Makundi ya urais 2015 yaitafuna UVCCM

regam

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
269
51
Mussa Juma, Arusha.

MAKUNDI ya vigogo wanaowania urais mwaka 2015, ndani ya CCM yamezidi kuugawa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), baada ya Kaimu Mwenyekiti wake, Beno Malisa na viongozi wengine wa kitaifa kujikuta wakikwama kufungua matawi ya umoja huo mjini hapa jana.

Malisa aliyekuwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Jamal Ally, mbunge wa vijana CCM, Catherine Magige pamoja na vigogo kadhaa wa umoja huo, jana walikuwa wazindue matawi 16 ya vijana katika Manispaa ya Arusha, lakini uongozi wa UVCCM wilaya ukagoma.

Viongozi wa UVCCM Wilaya ya Arusha, wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Godfrey Mwalusamba walipinga ujio wa ghafla wa vigogo hao na kufanya kazi ya kuzindua matawi huku uongozi wa umoja huo wilaya ukiwa hauna taarifa.

Mwalusamba pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya hiyo, walitoa uamuzi huo katika kikao kilichozua malumbano ambacho kilifanyika juzi, ofisi ya UVCCM Mkoa.

Jana, Mwalusamba alithibitisha kupinga kazi ya ufunguaji matawi hayo ya UVCCM kwa maelezo kwamba, walikuwa hawana taarifa za kazi hiyo.

"Wanasema mimi natumiwa na kundi moja la wanaogombea urais, hapana labda wao ndio wanatumiwa, itakuwaje wafike hadi wilayani kwangu na kufanya kazi kwenye kata, bila taarifa hata hizo kata hawana taarifa,"alisema Mwalusamba.Kazi ya uzinduzi wa matawi hayo, ulikuwa umepangwa kufanyika katika Kata za Sokone One,Sombetini, Kaloleni, Sekei na Elerai, lakini haikufanyika licha ya kuwa tayari mabango na baadhi ya vijana walikuwa wamejiandaa.

Kauli ya UVCCM Mkoa Arusha
Mjumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha, Ally Benanga ambaye ni mmoja wa waliokuwa waandalizi wa kazi ya ufunguaji wa matawi, alituhumu baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Arusha kutumiwa kukihujumu chama.

"Hawa ni wasaliti, tulikuwa tayari tumewaandaa vijana, tumetengeneza mabango sasa wamegomea, tunajua wanatumiwa na kundi moja la urais na Chadema kudhoofisha CCM Arusha,"alisema Benanga.

Hata hivyo, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Abdul Mpokwa alipotakiwa kuelezea mtafaruku huo, licha ya kukiri kuahirisha zoezi hilo, lakini alikataa kufafanua zaidi chanzo chake.

"Ni kweli leo (jana) tulikuwa na kazi hiyo ila tumeahirisha na tutaifanya siku nyingine, "alisema Mpokwa.

Katibu huyo, hata hivyo, alikataa kuelezea ni hatua zipi watachukuliwa viongozi wa UVCCM Wilaya ya Arusha ambao waligomea zoezi hilo kwa maelezo kuwa walikuwa hawana taarifa.

"Naomba uwasiliane na Katibu wa Mkoa Mary Chatanda yeye ndiye msemaji wetu katika chama,"alisema Mpokwa.

Malisa akana kutumiwa na makundi
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jioni, Malisa alikiri kuahirishwa jana kufanyika kazi ya uzinduzi wa matawi hayo kwa kile kilichoelezwa siyo siku nzuri.

Hata hivyo, alisema taarifa alizopewa na mkoa ni kuwa kazi hiyo itafanyika leo huku akikanusha kutumiwa na makundi. "Sidhani hapa kuna makundi, ufunguzi wa matawi ni kuimarisha chama na madai kuwa wilaya haina taarifa sisi haituhusu kwani uongozi wa Taifa unawasiliana na Mkoa,"alisema Malisa.

Tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu, CCM Mkoa wa Arusha kimekuwa katika vurugu kubwa za makundi ambayo yanadaiwa kusababisha kuangushwa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Arusha, Dk. Batilda Burian.
Source: Mwananchi 10/10/2011

“Naomba uwasiliane na Katibu wa Mkoa Mary Chatanda yeye ndiye msemaji wetu katika chama,”alisema Mpokwa.

Malisa akana kutumiwa na makundi
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jioni, Malisa alikiri kuahirishwa jana kufanyika kazi ya uzinduzi wa matawi hayo kwa kile kilichoelezwa siyo siku nzuri.

Hata hivyo, alisema taarifa alizopewa na mkoa ni kuwa kazi hiyo itafanyika leo huku akikanusha kutumiwa na makundi. "Sidhani hapa kuna makundi, ufunguzi wa matawi ni kuimarisha chama na madai kuwa wilaya haina taarifa sisi haituhusu kwani uongozi wa Taifa unawasiliana na Mkoa,"alisema Malisa.

Tangu kumalizika Uchaguzi Mkuu, CCM Mkoa wa Arusha kimekuwa katika vurugu kubwa za makundi ambayo yanadaiwa kusababisha kuangushwa kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Arusha, Dk. Batilda Burian.
Source: Mwananchi 10/10/2011

Hawa wajinga kila kitu kikiwashinda wanasingizia chadema.
 
sasa ivi chadema kimegeuka kuwa chama tawala,zamani vya vyama vya upinzani vilipalanganyika kutokana na ccm kuwagawa kwa pesa.sasa ni zamu yao kugawa kwa chadema kutokana na hoja nzito zinazo wafanya kuweweseka.
 
heeeeeeeeeeeeee heeeeeeeeeeeeeeeeeeee adui muombe njaaa atanyoosha mikono hata kama ni shuja
 
Ni mambo ambayo hayaeleweki hata kidogo na si kazi ngumu kusoma dhamira mbaya ya mpango huu. Mahitaji ya kufungua matawi yalitakiwa kutoka ngazi za chini (wilayani) na wale wa juu wangeitwa tu ili kulipa tukio hili umuhimu au limelight ya kitaifa. Sasa leo mtu anatoka juu kuja kulazimisha kwamba yanahitajika matawi. Amejuaje mahitaji hayo? Katika hili, Halmashauri ya UVCCM ilikutana na kujadili kwamba hakuna umuhimu huo au taratibu hazikufuatwa. Sasa uhalali huo wameupata wapi akina Malisa?

Malisa anaweza kubishia kila kitu anachohusishwa nacho, lakini kunapokuwa na ushahidi wa dhamira mbaya na kutumiwa kwa malengo ya kundi fulani kwa ajili ya 2015, hahitaji kukiri pia. Kila kitu kiko wazi na kila mtu sasa anajua kwamba huyu bwana ameshuka kutoka kuwa Mkubwa wa UVCCM mpaka kuwa kijana wa kazi na tarishi wa kundi fulani. Njaa bwana!
 
Back
Top Bottom