Makundi ndani ya chama yawang'oa viongozi wa CCM tawi la UDOM. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makundi ndani ya chama yawang'oa viongozi wa CCM tawi la UDOM.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by nsami, Jun 11, 2010.

 1. n

  nsami Senior Member

  #1
  Jun 11, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uongozi wa CCM tawi la UDOM college of Education chini ya mwenyekiti Nickson Mmanyi wiki iliyopita ulitangaza kujiuzuru uongozi baada ya wanachama wake kugomea uchaguzi wa viongozi uliotakiwa kufanyika siku hiyo huku mhe Mmanyi na katibu wake Ndg Egla Mamoto wakiwania kukomboa viti vyao.

  Ni ktk kikao cha mkutano mkuu wa tawi kilichofanyika 5 June 2010 ktk ukumbi wa Halimashauri kuu ya CCM Mjini Dodoma kwa madhumuni ya kufanya uchaguzi huku candidates wote wa uchaguzi huo wakiwa ni viongozi wale wale (wasiotakiwa). Ndipo hoja ilitolewa na wajumbe ya kutokukubaliana na uchaguzi kwa kile walichodai mchakato wa kuwapata wagombea ulighubikwa na wingu la urafiki, ukabila na maslahi binafsi, na kutafsiriwa kuwa ni mwendelezo wa mnyukano wa makundi ya siasa za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi uliofanyika mwezi uliopita.

  Kufuatia hatua hiyo, viongozi wa muda waliteuliwa kuongoza tawi mpaka uchaguzi utakapotangazwa tena.
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  sasa hicho kichwa cha habari JF inahusikaje?
   
 3. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Ni siasa za vyuoni/ki-anafunzi.
  Hivi maeneo ya kazi vyama vinaruhusiwa kufungua matawi? Au CCM inaruhusiwa.

  Naona CCM imeanza mtindo wa kufungua matawi vyuoni! What for? Au ndo Ufisadi?
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Jun 11, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nadhani ungawapelekea UVCCM ingekuwa bomba..Hapa sio mahali pake!
   
Loading...