Makusanyo ya TRA mwezi June ni Bilioni 500, kulikoni?!

ndio tatizo la mhemko wa kisiasa, akifuata wataalamu wa IT rwanda povu ,haya sasa TV yako mwenyewe umeiangalia na taarifa umeisikia nusu nusu!
 
wao ndio wenye mamlaka ya kukusanya kodi ulitaka niwaamini akina nani?? au ulitaka makusanyo yawe kidogo ili upate cha kupost?? basi wanekusanya billion 10 , haya shangilia!!
nimegundua kuna watu hawataki mapato yawe mengi
 
Inawezekana na isiwezekane! Kwa style ya sasa hawawezi kuonyesha kuwa bandari imeshuka makusanyo kwa watumiaji wake kuhama.
Bandari kwa mwaka hawafikishi tr 1, na waziri kawapa target ya kufikisha tr 1 mwaka huu, kwa hiyo bil 500 kwa bandari pekee yake kwa mwezi ni uwongo hata bil 200 kwa nwezi haijawahi fika. Ninavyi jua hiyo bil 500 ni kwa mwaka 2016 unao ishia june 2016.
 
Hayo ni makusanyo ya bandarini tu sio ya jumla. Wastani wa mapato bandarini umepanda kutoka bilioni 200 hadi 300 kwa mwezi hadi kufikia bilioni 400 hadi 500 kwa mwezi.
Bandari kwa mwaka hawafikishi tr 1, na waziri kawapa target ya kufikisha tr 1 mwaka huu, kwa hiyo bil 500 kwa bandari pekee yake ni uwongo hata bil 200 haijawahi fika
 
Wametaja vizuri tu. Wamevuka lengo la mwaka 2015/16 kwa asilimia mia moja pointi .......Halafu ukafuata ufafanuzi wa ongezeko la mapato bandarini ingawa mizigo imepungua. Tunawapongeza TRA.
Hayo ni makusanyo ya mwaka mzima 2015/2016 na sio ya mwezi june pekee yake ya bandari . Mwaka ujao 2016/2017 wanatakiwa kukusanya tr 1
 
Habari wakuu,

Nilikua naangalia taarifa ya habari ITV usiku huu na msemaji wa TRA ni kama nimemsikia kwamba makusanyo waliokusanya mwezi June ni billion 500.

Kulikoni makusanyo ya kodi kushuka hivi mwezi June.

Au kwa mliosikia vizuri au data zaidi ya kiasi halisi kilichosemwa mnaweza mkatoa data za uhalisia kwa maana naona kama billion 500 ni kama makusanyo yameshuka by a half.
Acha ujinga ,hautakusaidia chochote maishani
 
Huu uwongo wa wazi mm wala siamini Bandari empty vile pato limekuwa hivo kulikoni
 
Nyie mkusanye bilion 500 au 1000 mi ninachotaka kuona barabara za mkoa wa Katavi,na mikia jiran zinatengenezwa maana utafikiri huku ni njia yakwenda kuzimu.
 
Wananchi Tutimize wajibu wetu, tulipe kodi kwa bidii, serikali hii haitatuangusha. In JPM we trust
 
Habari wakuu,

Nilikua naangalia taarifa ya habari ITV usiku huu na msemaji wa TRA ni kama nimemsikia kwamba makusanyo waliokusanya mwezi June ni billion 500.

Kulikoni makusanyo ya kodi kushuka hivi mwezi June.

Au kwa mliosikia vizuri au data zaidi ya kiasi halisi kilichosemwa mnaweza mkatoa data za uhalisia kwa maana naona kama billion 500 ni kama makusanyo yameshuka by a half.

Mkuu ulikuwa umepata Kitwanga ama. Alisema haya

Akizungumza katika mkutano na wanahabari jana, Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata alisema upungufu huo wa mizigo bandarini umezikumba pia bandari za Beira, Msumbiji, Mombasa, Kenya na kwingineko na kusababisha mapato kupungua.

“Lakini sisi pamoja na upungufu wa mizigo bandarini makusanyo yanazidi kuongezeka kutokana na kuzibwa mianya ya kukwepa kodi, hivyo napenda kuwapongeza wafanyakazi wote wa mamlaka na kusema kwa sasa hakuna mtu anayeweza kukwepa kodi na wale waliozoea wakae katika njia kuu,” alisema Kidata.

Kidata alisema wananchi wanatakiwa kuwaunga mkono kwani sasa kodi inaonekana katika kufanya shughuli za serikali kama kuboresha miundombinu pamoja na kutoa elimu bure.

Kidata alisema katika kipindi cha Juni mwaka huu, TRA imekusanya Sh trilioni 1.4 sawa na asilimia 107.83 ya lengo la kukuzanya Sh trilioni 1.3 ambapo makusanyo ya mwaka wa fedha 2015/16 ni sawa na ongezeko la asilimia 23.70 la makusanyo ya mwaka 2014/15.


Akizungumzia mashine za kielektroniki za EFDs, Kidata alisema walipoanza utoaji mashine hizo zilikuwa 5,703 na mpaka sasa mashine 1,700 zimegawiwa kwa watumiaji na wataanza kupita duka hadi duka kuhakiki matumizi ya mashine hizo.

Kamishna wa mapato ya ndani, Elijah Mwandumbya, alisema mwaka huu wa fedha wamejipanga kuhakikisha wanaondoa changamoto kwa mtu mmoja kuwa na TIN zaidi ya moja hivyo watafanya uhakiki
 
Haya na wale waliopewa pesa ya Escrow wamelipa kodi kiasi gani? Vijana wa Lumumba leteni majibu
 
Makusanyo kwa wazalendo walipakodi watiifu, nongependa tuwe tunaita hivi maana TRA wao hawakusanyi pesa ila data tu.
 
Back
Top Bottom