Makundi 9 ya wapiganaji yaungana dhidi serikali ya Ethiopia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Makundi 9 yanayopiga vita serikali ya Ethiopia, yametangaza kuunda muungano hii leo ili kulazimisha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Hatua hiyo inaongeza shinkizo dhidi ya Waziri mkuu Abiy Ahmed, wakati makundi ya wapiganaji yakiendelea kukaribia mji mkuu wa Addis Ababa.

Makundi kadhaa yamejihami kwa silaha japo haijabainika iwapo makundi yote yanayopinga serikali yana silaha.

Makundi ya wapiganaji wa Oromo na lile linalodai kupigania demokrasia la Agaw, yameambia shirika la habari la Reuters kwamba muungano huo unaojumulisha wapiganaji wa Tigray, ni halali.

Wapiganaji wa Tigray wamekuwa wakipigana na serikali kwa mwaka mmoja sasa katika vita ambavyo vimeua maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni mbili kutotoka makwao.

Mataifa ya Afrika na ya magharibi yamekuwa yakitaka mapigano kusitishwa mara moja nchini Ethiopia, baada ya wapiganaji wa Tigray kusema kwamba wanaelekea kudhibithi mji mkuu wa Addis Ababa wiki hii.

Wapiganaji wametangaza kudhibithi mji wa Kemise, kilomita 325 kutoka Addis, lakini serikali imefutilia mbali madai hayo na kusema kwamba wapiganaji wanatoa habari za uongo kuhusu walipofikia.

VOA Swahili
 
Nchi imepitia majanga sana hii. Njaa, vita za wenyewe kwa wenyewe hadi kujitenga kwa Eritrea na sasa bado hakijaeleweka. Juhudi za kufufua uchumi ndo zilianza kuchipua, sasa zinafifia. Sijui bwawa la umeme litapona? duh!

Hapo ukichunguza hukosi kusikia ka mkono ka USA na jamaa zake.

Mungu ibariki Afrika
 
SPONSOR NI USA NA UK .

Ethiopia ilikuwa inakua kwa speed ya hatar , so ili kustop , suluhisho ni vurugu ka hizo.
Sio kweli kuna nchi ngapi zinazopaa kiuchumi mbona hawapigani. Ethiopia kwa muda mrefu imekuwa ikitawaliwa kidikteta sana na wapinzani wamekuwa wakinyanyasika sana ktk nchi hiyo.

Hili linalofanyika Ethiopia iko siku itakuja kufanyika hata hapa Tanzania ambapo ccm imegeuza Chadema kuwa "Their Punching Bag" kwa manyanyaso na mauaji ya watu wake.
It's just a matter of time.
 
Makundi 9 yanayopiga vita serikali ya Ethiopia, yametangaza kuunda muungano hii leo ili kulazimisha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Hatua hiyo inaongeza shinkizo dhidi ya Waziri mkuu Abiy Ahmed, wakati makundi ya wapiganaji yakiendelea kukaribia mji mkuu wa Addis Ababa.

Makundi kadhaa yamejihami kwa silaha japo haijabainika iwapo makundi yote yanayopinga serikali yana silaha.

Makundi ya wapiganaji wa Oromo na lile linalodai kupigania demokrasia la Agaw, yameambia shirika la habari la Reuters kwamba muungano huo unaojumulisha wapiganaji wa Tigray, ni halali.

Wapiganaji wa Tigray wamekuwa wakipigana na serikali kwa mwaka mmoja sasa katika vita ambavyo vimeua maelfu ya watu na kulazimisha zaidi ya milioni mbili kutotoka makwao.

Mataifa ya Afrika na ya magharibi yamekuwa yakitaka mapigano kusitishwa mara moja nchini Ethiopia, baada ya wapiganaji wa Tigray kusema kwamba wanaelekea kudhibithi mji mkuu wa Addis Ababa wiki hii.

Wapiganaji wametangaza kudhibithi mji wa Kemise, kilomita 325 kutoka Addis, lakini serikali imefutilia mbali madai hayo na kusema kwamba wapiganaji wanatoa habari za uongo kuhusu walipofikia.

VOA Swahili
Wacha wamchape atie akili.
Hili ndio tatizo la kuruhusu jamii moja inakuwa na nguvu za kijeshi kuliko zingine,hao Watigrey ni asilimia 6 tu ya wananchi wote,
Ubaya wa kuruhusu jamii zijione kikabila zaidi.Baada ya kuipindua Serikali,hizo jamii nazo zitataka kujitenga na kuwa nchi huru.
 
SPONSOR NI USA NA UK .

Ethiopia ilikuwa inakua kwa speed ya hatar , so ili kustop , suluhisho ni vurugu ka hizo.
Ila huu upuuzi wanaanzisha viongozi wa Africa. Hivi mfano watu wana pinga mambo fulani fulani na hawataki serikali muendelee why tu kidemokrasia msikubali nankuachia ngazi ili wengine wakae na wao wakileta upuuzi si mnawabalasa tu.
 
Siyo kweli nini ?

Kwamba wazir mkuu alivianzisha, yan watu wajitangazie uhuru wao ndani ya nchi huru then uwachekee???

Leo hii Kilimanjaro iseme ni nchi huru then waachiwe hv hv hali ya kuw hawatak hat majadiliano
 
Ila huu upuuzi wanaanzisha viongozi wa Africa. Hivi mfano watu wana pinga mambo fulani fulani na hawataki serikali muendelee why tu kidemokrasia msikubali nankuachia ngazi ili wengine wakae na wao wakileta upuuzi si mnawabalasa tu.
Kwa mazingira ya Ethiopia ya sasa we ungekuwa Rais uamuzi wako ungekuwa kuachia ngazi?
 
Back
Top Bottom