Makutano Show: Mahojiano Maalum na Mhe. January Makamba - Sept 29, 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makutano Show: Mahojiano Maalum na Mhe. January Makamba - Sept 29, 2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makutano Show, Sep 28, 2012.

 1. Makutano Show

  Makutano Show Verified User

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana-JF

  Wiki chache zilizopita nilipata udhuru sikuweza kuendesha kipindi na kukusanya maswali toka hapa JF, na sasa nimerejea.

  Katika Makutano Jumamosi hii natarajia kuwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa January Makamba tukijadili maisha yake ya kawaida na yale ya kisiasa. Ningependa kupata maswali toka kwenu ambayo atayajibu moja kwa moja katika kipindi.

  Kipindi kinaanza saa tisa mchana hadi kumi na mbili jioni kupitia Magic FM kupitia Magic FM 92.9 Dar, 93.3 Dodoma, 98.6 Arusha/Moshi,101.7Mwanza na pia kupitia ustream MakutanoShow on USTREAM: Makutano na Fina Mango. Radio

  Karibu
   
 2. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,437
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa kutushirikisha mjadala huu.

  Najua January kishashiriki mahojiano sehemu nyingi, mengine akiulizwa yatakuwa marudio. Nashauri mchambue maswali mnayoona yanafaa na yana mantiki ili yale muhimu yajibiwe.

  Nina maswali machache ambayo pia si lazima yaulizwe japo naamini ni muhimu:

  1. Kama Naibu Waziri, anakiongeleaje kitendo cha majirani zetu Kenya kuanza mkakati wa kuteketeza simu zilizo chini ya viwango? Wizara yake ina mkakati gani katika kutunusuru watanzania katika balaa hili? Ref: https://www.jamiiforums.com/kenyan-news/312456-kenyas-move-to-battle-counterfeit-mobile-handsets.html

  2. Kama Naibu Waziri, anaiongeleaje hatua ya majirani zetu Rwanda kuchukua hatua za kuziwajibisha kampuni za simu kwa huduma mbovu? Wao kama Wizara, wanaridhishwa na kinachoendelea Tanzania? Ref: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/330314-rwanda-fines-mtn-warns-tigo-over-poor-service.html

  3. Kabla ya kuwa Waziri alikuja na move moja nzuri ambayo kimsingi wengi tulimuunga mkono na hii ni kuhusu maisha ya watanzania na nyumba za kupanga; baada ya 'kutunukiwa' uwaziri, ndio tujue tumeliwa? Tutarajie nini katika hili toka kwake? Ref: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/217706-january-makamba-kiongozi-mwenye-uzalendo-licha-ya-kuwepo-ccm.html

  4. Tuweke siasa za vyama, chuki, udini n.k pembeni; angepewa nafasi ya kwa rais kwa miaka 5 tu, angefanya mambo makuu matatu yepi? Kivipi? Ana ndoto za urais 2015?

  5. Nje ya CCM, kuna mwanasiasa makini unayeweza walau kukiri wazi kuwa unamkubali?

  6. Najua nimeuliza mengi, nimalizie na hili: "Do you believe in Life after Death"?

  Asante Fina
   
 3. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,437
  Trophy Points: 280
  Naomba akiweza kujibu walau swali langu mojawapo, ajitahidi kutoa ufafanuzi, itamsaidia na itatusaidia wasikilizaji. Ni bora ajibu machache lakini kwa kina hasa.
   
 4. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Fina
  Nataka kujua hii Ustream inakuwa live wakati wa Makutano show tu ama iko live muda wote kwa vipindi vya Magic? Hili ni kwako sio January Makamba.

  Ngoja niongee na wana Bumbuli wanipe Data za jimboni kisha nitarejea na swali
   
 5. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  January mimi ningependa kujua Wanasiasa wengi huwekwa madarakani na mataifa ya magharibi kwa maslahi yao binafsi; wewe nuna maslahi na mataifa hayo kwa namna yoyote?

  Hatutaki kuuza nchi kwa tamaa za Wanasiasa.
   
 7. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,224
  Likes Received: 2,437
  Trophy Points: 280
  Fina,

  Hebu mwulize January;

  1. Wanasiasa wengi (yawezekana naye mmojawapo) huwa hawapendi kusikia mawazo yanayowapinga, wapo tayari hata kuua endapo aidha maslahi yao yanaguswa au 'mbaya wao' kaingia kwenye anga zao. Je, January anajitofautishaje na aina hii ya wanasiasa?

  2. Wizara yake inawasaidiaje vijana wanaoonyesha kujituma katika upande wa Teknolojia? Wana mpango wowote wa kufungia mitandao nchini katika kuzuia sauti za wanaowakosoa kama ambavyo watu wamekuwa wakionyesha kuhofia?

  2. Akifa, anadhani nini atajivunia mbele za Mungu wake? I mean, what will be his legacy?
   
 8. FULLUMBU

  FULLUMBU Senior Member

  #8
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 180
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Kama mwanasiasa kijana; Je, anajua kuwa kuna mafuriko ya degree ambayo yanaambatana na ukosefu wa ajira?

  Je, bomu litakalolipuka kutokana na hili anaishauri nini serikali (ambaye naye ni mmojawapo) kabla ya madhara makubwa kutokea?

  Mwisho ana kauli gani juu ya vijana 398 intern doctors waliosimamishwa ikiwa tuna upungufu wa madaktari?
   
 9. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Fina naomba niwakilishe nakuomba Makamba Jr. aulizwe haya:

  1. Akiwa kama mtoto wa mmoja wa viongozi waliokuwa maarufu sana (na bado maarufu kwa namna moja ama nyingine) katika medani ya Siasa; Je katika mafanikio ama matatizo ayakabiriayo katika ulimwengu wa siasa na utendaji kuna namna yoyote ambayo yeye (January) anaona kama huo uhusiano kama chanzo cha hayo (mafanikio/matatizo)?

  2. Kama mwezi mmoja alinukuliwa katika makala moja ya nje (The Observer) akiahidi kuwa mwezi ujao (ambao ndio huu wa 9) atazindua huduma mpya ya ujumbe wa simu chini ya jina ambalo kama sikosei ni ‘anti-corruption campaign’ ambayo italenga katika kusaidia kupunguza/tatua tatizo la rushwa katika jamii hasa mahospitalini… Je, tayari kishaizindua? Na kama kazindua hiyo huduma, inafanya vipi kazi na maeneo gani ya nchi ambayo hiyo kampeni imeyalenga?

  3. Kwa mtazamo wake January, nini kipimo cha maendeleo kwa Watanzania wa chini hasa vijijini? Kwa maneno mengine ni kitu gani ambacho akiona huyo Mtanzania kapata anaona sasa kakomboka na matumaini ya maendeleo kumnyemelea?
   
 10. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,824
  Trophy Points: 280
  1. Je, ni kwa nini ofisi ya maendeleo ya Bumbuli ipo dar na sio Bumbuli??

  2. Ni kwanini January unatumia mfumo wa mitandao ikiwepo simu, twitter na facebook katika kuwasiliana na wapiga kura wako juu ya matatizo ya Bumbuli ili hali unajua teknolojia ipo chini sana hasa kwa maeneo ya vijijini kama Bumbuli?
  Eg: Mpiga kura wako hana hata umeme atawezaje kuwasiliana na wewe unayetegemea Twitter kujua matatizo yake?
  Je, huyu mpiga kura wako alikupigia kura kwa kutumia Twitter/facebook or simu?
   
 11. Ansah Miles

  Ansah Miles JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Mh Makamba atueleze kuhusu Kamati yake ya nishati na madini iliyovunjwa kwa tuhuma za rushwa, (tuhuma hizo zilikuwepo katika kipindi cha uongozi wake), alifahamu nini kuhusu tatizo hili la rushwa ndani ya Kamati yake?
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Huyu mheshimiwa mimi niliku namtafuta siku nyingi sana,bora umemleta da fina.Mimi bila kuuma maneno kuna haka kakitu haka:

  Lisa M Rockefeller The So Called Ernesto Sheka's real name is January Makamba, is the one apparently threatening me. Let's see if he will ever set his feet in the American soil, this is nothing but an act of terrorism, I agree now, Kikwete is a Joke to hire people like these
  swali langu kwako januari,je unamfahamu huyu binti?kama ndio nahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu hiyo mistari yake ya maneno hapo juu,je ulikua na uhusiano upi na yeye na nini kilitokea mpaka kukawa na sintofahamu hiyo baina yenu wewe ukielezwa kumtishia maisha?maana siku moja unaweza kuwa rais wetu wewe,kwani wapi pameandikwa bumbuli haiwezi kutoa rais!sasa huu ni wakati wako mzuri wa kujitakasa na hii kitu ikiwemo kutueleza labda una mpango wowote wa kutembelea marekani hivi karibuni?

  mengine ni kutilia msisitizo maswali ya msingi sana ya daud mchambuzi hapo juu.
   
 13. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  swali kwako fina,mbona kipindi chako kinahoji wabunge wa aina fulani fulani tu mfano wafanya biashara,wanaoutamani urais n.k. mbona mbunge wangu azzan zungu ambae eneo lake bunge ni pamoja na hapo magic unapopatumia kufanyia mahojiano hujamualika hata mara moja?sina uhakika na kama hata meya wangu jerry umeshamualika hapo japo najua yeye nae ni wa aina ya watu unaowaalika alika hapo.

  Nahitaji ufafanuzi zaidi kwanini zungu hujamualika?
   
 14. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  mh january, nimepitia matokeo ya kidato cha nne katika jimbo lako nikakuta :- mwaka 2010 kati ya watahiniwa 1200 jimboni bumbuli ni wanafunzi 60 pekee waliofaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ikiwa ni sawa na 5%. Mwaka 2011(mwaka 1 baada ya wewe mheshimiwa kuwa mbunge)hali ikawa mbaya zaidi katika matokeo ya kidato cha nne ambapo kati ya watahiniwa 1327 ;-

  waliopata div 1= hakuna, div two=4, div three 39 tu. Jumla div 1-3= 3.2% ! na wanafunzi waliosalia 1274 walipata daraja la 4 na zero. Pia jimbo la bumbuli ni mojawapo ya wahanga wa tatizo la MIMBA mashuleni na utoro sugu.

  SWALI:
  1: je mh makamba nini chanzo cha matokeo ya kidato cha nne jimboni kwako kuzidi kuwa mabaya baada ya wewe kuwa mbunge?
  2: mh rais Jakaya kikwete aliwahi kunukuliwa akisema " wasichana wa sekondari na primary kupata ujauzito mashuleni NI KIHEREHERE CHAO! Je nini maoni yako juu ya kauli hii?
  3: ukiwa kama naibu waziri wa sayansi ,je ni shule ngapi jimboni kwako zina maabara za kisasa za kufundishia masomo ya sayansi?
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwanini anaitwa January na isiwe December?
   
 16. S

  Selemani JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Naomba ailezee hii makala aliyohojiwa inayohusu masuala ya gesi. Tanzanian gas: blessing or curse?


   
 17. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,098
  Likes Received: 11,248
  Trophy Points: 280
  1. Ningependa kujua wizara yake inawasaidiaje wanafunzi wenye vipaji vya uvumbuzi hasa katika fani ya ICT?

  2. Kwanin anaishi Dar na sio Bumbuli? Na kama kisingizio ni uwaziri, nin mawazo yake kwenye swala ya kutenganisha nyadhifa ya uwaziri na ubunge?

  3. Nin maoni yake kwenye katiba mpya?
   
 18. mr gentleman

  mr gentleman JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 2,615
  Likes Received: 2,730
  Trophy Points: 280
  January:kulikuwa na kutoelewana kwa hali ya juu kati yako wewe na Mh Joseph Mbilinyi 'Sugu' hapo nyuma,haswa akikuhusisha na kushiriki kumpora mradi wake wa Malaria ukishirikiana na kina Ruge pindi upo ikulu..swali-vipi mahusiano yenu kwa sasa???
   
 19. Transkei

  Transkei Member

  #19
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mr january kwanza nikupongeze kwa kuonyesha uwezo mkubwa sana katika ulingo wa siasa!!swali langu;shirika la maendeleo la bumbuli litaanza kazi lini? na linatarajia kuajiri vijana wangapi ili kupunguza tatizo la ajira nchini?
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  1: wewe kama naibu waziri: kuna swala la watu kutapeliwa kupitia mobile banking, je mmekwishapokea malalamiko ya namna hii? kuna mpango gani wa kuweka sheria zitakazo mlinda mteja (naomba maelezo ya kina)? na ni hatua gani mlizozichukua mpaka sasa kukabiliana na wizi wa namna hii (naomba mifano halisi na maelezo ya kina) kwasababu hali inazidi kuwa mbaya kila siku
   
Loading...