Serikali tayari imetoa maelekezo kwa Mmlaka za Serikali za Mitaa kuwa kuanzia mwaka wa fedha ujayo itabidi Mamlaka zenyewe zikusanye kodi zake badala ya Mawakala. Binafsi mimi ninatofautiana na Serikali kuwa Mwaka wa fedha ujao kama Serikali watumia njia hii hata robo ya mapato hayatafikiwa. Nitoe mfano hapa Mwanza, Jiji wanakusanya mapato yanayotokana na maegesho na kuna vituo zaidi mia mbii za makusanyo. Je watumishi wapatao mia mbili watatoka wapi kwa ajili ya kazi hii huku Serikali tayari imezuia ajira?. Pili nitoe mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, hawa wana mialo ya kama kilomita 70 na vituo vipatazo mia moja. Je wako watumishi watakaotosha kusimamia ukusanyaji wa mappato haya?. Nilikuwa nadhani kuwa Serikali ikishirikiana na Halmashauri wapitie vyanzo vyote vya mapato na wapate kiasi halisi ya kila chanzo mfano maegesho labda 50m kwa mwezi basi kutokana taarifa hiyo wawaelekeze Halmashauri kubinafsisha kwa hizo 50m. Mamlaka za Serikali za Mitaa wasiwe waoga wawaeleze Serikali ukweli juu ya athari hii.