Makubwa - Mbunge ashiriki chakula cha Krismasi na wafungwa

Kwani Candid scope ni mwandishi wa habari wa Deo Filikunjombe? maana kila upupu ukifanywa na Deo lazima utalipotiwa na Candid, au niyeye mwenyewe Deo anajiita Candid?
 
Ludewa,
Labda mimi sielewi vyema maana ya kufariji!!!
Hivi ni nini dhamira ya ujenzi na kuwaweka watu gerezani? Inawezekana sana ni kuwatenga na jamii............................

cha moto huenda upo sahihi. lengo la kupeleka watu gerezani kwanza ni kuwatenga na jamii, lakini lengo la pili ni kuwapa fursa ya kujipima upya nafsi zao kwa makosa waliyoyatenda uraiani, wajitafakari, wajute ja wajifunze ili wakirudi uraiani wawe watu wema.

gerezani si mahala pa mateso. wale wafungwa wanateseka.

lakini tatizo nilionalo mie ni watu kutokuwa na imani na wanasiasa. tendo hili la kuwatembelea wafungwa angelifanya askofu, msingelaumu. ila akilifanya mwanAsiasa mnalitazama with a microscopic eye. wanasiasa wajifunze. wajenge uaminifu.
 
Kwani Candid scope ni mwandishi wa habari wa Deo Filikunjombe? maana kila upupu ukifanywa na Deo lazima utalipotiwa na Candid, au niyeye mwenyewe Deo anajiita Candid?

Mimi si shabiki wa chama fulani kwa kuwa ninachoamini na kukipokea ye yote anayefanya mazuri kwa jamii yetu ni mfano wa kuigwa. Naliweka wazi hili Deo Filikunjombe ni mbunge kijana mwenye uchungu kwa nchi yake na asiyewaonea haya viongozi wanapofanya kinyume kwani anadiriki kutamka wazi mwelelkeo mbaya wa sera za CCM na kuwataka magamba yaanzie kujivua toka juu badala ya matawini.

Kumbuka viongozi wangapi wanatumbua maraha tu katika holiday hii wakati Deo Filikunjombe yuko kijiji cha porini kabisa mwambao wa Ziwa Nyasa mbali na nyumbani kwake kuwatembelea na kuwasaidia wapiga kura wake kijiji kilichosahauliwa miaka nenda rudi?

Wakati wengine wanastarehe kwenye fukwe za bahari na kwenye hoteli za kitalii yeye alicho nacho ameamua kuwapelekea wafungwa gerezani na kushirikia kula nao, hapa amebadilisha mtazamo wa wafungwa wengi kuliko kuwaachia polisi magereza wambao ni kazi yao .
 
This is a wise move that Deo has made. You need to be wise to understand that any citizen can be incacerated.Our jails are disgrace to human race because of the attitude of impunity among people who have either ill gotten wealth or position of leadership in our community.

Kuna mbunge mwingine Vincent Nyerere wa huko Musoma ameliona hili linalofanywa na Filikunjombe kwa kiwango chake kwani alishafanya mambo kadhaa kama kuwapelekea vifaa kadhaa magereza ya huko, huyo ni mbunge wa Chadema, kwani katika masuala ya kijamii tofauti za kiitikadi tuweke kando ili kupisha ukweli unaotendeka.
 
This is a wise move that Deo has made. You need to be wise to understand that any citizen can be incacerated.Our jails are disgrace to human race because of the attitude of impunity among people who have either ill gotten wealth or position of leadership in our community.

Kuna mbunge mwingine Vincent Nyerere wa huko Musoma ameliona hili linalofanywa na Filikunjombe kwa kiwango chake kwani alishafanya mambo kadhaa kama kuwapelekea vifaa kadhaa magereza ya huko, huyo ni mbunge wa Chadema, kwani katika masuala ya kijamii tofauti za kiitikadi tuweke kando ili kupisha ukweli unaotendeka.
 
bora angekula na watoto yatima na kuwafariji kwao wafungwa si kwa sababu ya uongozi mbaya wa kesi za kubambkikiwa? yeye angeenda kuwapa watoto yatima sawa kwani wameathirika labda kutokana na wazazi wao wakati wao hawana hatia

watu bwana! akila na wafungwa upupu! akila na yatima upupu! akila peke yake noma!

https://www.jamiiforums.com/jamii-photos/205969-picha-matukio-ludewa-filikunjombe-apitiliza-matarajio-ya-wengi-new-post.html
 
Sheria Zetu Zinasemaje? na kama huu Mchezo Ukiachwa kila Kiongozi aige haya basi watakuwa wengi na inabidi wawekewe zamu Bunge lina viti 300 na ushee Mwaka mmoja una siku 365 so Kila siku ni zamu ya Mbunge jala kutakuwa na raha kila siku hakuna atakaye jirekebisha na wale wapendao kule ndio watafanya makosa wakajazane huko kula raha...

Cha muhimu mazingira yaboreshwe tu jela iwe ni kumnyima mtu uhuru wake na si Mateso...kama ilivyo sasa hivi..

Jela nyingi tatizo kubwa ni Maji na Chakula ambacho kinatolewa na maafisa wanafisadi
 
Kwani yeye ni nani asilie gerezani mpaka uone ni makubwa au ulifikiri yupo juu ya sheria

Hao ndiyo wanasiasa wetu, mwisho wake atakwenda mpaka makaburini. kwani kwa msingi huo hata maana ya mtu kuwa gerezani kwa kutumikia adhabu kwa makosa yake ina msingi na fundisho kwa wale wa ulaiani. na hao askari magereza politicians sijui mwisho wao.
 
Huyu jamaa ni noma. bungeni alishawahi kumwambia spika kuwa wahujumu uchumi kwa ufisadi wanyongwe
kabla ya hapo alitaka kutumbukia ziwani akiwa kwenye mtumbwi anatoka kuwaona wapiga kura wake. Huyu jamaa anawaokoa sana magamba kwa mambo yake.
Hili alilolifanya ni jema sana kwa kweli.
 
Aache unafiki! Hii ni show up tu! Si ndo hao waliojiongezea posho kinyemela? Si ndo hao wanaowakandamiza wananchi walala hoi huku mafisadi papa na nyangumi wakiwaacha. Mwenye haki hajifunganishi na genge la wahuni.
 
Maadamu alishiriki kupitisha muswada mbovu na sasa ni sheria ya mabadiliko ya katiba, hata angegawa hela kitaa, hafai hafai hafai, sheria imejipanga kutupeleka gerezani, deo anatangulia huko gerezani anajidai kutufariji, alichaguliwa akawawakilishe wananchi kwenye chombo cha kutunga sheria ili apinge jaribio la kutunga sheria itakayokuwa kinyume na jamii, kuwatembelea wafungwa isingehusisha mlo wala misaada, ingekuwa ni baada ya kupambana ili kufuta sheria kandamizi zinazopeleka wananchi gerezani kwa hila, sijui mnamsifia deo kutekeleza wajibu upi kati ya majukumu yake ya kiuwakilishi.
 
Kula gerezani kama mfungwa ni ada ya wafungwa, lakini kwa mbunge kwenda kula sikukuu na wafungwa hii ni mpya katika historia ya nchi yetu, labda mwenzangu una kumbukumbu hapa nchini kiongozi aliyewahi kufanya hivyo, vinginevyo tumpe credit zake bila hiana.

Siku za hivi karibuni huyu mbunge amepata publicity sana ya vyombo vya habari; nahisi hii ni timing yake ya kuusaka uwaziri kwani amenusa kuwa mkweree karibu atafanya reshuffle ya baraza lake hivyo msijemkashangaa na jamaa yumo!!
 
Back
Top Bottom