Makufuli kwa level yako niwakati wa kuwa na "big plan" dar - moro highway"

Miimo

Senior Member
Apr 7, 2012
106
0
Wana JF
Ni siku nyingine tena tukitafakari hotuba ya budget ya mwheshimiwa Makufuli katika wizara yake.
Wengi tulitegemea kuona umahiri wa Makufuli katika kuwasilisha budget yake na kujibu maswali ya waheshimiwa wabunge na kwa hilo sinashaka na waziri Makufuli.

Nimejaribu kutafakari kuhusu swala la serikali kupitia wizara inayoongozwa na Makufuli kuwa na fikra mgando za kuendelea kupanua barabara ya Dar - Moro bila kuja na mawazo endelevu ambayo yatasaidia kupunguza msongamano na kupunguza ajali katika eneo la barabara hii. Mie napenda Kumshauri Makufuli kupitia wizara yake kuwa ni wakati sasa umefika kuanza kujenga barabara ya pili itakayounganisha kati ya Dar na Morogoro (200km). Hii itasaidia sana kuwa na barabara mbili kushoto kuelekea Moro na mbili kulia kuja Dar. Hii itaondoa ajali zote zinazotokea mara kwa mara katika kipande hiki na kupoteza maisha ya ndugu zetu na nguvu kazi ya taifa. Hili linawezekana, tena niabu kwa Taifa letu kwa kipindi cha miaka hamsini tumeshindwa kujenga hiyo barabara ya Dar-Moro katika hicho kiwango licha ya msokamano na ajali zinazotokea katika kipande hicho.

Dr. Makufuli, umetembea sana. Hivi hata hapo Ghana kama wameweza kutengeneza barabara mbili tofauti kutoka Accra hadi Ashanti (Kumasi Town) takribani 800km, kweli sisi tutashindwa kujenga kipande hiki cha Dar morogoro 200km? Mweshimiwa Makufuli naomba tu ujaribu walo kubroaden kidogo ubongo wako na kutumia shule yako katika hili.
Naamini inawezekana hata kwa mapato yetu ya ndani swala nikupunguza tu matumizi ya kawaida katika wizara mbalimbali hasa matumizi ya kawaida ya office ya waziri Mkuu. Mie najua serikali ya CCM ikishindwa kujenga hiyo barabara katika hicho kiwango, serikali yoyote ile itakayotokea out of CCM italiona hilo na kulitekeleza kwa haraka na kwa ufanisi wa hali ya juu.

Nakutakia kila la heri Pombe ukitafakari ushauri niliokupa kwa manufaa ya Taifa.

Nawasilisha.
 

pmwasyoke

JF-Expert Member
May 27, 2010
3,952
2,000
Usiache tukapewa ahadi hewa nyingine ya kufanya ulipendekezalo katika miaka miwili ijayo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom