Makubwa - Mbunge ashiriki chakula cha Krismasi na wafungwa

[COLOR=#FFFFFF said:
[/COLOR]Gosbertgoodluck
;3058903]Deo Filikunjombe tumekuelewa. Hata hivyo, kama alivyoshauri jamaa mmoja hapo juu, badala ya kutafuta cheap popularity kwa mwamvuli au jina bandia la MWANAHARAKATI nakushauri tumia muda wako mwingi kuwatumikia wananchi. Sifa zitakufuata tu hata uvunguni mwa kitanda. Ludewa ni wilaya tajiri sana kirasilimali lakini wananchi wake bado ni maskini wa kutupwa. Kwa hiyo una kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kubwabwaja bwabwaja humu JF na story za kijinga eti za kula na wafungwa kana kwamba ni jambo la ajabu wakati watu wengi tu wakiwemo viongozi wa dini wamekuwa na utaratibu wa mara kwa mara wa kuwatembelea wafungwa na hatusikii publicity yoyote ya kijinga kama ya kwako.

Ushauri wa bure:
(1) WANANCHI WA LUDEWA WANAHITAJI NYAVU NA SIYO
SAMAKI

(2) Ukitaka wananchi wakukumbuke basi watumikie vema. Waletee maendeleo na SIYO KUANDIKA JINA LAKO KWENYE MISAADA UNAYOWAPATIA. After all, HUO SIYO UUNGWANA KUWAPATIA MISAADA WANANCHI KAMA HAYO MASHUKA UKIWA UMEANDIKA MAJINA YAKO. KWANI WEWE NI KAMPUNI INAYOJITANGAZA!!!! USHAMBA MWINGINE BWANA!

Tafadhali Jamii Forums members, anayepost hii mada si Filikunjombe mnayemshambulia kama @Gosbertgoodluck@, ni mimi Candid Scope, nikiwa member hapa Jamii forums na hata katika baadhi ya blogs ambazo nimekuwa napeleka mada kadhaa.

Kwanza huyu Filikunjombe sijawahi hata kumtia machoni zaidi ya kuona picha zake na habari kwenye vyombo vya habari.
Na si Filikunjombe tu AMBAYE UTENDAJI WAKE NAUANIKA HAPA, naweka mada mbalimbali hapa mfano ni kama hizi zifuatazo:
  • Nilileta shughuli za mbunge Mchungaji Msigwa hapa lakini respond yake ilikuwa ni matusi, lengo lilikuwa kutangaza shughuli zake, lakini nimeamua kuacha ilivyo.
  • Nimeleta hapa mada kuhusu Mbunge wa Morogoro mjini, ambaye mada yake ingali live.
  • Nimeleta mada kuhusu Mbunge wa Musoma Vincent Nyerere
  • Nimeleta mada za Freeman Mbowe, Lema, Zito, Lukuvi, na nyingine nyingi tu.
  • Siko tayari kuwa vuvuzela wa chama fulani tu ila masilahi kitaifa.
  • Mimi sina mwelekeo wa kuyumbia upande mmoja tu kama bendera ielekeavyo upepo, niko huru katika kueleza yote mazuri ambayo wawakilishi wetu wanafanya kwa wananchi walio wachagua. Ndio maana nilichangia pia kumpongeza Mbunge wa Kilwa kwa kusaidia kuokoa maisha ya waadhirika na mafuriko Dar ingawa yeye si mbunge wa Dar.
Jambo la Msingi JF itikadi za siasa si chuki wala ubaguzi au matabaka, bali ni ushindani ambao huamsha na kuhimiza maendeleo ya nchi. Kwa vyo vyote ye yote ambaye anafanya mazuri kwa nchi yetu bila kujali tofauti za kiitikadi tumpongeze na kutangaza mazuri hayo ili kuwa kichocheo na mfano kwa wengine.

Kwa mtazamo wa wengi hapa naona ni itikadi za chuki, visa, na ubaguzi wa kiitikadi, kwa mwendo huu hatujengi utaifa ila tunajenga matabaka katika taifa tulilozoea mshikamano wenye kutujengea sifa ya utulivu na amani. Wachache wasitufanye tufarakane wenye hulka za uchochezi na ubaguzi wa kiitikadi wajirekebishe. Na hakuna binadamu aliye mkamilifu 100%, kila binadamu ana ukamilifu na upungufu wake, na tunachotazamia katika viongozi wetu katika mizani ubora uwe juu kuliko upungufu katika wajibu na utendaji.

Kama kuna jambo lisilokubalika katika mada hii lawama zote nipewe mimi badala ya kumshambulia mtu ambaye hata hajui kama kuna mada hii hapa au la na kubaki kusimuliwa na wanaoiona. Na siko tayari kushinda naimbia Chadema tu wakati vyama vyote vinajenga taifa, nikifanya hivyo nitakuwa nimepungukiwa na kitu fulani kisicho cha kawaida ubongoni
(lack something in common).

UKOMAVU NI KUPIMA PANDE ZOTE, KUEGEMEA UPANDE MOJA NI UDHAIFU.
 
Back
Top Bottom