Makundi ya Damu (blood groups) na Mahusiano

Heshima zenu popote mlipo na poleni na kupanda kwa gharama za maisha........

Moja kwa moja kenye mada

Kuna uhusiano kati ya Kundi la damu na Tabia ya mtu katika mahusiano/mapenzi.
Kwa mujibu wa tafiti na machapisho mbali mbali zifuatazo ni baadhi ya sifa za watu kulingana na kundi la damu (blood group) katika mahusiano au mapenzi.

Blood group "A"
* Ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao
*Sio waongo (waadilifu na wakweli)
*Wana aibu na waoga hupenda kujificha
*Ukitaka kuchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi A unahitaji uvumilivu
*Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote ingawa wataruhusu ufahamu sehemu ambayo unahusika. Hawawi wazi kila eneo

Blood group "B"
*Unaweza kufurahi nao sana kwenye mahusiano lakini uwe tayarii kuvumilia hasira zao za ghafla
*Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu
*Wanaweza kuwa wakali na wakatili na wasiomaanisha kile wanachosema.
*Wanatabia ya umbea na wachonganishi sana
*Wanaweza wasiwe watu wazuri kuwa wapenzi kutokana na kukosa uaminifu na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine

Blood group "AB"
*Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi
*Ni watu ambao mara nyingi hawaeleweki. Anaweza kuanzisha
Kitu kikaishia katikati halafu akaanzisha kingine
* Ni watu wazuri kwenye mambo yanayohusu fedha
*Ni wabishi na wakosoaji na mara nyingine hutoa maneno yanayo umiza
*Ukiwa katika mahusiano nao hufurahisha na unaeeza usiwe na nyakati nyingi za upweke

Blood group "O"
*
Huonesha mapenzi kwa wale wanaowapenda na hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao
*Wanaaminika kuwa na tabia za kijeshi
*Wana roho nzuri sana ila hawapendi uongo
---###-------###------

Kutokana na utafiti huu Binafsi naona kuna uhalisia kulingana na tunayokutana nayo katika jamii.
Tabia ni kama ngozi kuisha hadi uchune japo nguvu ya "pesa" inajaribu kuficha tabia za baadhi ya watu hasa wanawake.
Tujifunze kuishi nao maana ndivyo walivyo na hawawezi badilika maana washwahili wanasema "Mbwa ukimjua jina hakusumbui"
Ukiona hamuendani kitabia na unampenda jitahidi ujue mbinu za kivita za kuishi naye blood group inaweza kukusaidia maana nzi kufia kwenye kidonda sio ufala ila kupenda

Nakaribisha maoni ......
Group O stand uuuuuup
 
Godmmit brother.. umepatia kabisa.
Kwa kuongezea group O si pushover, ni wavumilivu ila ukiwapanda kichwani watakuadhib with extreme prejudice. Halaf ni watu wa maamuzi magumu sometimes
Hii ya maamuzi magumu hii, nishaifanya Sana tuu... Na sipendi kuona mtu akionewa, nitamtetea Kwa Hali yoyote ile kama uwezo ninao. Ni mpole sanaaa lakini pia ukinitibua doh hutaamini na macho Yako.
 
Group O, Kila kitu ni ukweli mtupu. Uongo dah nauchukia Sana Sana. Msimamo ss, liwe zuri liwe baya nikilisimamia siliachii.... Siwezi kumtendea mtu ubaya, nikikwambia nakupenda basi namaanisha.
 
Huu Uzi haijakamilika.
Kuna group
A+
A-
B+
B-
AB
O+
O-

Hakika hawa watu utaweza kuchambua ukihusisha kundi la damu na Rhesus factor zao.

N.B Mimi ni B+
 
Huu Uzi haijakamilika.
Kuna group
A+
A-
B+
B-
AB
O+
O-

Hakika hawa watu utaweza kuchambua ukihusisha kundi la damu na Rhesus factor zao.

N.B Mimi ni B+
Somo lilihusiana na blood groups in term of ABO system na sio rhesus factor mkuu bt asante
 
Back
Top Bottom