Makundi yaitafuna CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makundi yaitafuna CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sijui nini, Oct 21, 2010.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  ZIKIWA zimesalia siku 13 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Oktoba 31, makundi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), yanaonekana kukisumbua chama hicho kiasi cha wanachama kutishiwa kutimuliwa. Hali hiyo ilidhihirika jana wakati Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, alipotumia maandiko matakatifu ya Biblia kutoa onyo kwa viongozi na wanachama wa chama hicho watakaoendeleza makundi yaliyozaliwa baada ya kura za maoni.
  Akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Wilaya ya Arusha, Makamba alisisitiza kwamba chama hakina nafasi tena kwa wakiuka kanuni na sheria za chama hicho na kwamba ni vema kuwa na wanachama wachache waaminifu kuliko kuwa na kundi lisilokuwa na tija.
  Alisema baada ya kura za maoni kwisha na chama kupata wawakilishi wake wa ubunge na udiwani nchini hivyo, wana CCM wanawajibika kuwa kitu kimoja kwa kuhakikisha aliyeshinda kura hizo anaendelea kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo na kuacha dhana ya kumpigia kampeni mgombea wa CCM mchana huku usiku wakimpigia wapinzani.
  “Sisi wasambaa ukigombana na mkeo huendi mbele unarudi nyuma, kwani kuna sehemu akikushika utakaa chini, hao walioshindwa walishikwa pabaya, sasa wakubali matokeo kama mlikuwa mkicheza sasa basi! Tutawafukuza bila kujali ni kiongozi au mwanachama,” alionya Makamba.
  Alisisitiza siasa ni shughuli ya makundi kama ilivyo shughuli zingine kama mpira na ngoma, lakini inashangaza kuona viongozi wa chama hicho wakishiriki vitendo viovu vya kukihujumu chama hata baada ya kura za maoni kumalizika na kuwashabikia wagombea wa upinzani.
  Aliwaita viongozi hao akiwemo Mwenyekiti wa CCM wilaya (Jubilate Kileo), Katibu Itikadi na Uenezi wa wilaya, Katibu wa Uchumi na Fedha, Mwenyekiti UWT na Katibu wake na kudai kuwa wote walikuwa na upande wao binafsi, lakini wakati huu ni kipindi cha kuuungana ili kuwabana wapinzani.


  CHANZO>>


  MOTO UNAWAKAAAA...!!:A S 41::A S 41:
   
 2. M

  Mikomangwa Senior Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safari hii Makamba ajaribu kusoma na aya za Kihindu labda wana CCM watamwelewa vizuri zaidi!
   
Loading...