Makundi ya WhatsApp ya makazini yafutwe, tuheshimuni weekend zetu na muda wa mapumziko

spleen

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
3,225
4,662
Haiwezekani Jumamosi, Jumapili, Sikukuu usiku wa manane, kiongozi kwa utashi wake eti anatoa maagizo kupitia group la WhatsApp.

Jamani tuheshimuni weekend zetu na muda wa mapumziko, kazi zilikuwepo na zikifanyika tu hata kabla ya WhatsApp.

Inaboa sana unakutana na kiongozi mtaka sifa kila muda kutoa maagizo tu anavyojisikia, kama haujaona meseji ugomvi unaanzia hapo, daaaah hivi hii imekaaje wadau tujadili hizi mambo kwa upana, kabla hatujaanza kutoleana nishai huko mbeleni.
 
Si uzime Data Mkuu ukishatoka Kazini?
 
Group la whatsapp la kupeana maagizo ya kazi?? Labda madaktari na maaskari!

Kiongozi sahihi, atawasiliana nawe personally, na atakutaka radhi kwa kuharibu wkend yako. Akihitaji ufanye jambo.

Everyday is Saturday................................ :cool:
Mkuu mmewaza vyema
Kuna siku nlipigiwa simu na wenzangu tu kua kesho tunahitajika sehemu.
Ikumbukwe tupo mbali
Taarifa imenifikia saa4 usiku
Wao walipost kwenye group saa11
Et ndio imeisha
 
Aahahahahahaa majibu yenu tuu.

Kuna wakati nami yakiniboa hasa kuhusu kufatiliana maisha nje ya kazi.

Huwa nakuwa na msimu, kuna muda zipo kwenye group la ofisini aidha nazima data au nakuwa na kitochi au nawaambia kuna jambo binafsi nafanya linahitaji utulivu wangu. Atayenihitaji siriasily kiofisi nje ya muda wa kazi simu yangu iko hewani.

Haya mambo saa tatu usiku mtu anatuma ujumbe wasap kesho tuwahi saa moja tuwe ofisini na tubas in black colour, huwa nawafurahisha. Wakiniuliza najibu kirahisi tuu sijapata taarifa, hakuna aliyenipigia simu naona ujumbe haukuwa wa muhimu kwangu maana huwa sizimi simu.

Kasinde Matata.
 
Kuwa na namba 2 za WhatsApp, moja ya kazini nyingine tumia kwa mambo yako mengine.
Ukitoka kazini zima hiyo WhatsApp ya kazini... unaeza eka WhatsApp mods zinazokua na features za Do not Disturb then mambo yanajipa unawasha ukishaingiza kazini
 
Back
Top Bottom