Makundi ya Wazayuni yatishia kumuua mrithi mtarajiwa wa Netanyahu, Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,877
Makundi ya Wazayuni yatishia kumuua mrithi mtarajiwa wa Netanyahu, Israel

Jun 06, 2021 07:27 UTC

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimetangaza kuwa, waziri mkuu mtarajiwa wa utawala huo Naftali Bennett anayetoka muungano wa wapinzanii wa waziri mkuu wa ssaa Benjamin Netanyahu ametishiwa kuuawa.

Televisheni ya Israel imetangaza kuwa, vyombo vya usalama vya utawala huo vimesema, vimepokea ripoti ya vitisho vya kuuliwa kiongozi wa chama cha New Right, Naftali Bennett, na kwamba vinafuatilia ipasavyo suala hilo.

Awali Jenerali Nadav Argaman mkuu wa Shirika la Usalama wa Ndani la Israel (Shin Bet) alikuwa tayari ametahadharisha kuhusu mpango wa kuuawa viongozi wa kisiasa wa utawala huo kufuatia kuungana vyama vya mrengo wa kulia, vile vya mrengo wa kati na vya kushoto kwa ajilii ya kumuondoa madarakani Benjamin Netanyahu na kuunda serikali mpya.

Itakumbuka pia kwamba wafuasi wa Benjamin Netanyahu hivi majuzi walikusanyika mbele ya ofisi ya Yair Lapid, kiongozi wa chama cha upinzani cha Yesh Atid wakipinga jaribio lolote la kundwa serikali mpya.

Jumatano iliyopita Yair Lapid alimtaarifu Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Reuven Rivlin kwamba yuko tayari kuunda serikali mpya baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda baraza jipya la mawaziri.
 
Ni kosa kubwa arabs kushare utawala katika Taifa la kiyahudi.. wapuuzi hao kisa tu kumtoa madarakani Netanyahu wameona walinajisi Taifa kujaza uislam serikalini... Yaliyomkuta Rabin kwa kuwapa Arabs Gaza yanaweza mtokea Kwa kina Bennet hilo Taifa limeooteza damu ili kuwaondosha wavamizi Arabs waliotokea Egypt na nchi za kiarabu jirani.. and then wanaleta Ushora ndago kuungana na Waarabu
 
Unateseka sana kijana......ni kama kuzuia mafuriko kwa mkono tu maana sahivi couple za arab-jews zinapamba moto

Back
Top Bottom