Makundi ya watu ni kutokana na kigezo cha muda na pesa

Kumhama

Member
Oct 26, 2012
19
2
Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda.. Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, Why?

Because ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoma Dar kwenda Moshi ni dk45 tu kwa ndege but kwa gari ni takribani masaa 7-8).

*Linapokuja suala la MUDA NA PESA, duniani kuna makundi manne ya watu;

1. Wapo wenye muda wa kutosha bt hawana pesa mfano watu wasio na kazi maalum au wa kijiweni(ukimwambia akusindikize mahali yuko tayari muda wowote)

2. Wapo wenye pesa lakini hawana muda. Unaweza kumualika katika harusi akaacha kuja lakini akakuchangia hela ya maana tu, hili ni kundi la madirector na mameneja wa vitengo muhimu katika makampuni (ndio hawa JPM amewataka walipwe sio zaidi ya 15mil kwa sasa)

3. Wapo wasio na PESA wala MUDA. Takwimu zinaonyesha kuwa hawa ni 95% ya watu wote ulimwenguni. Hili ni kundi la wafanyakazi na vibarua (unaweza ukamualika katika shughuli yako na akakosa nafasi lakini pia hana hela ya kukuchangia). Yaani mtu yuko busy 24/7 but ukimwomba hata elfu 50,000/= hana.. Why?

Mtu huyo unakuta ana mshahara mdogo halafu ana mikopo mingi mf kakopa nyumba, gari, mtaji wa biashara ambapo kutokana na kukosa usimamizi makini napo hakuna pesa, hivyo neno MAREJESHO ndio msamiati mkuu kwao.

4. Wapo watu wana PESA na MUDA wa kutosha. Ndio matajiri au watu waliofanikiwa sana. Why?

Hawa wameandaa mfumo ambao hata wasipokuwepo pesa inaingia (mf Mengi au Bakhresa akienda likizo hata miezi mitatu bado akirudi biashara zinaendelea vizuri).

Hapa unakuta yeye ndio CEO na pengine asubuhi yuko anawaandaa na anawapeleka wanae shule huku mimi na wewe ndio tunakomaa na mafoleni tukielekea kufanya kazi za kujenga ndoto za hao watu kwa masaa mengi na tunalipwa kidogo.

Wapo watu wanasema, usipoitengeneza FUTURE yako mtu mwingine atakutengenezea kadiri atakavyoona inakufaa
AU
Usipojenga ndoto zako kuna mtu atakuchukua (kukuajiri) ukajenge ndoto zake!

JE, WEWE UPO KUNDI GANI? WASWAHILI HUSEMA, USIPOJIPANGA UTAPANGWA..

Amka na Tafakari sana. Siku zote ni wazo kijani ndiyo jibu kubwa...

Siku njema kwenu wote.
 
Back
Top Bottom