Sasa ni dhahiri ndani ya CCM kuna kundi la Rais Samia na la Hayati Magufuli

Hahahahaaaa.Makamu wa Rais huwa kazi yake ni IPI?awamu ya tano na ya 6 ni kitu kimoja.ilani chama ni ile ile.na alishiriki kuinadi.kusema kweli Rais ana kazi ngumu ya urais kwa sababu yuko na watu ambao hakuwanadi kipindi cha kampeni.ushauri ni kwamba akitaka kumaliza awamu hii kwa amani atekelezi ilani ya CCM iliyonadiwa 2020 na miradi iliyoanzishwa na awamu ya Tano.Asipende kuanzisha vyake na kujaribu kumpinga hayati JPM wakati anafahamu fika alikuwa mshauri wake.kuna kitu tunakiita Autoinoculation. Asipokuwa makini atajimaliza mwenyewe.kuna watu wabaya wakitaka kummaliza kisiasa wanaweza kutumia hata kifo cha mtangukizi wake.usimwamshe simba aliyelala
Yaan nyie mnao sema alishiriki ya awamu ya 5 huwa nawaona ni wajinga na wapumbavu hivyo tu.
Kwa sababu nina uhakika hata wewe kuna mengi umeyaamua ndan ya familia yako kama baba wa familia lakini hayampemdenzi mkeo wala watoto wako lakini kwa vile wewe ndiye baba mkaidi wamekuacha tu.
 
Huu ndio ukweli ulio wazi ingawa CCM wenyewe hawawezi kukiri hadharani. Kuna hatari ya kundi la Mwendazake kutaka kumuhujuma Mama na mnyukano huu unalenga uchaguzi wa 2025.

Hata hivyo, kundi la Mwendazake wajue tu kwa katiba hii mbovu, hakuna wataloweza na ninachowashauri waungane na wapinzani kudai katiba mpya vinginevyo wataishia kupiga kelele tu.

Kuna dalalili Mama kachoka kuwavumilia na sasa kaamua kuanza kuanika madidu ya awamu iliopita lengo ni kuthibitisha hata awamu iliopita kulikuwa na wizi na ufisadi.

Ngoma inogile.
Mapigaji matupu, tena huyu kwa kulialia atadhani watu watamwonea huruma ipo watanzania watachoka kuvumilia upuuzi.
 
Ni mtu asiye na uwezo wa kufanya jambo ndiyo hukimbilia kusingizia sababu lukuki.
Wewe una nguvu zote na vyombo vyote na mamlaka yote,unahujumiwajee!!?
Hizo taasisi kwa nini ziendelee kuwepo kama hazifanyi kazi zake!?
Unahujumiwajee ukiwa na TISS!!??

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Kumeibuka utamaduni wa baadhi ya wanaCCM kuwaita wenzao ambao hawana muda mrefu ndani ya chama 'wa kuja', 'wa kuletwa' na majina mengine mengi yanayotweza uanachana wao.

Misingi na kanuni za CCM zinatambua usawa wa kila mwanachama bila kujali nafasi yake au muda wake ndani ya CCM lakini watu ambao hawakushiriki kuandika kanuni hizo wanajiona ni bora sana.

CCM ndio chama pekee cha siasa Tanzania chenye Sera zenye kuleta mshikamano, umoja na amani na ndio chama pekee chenye sifa ya kutoa kiongozi bora na safi. Hivyo mjadala huu wa kudharauliana unapelekea kujenga ufa wa mshikamano na umoja.

CCM maslahi ni hatari sana, kazi ya mwanaCCM ni kuonesha njia kwa wengine lakini inapotokea wakongwe ndani ya chama wanawaona wachanga hawafai kushika madaraka basi ni ishara kwamba hatutaki wanachama wapya na hiki kitasababisha anguko kubwa.

Kauli kama hizi zinatolewa na watu wa kundi Fulani kulinda maslahi ya kundi lake na si kwa maslahi mapana ya nchi yetu, siasa za makundi ni hatari sana si tu ndani ya CCM ila kwa taifa letu kwa ujumla. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana.

Rai yangu kwa mwenyekiti wangu MHe. Samia Suluhu Hassan, unayo nafasi kubwa ya kuvunja makundi ndani ya CCM ili kuleta usawa wa haki kwa wanaCCM. Kauli hizo zinatia hofu wenye uwezo na weledi wa uongozi kugombea nafasi za uongozi wakiamini ni wakuja tu hivyo hawana nafasi yoyote ndani ya CCM.

Ndugu Mwenyekiti, kwa nafasi za uteuzi na kugombea tunaomba watu wasio na makundi na wenye uadilifu usio tia shaka wapewe nafasi. Naamini tunao Mzee Mangula wengi ambao ni waadilifu kweli kweli.
 
Miaka 60 ya kutawaliwa na chama dola bado maadui wale wapo na wametamalaki zaidi,umasikini,maradhi na mbaya zaidi UJINGA (na hili middle class wengi wamo kundi hili,wamepata mwanga wa elimu ila bado hawajafuta UJINGA)
 
Hayo mafisi yanagombana wee ukitokea mzoga wanaacha ugomvi kwanza wanafanya karamu, wakimaliza njaa zukianza kuwauma wanalianzisha tena
Masikini keki ya taifa inataka kuyatoa roho maviroboto na mahuni ya chama dola.
 
Samia kaanza kutukana mawaziri kwa kuwageuzia kibao kama vile kwenye uingizaji wa sukari toka nje waziri mkuu na waziri wa kilimo waliosema NO they are nuisence hilo ni tusi,,, Mkenda na Majaliwa wana damu ya uzalewndo siyo upigaji
Sasa pale kamuweka mtoto wa Rostam ( Bashe) watapiga magendo ya vibari vya kuagiza sukari nje nje!
 
Jana ndio nimethibitisha hii kitu baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri.
 
Kabla ya mwaka 2015 tulikuwa tukishuhudia baadhi ya wanachama maarufu na wenye nguvu ya ushawishi wakiwa na makundi yao ndani ya chama kwamba lolote litakalopangwa na watu hao wenye nguvu basi uwezekano wa kufanikiwa ni mkubwa kutokana na safu itakavyopangwa.

Tuliwashuhudia akina kikwete,lowasa,membe, n.k tuliona namna walivyokuwa na ushawishi ndani ya chama na kwa asilimia kubwa kila waliyoyapanga kufanikiwa na ndio maana hata uamuzi wa kukata majina ya lowasa na membe kwenye uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni uamuzi mgumu Sana ndani ya chama kuwahi kutokea na tuliona mtikisiko uliojitokeza baada ya kuyakata majina ya hao miamba.

Sasa baada ya ujio wa JPM tuliona nae kupitia ushawishi mkubwa aliokuwa nao nae alisepa na kijijii yaani watu walimpenda na kumtukuza yeye(mtu) zaidi kuliko chama kitendo ambacho kilizalisha kundi jingine kubwa ambalo ni sawa sawa kabisa na Yale makundi ya akina lowasa enzi hizo licha ya JPM mwenye kujinasibu kuwa ameua na kuondoa makundi yote ndani ya chama chake pasipo kuona kundi kubwa alilojitengenezea yeye binafsi.

Nilichokiona mpaka Sasa watu wengi wanaokesha kuukosoa utawala wa awamu ya sita na kupinga uwepo wa mapungufu yaliyokuwepo awamu ya tano kwa kuleta huku wakikubali kuwa marehemu hakuwa malaika lakini bado wanataka asisemwe kwa mapungufu ya serikali yake hata Kama yatasemwa kwa nia njema ili tujirekebishe huko mbeleni, kwa wachache kutoka kundi la jpm wanaokubali kuwa kulikuwa na mapungufu ya kibinadamu hutaona wakiainisha hayo mapungufu waziwazi hata Kama ni kwa nia njema.

Leo hii ikitokea uteuzi ama utenguzi wa waziri yeyote utaona Kuna watu hawafikilii juu ufanisi wa muhusika zaidi ya kuangalia huyo mtenguliwa au mteuliwa anatokea kundi gani na ikitokea mteule wa aliyekuwa rais wa awamu ya tano akatenguliwa utaona namna watu kutoka kundi husika watakavyo isakama na kuinanga serikali juu ya utenguzi husika kwao hao wateule ni malaika hawakosei hata wakifanya makosa waachwe.

Ombi kwa watawala wetu, wajitahidi kuimarisha mifumo zaidi kuliko kujiimarisha mtu binafsi kwani athari ya mtu mmoja kuwa imara zaidi kuliko taasisi madhara yake yatajitokeza siku atakapokuwa nje ya mfumo husika yaani nchi itajikuta inarudi kwenye matatizo makubwa zaidi kuliko hata yaliyokuwepo.
Wananchi pia wapewe elimu ya uraia ya kutosha ili wasiingie kwenye mtego wa kuwa shabiki wa mtu badala ya taasisi.
 
Kabla ya mwaka 2015 tulikuwa tukishuhudia baadhi ya wanachama maarufu na wenye nguvu ya ushawishi wakiwa na makundi yao ndani ya chama kwamba lolote litakalopangwa na watu hao wenye nguvu basi uwezekano wa kufanikiwa ni mkubwa kutokana na safu itakavyopangwa.

Tuliwashuhudia akina kikwete,lowasa,membe, n.k tuliona namna walivyokuwa na ushawishi ndani ya chama na kwa asilimia kubwa kila waliyoyapanga kufanikiwa na ndio maana hata uamuzi wa kukata majina ya lowasa na membe kwenye uchaguzi wa 2015 ulikuwa ni uamuzi mgumu Sana ndani ya chama kuwahi kutokea na tuliona mtikisiko uliojitokeza baada ya kuyakata majina ya hao miamba.

Sasa baada ya ujio wa JPM tuliona nae kupitia ushawishi mkubwa aliokuwa nao nae alisepa na kijijii yaani watu walimpenda na kumtukuza yeye(mtu) zaidi kuliko chama kitendo ambacho kilizalisha kundi jingine kubwa ambalo ni sawa sawa kabisa na Yale makundi ya akina lowasa enzi hizo licha ya JPM mwenye kujinasibu kuwa ameua na kuondoa makundi ndani ya chama chake pasipo kuona kundi kubwa alilojitengenezea yeye binafsi.

Nilichokiona mpaka Sasa watu wengi wanaokesha kuukosoa utawala wa awamu ya sita na kupinga uwepo wa mapungufu yaliyokuwepo awamu ya tano kwa kuleta huku wakikubali kuwa marehemu hakuwa malaika lakini bado wanataka asisemwe kwa mapungufu ya serikali yake hata Kama yatasemwa kwa nia njema ili tujirekebishe huko mbeleni, hapo utaona wengi wanaopinga serikali ya sasa awamu ya sita wanapinga kwa hisia zaidi kuliko uhalisia kutokana na kuwa sehemu ya makundi yaliyojijenga na kuwa matiifu kwa mtu kuliko taasisi.

Leo hii ikitokea uteuzi ama utenguzi wa waziri yeyote utaona Kuna watu hawafikilii juu ufanisi wa muhusika zaidi ya kuangalia huyo mtenguliwa au mteuliwa anatokea kundi gani na ikitokea mteule wa aliyekuwa rais wa awamu ya tano akatenguliwa utaona namna watu kutoka kundi husika watakavyo isakama serikali juu ya utenguzi husika kwao hao wateule ni malaika hawakosei hata wakifanya makosa waachwe.

Ombi kwa watawala wetu, wajitahidi kuimarisha mifumo zaidi kuliko kujiimarisha mtu binafsi kwani athari ya mtu mmoja kuwa imara zaidi kuliko taasisi madhara yake yatajitokeza siku atakapokuwa nje ya mfumo husika yaani nchi itajikuta inarudi kwenye matatizo makubwa zaidi kuliko hata yaliyokuwepo.
Wananchi pia wapewe elimu ya uraia ya kutosha ili wasiingie kwenye mtego wa kuwa shabiki wa mtu badala ya taasisi.
Mambo ya CCM wewe Chadomo yanakuhusu nn

USSR
 
Membe hakukatwa jina bali alishindwa kwenye sanduku la kura kwa ushawishi wa Lowasa.

Hata Magufuli Urais alipewa na Lowasa ndio sababu ya Magufuli siku zote alimuheshimu Lowasa aliujuwa ukweli hasira za Lowasa kura zake akapewa Magufuli.
 
Hakuna kundi wala wafuasi wa Magufuli ndani ya CCM.

Wanasiasa huangalia manufaa yao binafsi na ndio maana Kinana alipita kwa 100%.

Mwanasiasa pekee aliyeangalia masilahi ya umma ni Magufuli tu.
Hata wewe mkuu unatetea maslahi yako binafsi na sio ya umma?
 
Huu ndio ukweli ulio wazi ingawa CCM wenyewe hawawezi kukiri hadharani. Kuna hatari ya kundi la Mwendazake kutaka kumuhujuma Mama na mnyukano huu unalenga uchaguzi wa 2025.

Hata hivyo, kundi la Mwendazake wajue tu kwa katiba hii mbovu, hakuna wataloweza na ninachowashauri waungane na wapinzani kudai katiba mpya vinginevyo wataishia kupiga kelele tu.

Kuna dalalili Rais Samia kachoka kuwavumilia na sasa kaamua kuanza kuanika madidu ya awamu iliopita lengo ni kuthibitisha hata awamu iliopita kulikuwa na wizi na ufisadi.

Ngoma inogile.
Sasa wewe unaungana na Marehemu atafufuka kukusaidia ? Si utakuwa ni taahira wewe.
 
Hakuna kundi wala wafuasi wa Magufuli ndani ya CCM.

Wanasiasa huangalia manufaa yao binafsi na ndio maana Kinana alipita kwa 100%.

Mwanasiasa pekee aliyeangalia masilahi ya umma ni Magufuli tu.
Kama haya hapa 👇

Screenshot_20220416-182331.png
 
Back
Top Bottom