Makwaiya wa kuhenga umetufunua wengine

BadoNipo

Senior Member
Jul 4, 2008
170
28
janal nilikuwa naangalia Channel ten kipindi cha ' Je Tutafika' ambacho kinaendeshwa na Mzee Makwaiya wa kuhenga. alikuwa ameenda nchi ambayo inaitwa Sumaliland, yaani sijawahi hata siku moja katika maisha yangu kusikia nchi inayoitwa kwa jina hilo zaidi ya kujua kuwa kuna nchi inayoitwa Somalia.

Kwa jinsi nilivyoona katika TV na maelezo toka kwa Raisi wa nchi hiyo na mazingira yake ianelekea nchi hiyo ina amani sana kwani hela zinabadilishwa tu hadharani, zinabebwa kwenye Mikokoteni, Yaani wabadilisha hela wako sokoni tena wameweka hela zao chini tu na watu kibao wanapita. Yaani ukifika muda wa kwenda kuswali wanaacha hela zao hapo hapo sokoni na wakirudi wanakuta vitu vyao kama walivyoviacha. kitu kingine kilichonifurahisha ni jinsi muda wa kuswali ukifika wanafunga hata Bank kuu ya nchi yao.

Nadhani lazima kuna wengine ambao pia hawajawahi kuisikia nchi hii.
 
Hii nchi inakuwa kama nchi ya "kufikirika" Maana ni sawa na hadithi ya Bustani ya Eden, enzi ya Adam na Eva. Hapa Bongoland hata wanawake ni washika mitutu.
 
wala sio nchi ya kufikirika, me nimeona kabisa kwenye TV jinsi wanavyoonyesha hiyo nchi.
yaani raha tu. ila sema haitambuliki na mataifa mbalimbali
 
Kama ni hivyo, mbona yale majambazi yalyovamia Ngorongoro yalikwa Wasomalia?

Mbona wanpora maduka huko kwao kila kukicha. Tuelezeni fresh
 
Hii sio Nchi bali ni ka-renegade fulani hivi kako ndani ya Somalia. Viukoo viko vingi ndani ya Somalia na vyote vinataka vitambulike kama Nchi.
 
Country History
The Republic of Somaliland known as the Somaliland Protectorate under the British rule from 1884 until June, 26th 1960 when Somaliland got its independence from Britain. On July 1st 1960 it joined the former Italian Somalia to form the Somali Republic. The union did not work according to the aspirations of the people, and the strain led to a civil war from 1980s onwards and eventually to the collapse of the Somali Republic. After the collapse of the Somali Republic, the people of Somaliland held a congress in which it was decided to withdraw from the Union with Somalia and to reinstate Somaliland's sovereignty.


Hiki ni kiukoo tu, wanalazimisha kukaita nchi, Internationally bado hakatambuliki.
 
Sehemu kubwa ya Somalia ilitawaliwa na Wataliano, sehemu ndogo ilitawaliwa na Waingereza.Hii sehemu iliyotawaliwa na Waingereza ndiyo inataka kujitenga na inaitwa Somaliland.

Hii ni nchi "de facto" lakini si "de jure". Ili declare independence kutoka Somalia mwaka 1991.
 
Back
Top Bottom