mabuba
Senior Member
- Dec 5, 2006
- 133
- 90
Kuna kundi la watu linalomsifia Mh. JPM. Kundi hili ni kundi kubwa lina jumuisha watu wa rika tofauti, uwezo wa kiuchumi tofauti na hata mienendo tofauti. Kundi hili limegawanyika katika makundi yafuatayo:
1. Wale ambao waliona kuwa kipindi cha nyuma, utumishi wa umma ulikuwa uko fungate, ulitenda yale yasiyo ya kiutumishi wa umma. Wanaona ujio wa JPM umekuja kuwajibisha watendaji wabovu ambao waliishi maisha ya utwana. Kundi hili ni kubwa sana,
2. Amba wanasifu utendaji wa JPM sio kwa moyo wa dhati, wao wanasifu kwasababu JPM anafichua maovu ya mahasimu wao kisiasa. Hili kundi ni lile ambalo lilikinzana na wafuasi wa mafisadi.
3. Ambao ni makasuku, wazandiki, mapashikuna na walaghai. Hawa ni ambao walizoea kufanya kazi kimazoea, wategemea posho za vikao, semina, nk. Hawa wanamsifu machoni lakini kiroho hawapo naye.
4. Wapo ambao wao, wanaona mabadiliko katika uongozi, hawa hawana maslahi yoyote, wengi ni nchi za nje na wachache ndani.
5. Ambao hawajui kwanini wanamsifia. Wanaangalia nani kasifia nao wanasifu.
6. Wale walioumizwa na mfumo wa utoukweli, mfumo wa utowajibikaji. Hawa waliumizwa kutokana na kuisimamia kweli
Mwanamtaa.
Mabuba FKM