Makundi ndani ya vyama vya siasa ndio mtaji mkubwa wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makundi ndani ya vyama vya siasa ndio mtaji mkubwa wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Oct 14, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Katika historia ya siasa nchini inaonyesha makundi ndani ya vyama vya siasa inachangia mgawanyiko mkubwa na hatimaye kusambaritika na ndio mtaji mkubwa kwa chama cha CCM.

  Miongoni mwa vyama vilivyosambaratika na makundi, na kuporomoka kutoka kileleni mpaka sakafuni ni NCCR Mageuzi, makundi mawili ya aliyekuwa mwenyekiti Augustine Mrema, na aliyekuwa katibu wake Mabere Marando, NCCR Mageuzi ilikuwa na wabunge 19 ilijikuta ikiporomoka hadi kukosa mbunge hata mmoja kwa vipindi vitatu vya miaka 15.

  Chama cha CUF imepataka kumeguka takribani mara tatu tangu kianzishwe kutokana na makundi ilianzia kwa James Mapalala aliyekuwa mwenyekiti wa kwanza wa CUF alitimuliwa na kupunguza nguvu ya CUF na kukirudisha nyuma, kundi la pili ni la kina Hamadi Rashid ambalo lilitimuliwa ndani ya chama hicho lilitaka kumng'oa Maalim Seif, CUF imekosa mvuto inaonekana ni maslahi binafsi.

  Chama cha Chadema kinavyotazamwa kama chama kikuu cha upinzani nchini kwa hivi sasa, nacho kinaonekana kufuata nyayo zile zile zilizopitia CUF na NCCR Mageuzi, harufu ya makundi imeanza kunukia lilianza kundi la marehemu Chacha Wangwe, alipotangaza kuwania ya uenyekiti jambo ambalo lililomleta mgogoro mkubwa ndani ya chama hadi mauti yalimpomkuta, limeibuka kundi la Zitto Kabwe ambalo limeendelea kukitesa chama hicho kutokana na msimamo wake wa kugombea urais.

  Zitto mwenye wafuasi wengi wanaomunga mkono ndani ya Chadema, anatajwa kuwa na mtandao mkubwa, vile vile kuna kundi la Dr Slaa ambalo alitaki kabisa Zitto Kabwe agombee urais kupitia Chadema.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MFUMO MPYA WA 'UANAMTADAO' NI ADUI MKUBWA HAKI KUCHAGUA NA KUCHAGULIWA HIVYO HUFIFISHA DEMOKRASIA KATIKA NCHI, WATU WENYE AKILI ZURU TU HUGEUKA MATAAIRA GHAFLA NA HATIMAYE UCHUMI WA KIFISADI KUPATA MBOLEA

  Urais unapopatikana misingi ya UNAMTANDAO katika taifa, wananchi wapiga kura mwisho wa siku hubakia tu kama watazamaji katika uendeshwaji wa serikali itakayopatika na misingi yote ya kidemokrasia husalitika kwa kiasi kikubwa.

  Kosa hili likirudiwa tena Tanzania wengi walioko nje ya mipaka ya UANAMTANDAO huo kamwe hawatokua mali kitu na mwisho chuki kuchukua mimba na sura mbaya kujitokeza katika taifa. Kila mmoja tujihdhari sana.

  Katika mfumo kama huo wa UANAMTANDAO, mambo mengi ni geresha tupu na hata uchaguzi ama ndani kwa ndani ya chama ni geresha na ule wa kitaifa nao hufuata mkondo kama huo huo na kudhihirishie wengine wengi tu ukweli wa haya maneno machungu; 'NDANI YA UANAMTANDAO HACHAGULIWI MTU, HUCHAGULIWA POCHI'.

  Mzee Hassan Ngwilizi, Fredrick Sumaye, Malecela Junior, Makongoro Nyerere pamoja na wengine wengi wa aina yao, katika mfumo wa UANAMTANDAO, kamwe kura zao haziwezi zikaja zikatosha hata siku moja kwa kuwa ile sifa mama ya UANAMTANDAO kwamba hachaguliwi mtu bali huchaguliwa pochi, hawana hiyo sifa bado.

  Enyi wenzetu ambao inaonekana kwamba KURA HAZIKUTOSHA huko kwenye uchaguzi ndani ya CCM unaoendelea hivi sasa kote nchini, nawapeni pole sana kwa kuwa hamkujua sheria na kanuni za mfumo huo mpya wa siasa ulioibuka ndani ya nchi yetu tangu 1995.


   
 3. b

  blueray JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Mkuu, lakini mbona hujashauri chochote? Au unafurahia makundi ndani ya vyama Na hatimaye kuporomoka kwa vyama vya upinzani ili CCM iendelee kutawala milele?
  Halafu Mkuu, nani mastermind wa haya makundi ndani ya vyama?
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa maneno machache ni kwamba taifa zima linajikuta likilazimika kuwa mateka wa MAFISADI wachache wanaowekeza mabilioni kuwalipa HATA WASOMI WASAFI SANA VICHWANI kuhiari kuwatumikia katika makundi ndani ya vyama mbali mbali, na uwezo wa kufikiri kuwasimama kabisa tena na badala yake hujikuta fikra zao zikikimbiza tu mikondo mbalimbali kuliko na dau kubwa zaidi.

  Hali kama hii NI HATARI SANA KATIKA USTAWI MZURI NA MUSTAKABALI MZIMA WA TAIFA: ni huzuni tena simanzi kubwa kuona ukweli kwamba mbele ya MAFISADI wachache 'karibia kila goti litapigwa na watu wazima kugeuka watoto, vijana wenye nguvu na mtaji wa taifa la kesho kuanza kushindana katika viwango vya ubora zaidi na hata kupigana vikumbo katika kuwaabudu wateule wachache hawa ilmradi mkono uende kinywa.

  Huo ndio mfumo mpya wa UANAMTANDAO tulioridhishwa tangu 1995 unavyofanya kazi na na juhudi zingine zote za kidemokrasi katika uhalisia wake hugeuka majivu, na kile nilichowahi kukiita MKAKATI CCM-AMOEBA (CCM kuwaajiri makuwadi katika kila chama cha siasa kuwatumikia wao kwa kadiri hali inavyoruhusu ili kuwashinda wapiga kura wanaokichukia hivi sasa wasiweze kukiondoa madarakni) ndani ya mfumo usio rasmi kisiasa duniani uitwao uanamtandao.

  Ili mfumo huu mpya uweze kufanya kazi vema ni shurti (1) wamiliki wake wawe na fedha za kumwaga, (2) kuwepo na wasomi wazuri sana lakini wenye utayari kutumikishwa kwa maslahi ya wateule wachache, (3) tasisi za kiserikali zinazobinafsishika, (4) baadhi ya vyombo vya habari vinavyohifadhika mifukoni (5) wapiga kura wasioelimishwa vya kutosha kuhusu haki na majukumu yao ya uraia katika taifa na (6) utitiri wa vikao vya siri usiku wa manane.

  Hakika ni huzuni kubwa kuona hata hizi baadhi ya best brains katika taifa letu kujitolea to the drains tena kwa nguvu mpya, kasi mpya na ari mpya katika kusaliti umma wa Tanzania kiasi hiki.

  Naam, hakika nawaambieni hapa leo hii, endapo vijana wasomi hawa hawatojirudi na kutazama katika ukweli wote hali ya umasikini ya vijiji walikotoka na hata kukataa kutumikia MAFISADI katika mfumo wao mpya wa UANAMTANDAO chini ya MKAKATI CCM-AMOEBA huu, taifa litaangamia mbele ya safari kwa kuwa vijana wamehiari kutumika vibaya ujana wao leo hii kabla haujageuka wa baridi kama brafu katika uzee wao kesho.
   
 5. r

  rombo girl Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 6, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa sasa Tanzania haijapata chama kizuri kama ccm ukweli utabaki palepale.ww sasa mtu anayetuka na watu awe rais ww ni nani asikutukane.tukizungumzia mafisadi ruhasa hamshindi zzito kabwe kwa ufisadi.mm ni chadema Ila 2015 nawapa ccm ni bora kuliko kutengeneza vita ya chadema.
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka maneno ya Dr Kitila Mkumbo "anasema uwepo wa makundi katika vyama vya siasa ni jambo lisiloepukika isipokuwa jambo la msingi ni vyama kuruhusu demomokrasia ya kweli, ukigombea lazima uwe na kundi linalokuunga mkono huwezi kufuta hili".
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kama CDM watatikiswa na mtu asiye na sifa za kikatiba za kugombea urais itakuwa ni bonge la kichekesho, sawa na kumuogopa chui wa mambao au kuogopa sanamu ya simba.

  Mimi nawashauri CDM waendelee na M4C, itaimarisha chama na chama kikishakuwa mioyoni maw Watanzania hata wakimsimamisha Ritz kugombea urais atashinda. Ila wakiwekeza kwenye makundi ya urais kwa watu wasio na sifa wataishia kunawa tu. Watu hawajiulizi kauli ya Wassira kuwa CDM itasambaratika 2012 ilikuwa na maana ya kumtumia wakala gani kusambaratusha chama?
   
 8. m

  matasha JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kulinganisha CCM na Chadema sawa na kulinganisha kifi na usingizi, kifo ccm na usingizi chadema
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hii thread imeletwa na mtu aliyelewa gongo
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,744
  Likes Received: 12,822
  Trophy Points: 280
  Nilijua nia yako ni kumchafua zitto na chadema!

  "Zitto ni chadema, chadema si zitto-zitto"

  Ccmweli bwana, yani mnaona uongo ni mtaji
  Nani asiye jua kwamba ccmweli kuna makundi na ndio mtaji wa wawa pinzani?

  Yani umeona ugeuze topic kupima upepo!
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana na huyu mlevi anaetembea na vibiriti na mafuta ya taa
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tatizo la msingi siyo uwepo wa makundi ila unafiki wa kutokuwa wawazi kuhusu makundi. Kama kiongozi au mwanachama anamuunga mkono mgombea fulani ni busara na hekima kuwa muwazi na kuelezea hadharani kuwa anamuuga mkono mgombea huyo ili jamii yote itambue hilo na kufanya maamuzi sahihi kutokana na taarifa hiyo.
   
 13. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hebu rekebisha kwako kwanza kabla ya kutoa nasaha zako kwa wengine
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Kinachosababisha mpasuko katika vyama vya siasa hususani vile vya upinzani ni kuwapo kwa mfumo wa chama kimoja ndani ya vyama vingi ambao unatengenezwa na viongozi wa vyama.
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Badala ya kujenga hoja unamshambulia mleta hoja.
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni wapi nimemchafua Zitto na Chadema, mie nimelezea makundi katika vyama vya siasa nimewataja NCCR Mageuzi, CUF, Chadema huo ndio ukweli mkuu.
   
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Athari za makundi zinazokumbukwa na ambazo zimeacha fundisho katika historia za siasa za nchi ni mpasuko ndani ya CCM kutokana na mafanikio yaleyoletwa na na mtandao ulimumweka rais Kikwete madarakani mwaka 2005, licha ya faida iliyopatikana ya kufanikisha malengo yake, ni mtandao huo huo uliochangia kuleta ufa ndani ya CCM na kuzaa makundi ambayo yalisababisha kupoteza baadhi ya majimbo.
   
 18. b

  blueray JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hapa naona hueleweki! ila we endelea kulala, si tunasonga mbele
   
 19. b

  blueray JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Ritz, we huoni mamluki wanaopandikizwa Na chama tawala kwa kiasi kikubwa ndio wanaleta migawanyiko ndani ya vyama?
   
 20. K

  Kahamba Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Makundi ndani ya CDM ni ya kufikirika. Ni wazi Zitto anatamani kuwa na kundi kubwa la kumuunga mkono ingawa imemuwia ngumu kutokana na uthabiti wa uongozi wa juu. Lakini sioni hicho kinachoitwa "Kundi la Dk. Slaa". Dk Slaa hahitaji kuwa na kundi. Watu huanzisha makundi kwa maslahi binafsi, hasa tamaa ya uongozi. Lakini ikumbukwe kwamba Dk. hakutaka hata kugombea urais 2010 mpaka baada ya kuombwa sana. Ila anaungwa mkono na wengi. Ila anayepingana na Dk Slaa huyo ndo analazimika kuunda kundi la kumuunga mkono. Tahadhari " Hatuhitaji makundi ndani ya CDM". Anayeshabikia makundi aende CCM yanakozaliwa.
   
Loading...