Makutano ya kiroho

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,782
Si kwa muktadha wa kimapenzi ama hisia za kufikirika, zile tamanifu zenye kuleta mvuto wa hisia za mahusiano ya kingono... Zile za kusema you stole my heart - umeiba moyo wangu....!

Haya ni makutano ya kiroho uwapo nje ya ufahamu wako, uwapo usingizini
Kipindi hiki roho husafiri huko na kule na katika safari hizo, roho hukutana na roho nyingine nyingi tu.... Roho mbaya nzuri nknk, za majini za wachawi za watu wa kawaida nk nk

Unapokuwa na ndoto mbaya sana na za kutisha basi roho yako inakuwa imekutana na roho za kutisha ama roho mbaya
Unapokuwa na ndoto nzuri basi huko kwenye kuvinjari jua roho yako imekutana na roho nzuri....

Utambuzi na kumbukumbu ya makutano ya roho katika ufahamu hutegemea na asilimia mia ufahamu wako umeweza kukamata yani kuna kuanzia asilia 0 mpaka 100, kadiri asilimia zinavyopungua ndio kumbukumbu ya ndoto husika huwa finyu na kuwa kama vague memories na vile jinsi asilimia zinavyozidi basi ufahamu na kumbukumbu ya ndoto husika huwa dhahiri zaidi na kuleta uhalisia zaidi

Ndoto za namna hii, hizi zenye kuleta uhalisia zaidi huwa karibu sawa kabisa na ndoto maono, zile ambazo huweza kusimulia kwa usahihi kabisa mwanzo wake mpaka mwisho wake... Tofauti yake ni moja tu!

Ndoto maono hizi huwa na tabia ya kujirudiarudia wakati hizo nyingine hazijirudiii japo huwa clear sana. Ulimwengu wa ndoto kwa asilimia kubwa sana huhusika na roho moja kwa moja, hivyo tunaposema kuna makutano ya kiroho jua kwamba si kingine bali ni kupitia ndotoni, japo kwa meditation pia inawezekana


Jr
 
Kwa muktadha wa MMU, kwa nini nikiota mwanamke ninaemfahamu huwa simpati? Wakati makutano ya kiroho ndotoni, tumekubaliana hadi tunda nimekula?
 
Kwa muktadha wa MMU, kwa nini nikiota mwanamke ninaemfahamu huwa simpati? Wakati makutano ya kiroho ndotoni, tumekubaliana hadi tunda nimekula?
Mmh pengine ni kwakuwa tayari mshakutana kindoto

Jr
 
Mshana kwanini ukiota unaona tukio linachukua hata saa takriban sita lkn ktk uhalisia yaweza kuwa ni dakika kumi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom