BadoNipo
Senior Member
- Jul 4, 2008
- 170
- 28
janal nilikuwa naangalia Channel ten kipindi cha ' Je Tutafika' ambacho kinaendeshwa na Mzee Makwaiya wa kuhenga. alikuwa ameenda nchi ambayo inaitwa Sumaliland, yaani sijawahi hata siku moja katika maisha yangu kusikia nchi inayoitwa kwa jina hilo zaidi ya kujua kuwa kuna nchi inayoitwa Somalia.
Kwa jinsi nilivyoona katika TV na maelezo toka kwa Raisi wa nchi hiyo na mazingira yake ianelekea nchi hiyo ina amani sana kwani hela zinabadilishwa tu hadharani, zinabebwa kwenye Mikokoteni, Yaani wabadilisha hela wako sokoni tena wameweka hela zao chini tu na watu kibao wanapita. Yaani ukifika muda wa kwenda kuswali wanaacha hela zao hapo hapo sokoni na wakirudi wanakuta vitu vyao kama walivyoviacha. kitu kingine kilichonifurahisha ni jinsi muda wa kuswali ukifika wanafunga hata Bank kuu ya nchi yao.
Nadhani lazima kuna wengine ambao pia hawajawahi kuisikia nchi hii.