Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Wakuu,

Waziri wa Fedha, Dr Mwigulu Nchemba anazungumza na waandishi wa habari muda huu kuhusu miradi ya Serikali pamoja na Tozo za miamala ya simu pamoja na mafuta. Kuwa nami kukujuza yanayojiri

==========

Mwigulu Nchemba-Waziri wa Fedha na Mipango
=▷
Itakuwa aibu mtanzania yoyote alie hai, kuna mradi umekwama kwasababu tu viongozi waanzilishi labda hawapo duniani au hawapo kwenye madaraka, itakuwa aibu ya kila mtanzania alie hai leo.

=▷ Watanzania wameendelea kufanya shughuli za miamala, namba zinaendelea kucheza mulemule kama zilivyokuwa kabla. Kwa mfano kabla hatujaanza kulikuwa na miamala milioni kumi/ kumi na moja na sasa inacheza humo humo kwenye milioni 10/ tisa kama ilivyokuwa mwanzo.

=▷ Katika wiki nne ambazo tumefanya hii shughuli wakati tukisubiri marekebisho haya tunayopanga kuyafanya, kwasababu hii ilikuwa sheria ya bunge iliendelea kutekelezwa

=▷ Lakini katika kipindi hicho ambapo shughuli hii ilianza hapo tarehe 15 mwezi wa saba mpaka hivi tunavyoongea leo ukioanisha na mapendekezo tuliyokuwa tumeyapangilia, tayari tumeshakusanya 48,489,225,670(Bilioni 48.4)

=▷
Katika hizo, tayari tumeshapeleka zaidi ya bilioni 22 kwenye vituo vya afya kwa maeneo ambayo hayana vituo vya afya kabisa ambapo ukipiga hesabu kwa haraka haraka ni zaidi ya vituo 90 vya afya

=▷ Tumeshapeleka nyingine zaidi ya bilioni 15 iende kwenye eneo hilohilo ambayo itafanya zaidi ya vituo 150 sasa kwenye maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na kituo

=▷ Zaidi ya bilioni saba zingine kwaajili ya madarasa kwa ajili ya kujiandaa kupokea watoto wa form one, waziri mwenye sekta atakuja kusema jinsi alivyopangilia.

=▷ Kipindi cha mwezi mmoja Serikali imekusanya Sh 24 bilioni, kutokana na tozo za mafuta ambazo ni mahususi kwa ajili ya kujenga barabara.

=▷ Kama serikali tutaendelea kupokea na kuyafanyia kazi maoni yote, na haijalishi mtoa maoni yuko Serikalini au la, kwetu maoni ni maoni muhimu maoni hao yanalenga kujenga nchi yetu



Mwigulu.jpg


=▷ Tuliokuwepo hapa ni dhamana tu, la msingi hata yote tunayofanya ni yetu na ni njia ya kupangalia namna ya kuyafanya, ndio maana ndio maana kiongozi wetu mkuu alisikia sauti hizo na akaelekeza kwamba haya mambo yafanyike.

=▷ Imechukua muda, ni utaratibu tu za kiutekelezaji wa maelekezo na sababu nitazielezea mbele, huwa tunahusisha na makundi mengine ambayo yako nje yetu sisi.

=▷ Mheshimiwa Rais akishakuwa na malengo mazuri namna hii na kule vijijini kwenye maeneo yetu, yakishakuwa mazuri hivi tusigombane kuhusu malengo wala khusu utaratibu. Tushauriane tu namna ya kufanya vizuri kwa ufanisi mzuri zaidi.

=▷ Tunapata ufanisi zaidi tukifanya hivyo, watanzania wanaoishi vijijini na wanaoishi mjini wote wajione wako Tanzania.

=▷ Hii ndio itakayotuondlea pengo la walionacho na wasianacho, zamani ilikuwa inatokea wanafanya mtihani, kijiji kizima hatokei hata mtoto mmoja aliefaulu kwahiyo kuboresha hii miundombine, afya watanzania tukibebe kwa yowe kabisa kwa sababu ni chetu. Niwaombe watanzania kuendela kuwa watulivu na wavumilivu.

Pia, soma=▷ Dkt. Ndugulile: Rais Samia ameagiza tulitazame upya suala la tozo, wananchi kuweni na subira tutakuja na mapitio
 
Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba amesema katika kipindi cha wiki nne Serikali imekusanya Sh 48.4 bilioni kutokana na tozo za miamala ya simu, na zaidi ya Sh22 bilioni zimepelekwa katika vituo vya afya zaidi ya vituo 90.

Pia ameendelea kusema, katika kipindi cha mwezi mmoja, Serikali imekusanya Sh 24 bilioni, kutokana na tozo za mafuta ambazo ni mahususi kwa ajili ya kujenga barabara.
View attachment 1899468
 
Back
Top Bottom