Makumira university:heslb[bodi ya mikopo]mmetufanyia usanii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makumira university:heslb[bodi ya mikopo]mmetufanyia usanii

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kinganola, Oct 21, 2011.

 1. kinganola

  kinganola Senior Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu mpango wa HESLB wa kutuma pesa za Wanafunzi Chuoni moja kwa moja,Chuo cha Makumira tumebaini usaanii mkubwa tuliochezewa na bodi.Raisi wa Chuo chetu Bw.Benard Adam alikuwa Bodi kwa muda wa wiki nzima akifuatilia suala la pesa za Wanafunzi wa mwaka wa pili na wa Tatu.Tunashukuru jumatano ya tarehe 19.10.2011 amerudi na majina ya kusaini ili tuingiziwe pesa za Accomodation na Stationary,Chakusikitisha majina yaliyokuja ni 820 wakati wanaostahili kupewaa mkopo ni wanachuo zaidi ya 1500,mbaya zaidi wengi ya ambao hawajapewa na wanaosoma Sheria mwaka wa pili na wa tatu,tumewapigia simu mnajifanya kushangaa,sasa mnataka nini?,Kweli ninyi ni chanzo cha Migomo vyuoni.
   
 2. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Wanataka mgome kaka mbona hilo liko wazi.
   
 3. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Na Mosha naye atawakurupua sasa hv,poleni andaeni mgomo mwende mkagome bodi
   
 4. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Raisi wenu hajui idadi ya watu wake wanaopata mkopo HESLB?hayo majina alikabidhiwa yakiwa sealed kiasi kwamba hata hakuyaona kama pungufu?raisi wenu ametoa ufafanuzi mpaka akapewa majina nusu?au aliambiwa tutaweka kwa batch?
   
 5. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Serikali ya wanafunzi wanasemaje?. Hapo lazma mjipange kuingia barabarani.
   
 6. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,370
  Trophy Points: 280
  Poleni sana.
   
 7. kinganola

  kinganola Senior Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua heslb ndo waliokuwa wanaingiza pesa za wanafunzi moja kwa moja hadi mwaka huu walipo amua kuziingiza kwanza chuo,sasa wenyewe ndio wenye idadi kamili ya nani anastahili kupewa pesa,sasa kutokana na hili lililotokea,itabidi ipitishwe sensa ijulikane idadi kamili ila haita saidia kwani wao wana majina yote kwenye data base yao,wamefanya usanii tu,ni wazi hawa hawakujipanga.
   
 8. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu chukueni hatua bodi safari hii wamechemka sana bora warudishe utaratibu wazamani!
   
 9. E

  Elai Senior Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Poleni sana. Sisi wanafunzi wa mwaka 2 na 3 Tumaini-Iringa hata majina machache bado hatujapata mpaka sasa. Utaratibu mpya wa bodi ulilenga kumaliza matatizo ya mikopo. Lakini imekuwa zaidi ya matatizo. Mungu wafungue viongozi wetu!
   
 10. kinganola

  kinganola Senior Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poleni sana nanyi pia,mjitahidi kuwafuatilia,Raisi wetu aliweka kambi pale wiki nzima ndo kikaeleweka.
   
 11. kinganola

  kinganola Senior Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana Rais wa Tumanini Makumira.Jamaa alikwenda Bodi siku ya Jumatano akitokea Arusha,alhamisi akajihimu Bodi,akaambiwa swala lake aende ijumaa atashughulikiwa,Ijumaa jamaa wakampotezea wakamwambia"LEO NI NYERERE DAY" njoo jumamosi,jamaa akajihimu jumamos,akaambiwa amsubiri Mkurugenzi yupo Wizarani,jamaa akashinda hadi ofisi zinafungwa hajasikilizwa.Akavunga DSM hadi jumatatu,alipokwenda akakutana na Mkurugenzi,Ikabidi asikilizwe.Alipomueleza kuwa Jamaa wa Tumanini Makumira wanataka Chao na leo hii wamegoma Kuingia Darasani,akaambiwa Arudi Arusha pesa itatumwa Jnne,jamaa akasema hatoi mguu Bodi ahadi akabithiwe Nakala za uthibitisho yakiwemo majina,wakamwambia subiri kesho,Jnne wakamzingua tena,alipo waambia hatoondoka bodi,Jumatano ndo wakamuandalia fasta na kumpa.Jamani wanachuo wa vyuo vingine,nendeni Bodi othewise hakitaeleweka.
   
 12. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  tatizo lenu makumira mnaleta uchungaji sana ndio maana wanawazoea.. Hamjawahi hata kuwapima joto hata mara moja, mligoma one hour polisi wakaja mkanyamaza... Zuieni barabara mpaka kwa mkuu wa wilaya hapo na mabango yenu mumpe ujumbe autume serikalini maybe watawasikieni.. Otherwise mtalia sana huku JF, facebook Na Chuoni bila majibu
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hakuna jipya hapo hebu mliopata jiungeni na wenzenu amabao hawajapata muingie road
   
 14. m

  mahuwi Member

  #14
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bodi hawazidi usanii wa elimu yenu, bora peas inachelewa mnapewa je elimu mtakayoenda wapa wadogo na watoto wetu kwa elimu ya kisanii itakuwaje?
   
 15. f

  fredduar Member

  #15
  Oct 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani ndugu hapo ni kuingia road na mabango au kuwatokea body mikopo kabisa. wanatuzingua wengi sio ninyi tu. hata sisi IAA tunakufa na njaa tu mpka leo hakuna hata fununu kuhusu pesa za field coz sie mwaka wa tatu semister nzima tuko field na pesa inatakiwa kutoka soon ili tunapaoanza field iweze kutusaidia wengine wanasafiri kwenda kazini, bado hawapewi pesa za kula wala mshahara kama wapo ni wachache sana. na hii mikopo tumepata watoto wa wakulima ingekuwa hakuna utaratibu huo cjui kama hata wengine tungekuwa chuoni leo hii, so hawa body ni kuandamana mpka pale TIDO then kuongea na mkurugenzi tu ndyo kitaeleweka. Viongozi wa serikali ya wanafunzi wanasumbiliwaga sana na kuonewa pale body, cha msingi ni kuzama dar kwa huku ni ngumu kuelweka kabisa jamani.sie wanajua tuko mbali so kwenda dar inatakiwa tujipange sana. suala la msingi kam akuna mizunguo ni kwenda kulala pale nje kwenye yale mawe yao mpaka mrudi na cheki ya pesa siyo majibu ya mdomo
   
 16. kinganola

  kinganola Senior Member

  #16
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe mahuwi unajielewa kweli?,hayo masiala yako peleka facebook tuondolee ujinga wako hapa,watu tunamachungu na mauzauza ya bodi,we unaleta masiala,mjinga wewe.
   
Loading...