfunika, atakimbia nchi, kwasababu atatamani hata milima imfunike.
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tatizo liko wapi? Nasi tufungue moyo wako ili tujuwe kuwa masuwala ya dini ya wenzio ni mwiba kwako? Pingana kwa hoja lakini usimpinge mtu katika imani na mtizamo wake? Ni bora watu kama nyie mkaleta mada zenu wazi ili tujadili mitazamo yenu.
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hivyo hata yale ya Ufisadi huoni kuwa anapendelea upande mmoja na kwanini humwambii awalete na Mafisadi nao wajiteteee? Walioandika waraka walitaka wananchi wausikie na unachoona ndani ya Kipindi ni kile wananchi wanachoona juu ya kilicholetwa kwao. Kwanini hao Watayarishaji wasifanye kipindi maalum cha kuwaelimisha watu? Nafuikiri wametosheka na na hali ya kuusambaza tu.
   
Loading...