Makubwa - Mbunge ashiriki chakula cha Krismasi na wafungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makubwa - Mbunge ashiriki chakula cha Krismasi na wafungwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 28, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mhe.Deo Filikunjombe

  MBUNGE WA CCM FILIKUNJOMBE ALA KRISMASI GEREZANI

  • Ludewa wana jengo zuri la mahakala lisilo na hakimu
  MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ametembelea wafungwa wa gereza la Ludewa na kula nao chakula cha krisimas pamoja na kuwapa misaada mbali mbali ikiwemo ya mashuka 200 na kuomba serikali kusaidia uboreshaji zaidi wa magereza hapa nchini. Mbunge Filikunjombe alitoa msaada huo jumatatu ya Krismas na kuelezea ziara yake katika gereza hilo kuwa ni kutaka kuwafariji wafungwa na mahabusu wa gereza hilo kwa madai kuwa ni wapiga kura wake na wanahitaji kufarijiwa zaidi.

  Akizungumza baada ya kutoka kula chakula na wafungwa na mahabusu hao ,mbunge Filikunjombe alisema kuwa zipo changamoto mbali mbali ambazo amepata kuziona katika gereza hilo kutoka kwa askari wake hadi wafungwa hasa katika uboreshaji wa nyumba za watumishi na gereza hilo zaidi.

  Kwani alisema kuwa gereza lipo kwa ajili ya kila mmoja hata kama mbunge ama kiongozi wa serikalini na kuwa iwapo wao kama wabunge wasiposaidia kupigia kelele uboreshaji wa magereza nchini ipo siku na wao wanaweza kufikishwa hapo. Hivyo alisema kuwa kwa upande wake mara baada ya kufika na kula chakula na wafungwa hao pia alipata nafasi ya kuwafariji na kuwasikiliza kero zao na kuwa moja kati ya kero ni juu ya kucheleweshwa kusikilizwa kwa kesi katika wilaya hiyo ya Ludewa ambayo mbali ya kuwa na jengo zuri la mahakama ila haina hakimu . Aliiomba idara ya mahakama nchini kusaidia kupunguza msongamano wa mahabusu katika gereza hilo kwa kutatua tatizo la uhaba wa hakimu wa wilaya katika wilaya hiyo .


  Kuhusu uchakavu wa nyumba za watumishi katika gereza hilo alisema kuwa nyumba nyingi za gereza hilo zimechakaa kutokana na kujengwa muda mrefu na tatizo la mchwa kuendelea kuwa kubwa eneo hilo. Pia mbunge huyo aliahidi kuwasaidia TV wafungwa wa gereza hilo pamoja na radio ili kuweza kupata haki yao ya msingi ya kupata habari na kuweza kujifariji zaidi wakati wakitumikia adhabu yao. Mbali ya misaada hiyo pia alikabidhi sabuni ,mafuta ,miswaki na dawa ya meno pamoja na kandambili kwa kila mfungwa na mahabusu wa gereza hilo huku akiwataka pindi wanapotoka gerezani kujiepusha na vitendo vya uharifu ambavyo vimewafikisha hapo.
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani yeye ni nani asilie gerezani mpaka uone ni makubwa au ulifikiri yupo juu ya sheria
   
 3. Mangandula

  Mangandula Senior Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 186
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hapo umeonyesha njia na wengine wafuate, jitahidi pia kwenda kula na wagonjwa hospitalini mwaka mpya.
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  badala ya kupiga makelele kuboresha magereza ni bora kama ungepigia makelele mfumo sheria na polisi ambao umekuwa ukitumika vibaya kubambikizia watu kesi na kufungwa bila makosa au kwa makosa madogomadogo ili hali mfumo huwa ukiwalinda mafisadi papa walioiacha nchi yetu kubaki mifupa tu!! wewe unatungwa sheria bungeni peleka hoja iundwe tume ya kuchunguza tuhuma za baadhi ya watu kufungwa kwa kesi za kubambikiziwa huku mafisadi papa wakitesa na kodi zetu na mali asili zetu, wengine wamefikia hata kuuza twiga, tembo, swala nk?? wewe jaribu tu kuua hata dikdik kwa ajili ya mboga ukamatwe uone cha mtema kuni!!!
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yule mzee wa mipasho ya kutetea posho za ujira wa mwiwa hatuoni anakopeleka posho anazotetea, na wiki hii amekaza misuli usoni kumlinda kikwete kwa kuwabamiza Maaskofu wanaowatetea wananchi, angekuwa anafanya kama anavyofanya mbunge wa Ludewa utetezi wake ungeleta uwiano wa anachotetea, lakini anakusanya tu kwa ajili ya kuja kuwarubuni wapiga kura kipindi cha uchaguzi kitakapowadia.

  Walao Mbunge huyu malupulupu ayapatayo bungeni anayatumia kwa wapiga kura wake na hawa wenye kuhitaji zaidi badala ya kumaliza kwenye starehe kama wabunge wengine.
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Amefanya jambo zuri sana na huu ni mfano mzuri wa kuigwa!
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kula gerezani kama mfungwa ni ada ya wafungwa, lakini kwa mbunge kwenda kula sikukuu na wafungwa hii ni mpya katika historia ya nchi yetu, labda mwenzangu una kumbukumbu hapa nchini kiongozi aliyewahi kufanya hivyo, vinginevyo tumpe credit zake bila hiana.
   
 8. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ameonyesha mfano mzuri wa kuigwa Nimemkubali sana
   
 9. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  safi ni jambo zuri hilo!
   
 10. Kardo Joseph

  Kardo Joseph New Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naam ni jambo jema kushiriki chakula na watu wenye makosa watumikiao adhabu gerezani! Kama nia ya Mbunge ni njema basi ni jambo la kuigwa lakini kama kutakuwa na hisia za kisiasa pia kutafuta umaarufu (Cheap popularity) basi haitajenga maana miongoni mwa jamii yenye mitazamo ya tofauti kisiasa.
   
 11. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa yuko tofauti sana, kazi nzuri sana
   
 12. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  ana hamu ya kufungwa tu huyo
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Da! hii heading niliielewa vibaya kumbe!!
   
 14. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Great new ideas.... Sio kutumia watoto yatima kila siku kwa ajili ya kujipatia umaarufu.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hata kama inaweza kutafsiriwa kama kutafuta umaarufu wa kisiasa kwa kiwango hiki amepitiliza kiwango kwani wabunge wengi wanatoa visingizio vya kujumuika na familia zao kipindi hiki cha sikukuu, na hata mkuu wa kaya alienda kustarehe mbuga za wanyama badala ya kule kijijini kwake Msoga.

  Tujue kuwa nafasi kama hizi wafungwa wanapopata fursa ya kuonana na viongozi wa wananchi na kujadiliana nao mambo mbalimbali ni moja ya funzo kubwa la kuwajali na muda wanaporudi wanakuwa wamebadilika na kuwa raia wema, ingawa kama si wote kwa vyo vyote kuokoa kondoo moja kati ya 100 waliopotea ni bora kuliko kukosa wote.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Labda mleta mada alikusudia uichangamkie kuisoma
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu soma vizuri kabla huja comment...........
   
 18. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Ingawa huyu jamaa anabelong to magamba,mi namkubali sana!
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mimi nilishamgundua muda mrefu upekee wake tofauti na wanamagamba wengine, ndio maana sioni haya kumwanika juani.
   
 20. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,216
  Trophy Points: 280
  Soma habari yote,sio unasoma kichwa cha habari tu.
   
Loading...